Nchi ina changamoto ya uwezo wa kujibu hoja kwa hoja. Hili ni tatizo kubwa sana

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,734
Kinacho endelea baada ya TEC kutoa Walaka ni refliction ya watanzania walivyo weupe vichwani,Ukiangalia tu hata humu Jf mtu anaweza kuja na Maada yake na kitakacho fuatiwa ni attacking binafisi na wala sio kujibu hoja.

Tusha shuhudia mara kibao hata huko Serikalini huwa watu wa kujibu hoja ni adimu sana na hoja zao huwa zinajibiwa na Police, au AK 47, au ndio UVCCM huitwa na kuanza kutishia badala ya kujibu hoja.

Hili tatizo lipo sana hata huko Makazini, ni triend ya nchi nzima.

Wanao jibu walaka wa Maaskofu hadi sasa naona matusi hakuna hata mmoja amekuja na Fact kuwapinga TEC, yaani swala la kujibu hoja kwa Tanzania ni sawa na kutafuta Bikira kwemye Wodi ya Wazazi.

Kwenye walaka sijaona sehemu mtu ali atackiwa, sijaona mahala Dini ya mtu alitajwa ila sasa wajibu walaka wote ni full attacking Maaskofu na Kanisa kwa ujumla.

Hii sio Jambo geni kwa Bongo, tuna shida sana linapo kuja swala la kujibu hoja kwa hoja, Hapo unaweza shangaa utatukaniwa hadi wazazi wako na watoto wako.
 
Kuhusu samaki, maji , siasa na dini. Mvuvi alimvua samaki, akamleta sokoni, mteja akamnunua.Kabla ya kumpika ikabidi amuoshe huyo samaki na maji, kisha akamuweka samaki kwenye sufuria, akaweka maji na kuanza kumpika. Maji yalipopu gua ,kabla ya samaki kuiva, akaongezea maji ili aive vizuri. Alipoiva akamuweka kwenye bakuli tayari kwa kuliwa. Kabla ya kumla samaki, mlaji ikabidi anawe mikono kwa maji.

Baada ya kula na kushiba, mlaji akashushia na glasi ya maji na kisha akanawa mikono kwa maji.Baada ya muda ,mlaji ikabidi aende kupunguza uzito. Alipomaliza akanawa kwa maji. Muda wote huo tangu kuvuliwa samaki, hadi kuliwa,maji na samaki wanatengana kwa muda kisha mazingira yanasababisha wanarudiana japo kwa muda.

Hii ni sawa siasa na dini. Hata wakati wa vita viongozi wa dini uwa wanaingilia kutafuta amani maana waangamiao ni waumini wao. Wakikaa kimya, waumini wao wakaangamia wakaisha, watawahubiri akina nani
 
DINI KWENYE ELIMU SAWA,NDIO MAANS WANAJENGA SHULE.DINI KWENYE AFYA ZA WANANCHI SAWA, NDIO MAANA WANAJENGA HOSPITAL. DINI KWENYE SIASA ETI NO NO NO NO NO KWANINI???? ILI UHUBIRIWE UELEWE, INABIDI UWE NA UELEWA MZURI( ELIMU) NA AFYA NJEMA. LAKINI PIA LAZIMA IWEPO AMANI. AMANI INATOKANA NA SIASA SAFI. HAPO DINI UTAITENGAJE NA SIASA.MBONA BUNGENI KUNA MAASKOFU NA WACHUNGAJI?
 
Back
Top Bottom