Nchi imeuzwa au viongozi wamelala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi imeuzwa au viongozi wamelala?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msheku, May 15, 2011.

 1. M

  Msheku Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Watanzania najua nikiwauliza hamjambo jibu ni lile lile hatakama mmeshinda njaa.

  JF members na Watanzania wenzangu tunayo mapungufu lakini kama wapo watanzania wanaotaka kusaidia watoke pale walipo basi tufanye hivyo, na kuwasaidia ni watu kama wewe mwenye mamlaka, na hapa hatumaanishi kupendelewa.
  Nazungumzia jambo nililofanyia utafiti na nimepata taarifa za ndani kabisa zenye uhakika 99.99% kuhusu kampuni ya JUBILEE INSURANCE Hapa tz ikiwakilisha kampuni kibao.
  Katika kampuni hii meneja wote na wakuu wa vitengo ni wakenya, hata zile nafasi ambazo kwakweli zilipashwa kuwa chini ya wa tanzania, wanafanya kila namna wapewe wakenya.

  1. Mkurugenzi Mtendaji mkuu- Ziporah Mungai - Mkenya
  2. mkurugenzi mkuu msaidizi- Vijay Mahrotra - Mhindi
  3. Meneja wa fedha na Mhasibu Mkuu- Ronald Nyamosi - Mkenya
  4. Meneja Madai (Claim Manager) - Philip Kilinzo -Mkenya
  5. Meneja Biashara Life - Peter Malinda - Mkenya
  6. Meneja Biashara Medical Insurance - Andrew Munyi - Mkenya
  7. Msimamizi Madeni (Credit Controller) - Jared Awando -Mkenya
  8. Mkaguzi wa Mahesabu ya ndani - Francis Ochieng - Mkenya
  9. Meneja Msaidizi Underwriting - Mary Kamene - Mkenya
  10. Meneja Utumishi (HRM) - SELINA IRAFAY - MTANZANIA

  Kibaya zaidi katika haya makampuni yanawatumia Meneja Utumishi na Utawala kama vibaraka wa kuwauza watanzania wenzao, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni moja ambaye ni Mkenya hivi karibuni alimwagiza HR meneja wa mojawapo ya kampuni ya bima kuwa wakenya wanaoletwa hapa wasipopata vibali vya kufanya kazi Tanzania, atakuwa hana kazi.

  Maswala haya inabidi yafanyiwe kazi haraka watanzania wenzangu wenye uwezo zaidi yangu, sisi ni wanyonge, watoto wa wazazi maskini, baadhi ya watu walizoea kusema watu hawasome kozi za bima, sasa tunasoma na kwa zaidi ya miaka minne bado tuko mtaani hatujapata kazi na mitaji hatunayo, tukiandika barua za kuomba kazi, hata hazijibiwi, wakenya wanapata kazi mshahara mzuri na kupewa nafasi ya kwanza, Ndo maana nauliza kama tz imeuzwa bei poa? au hili toleo la viongozi limeoza na rushwa na halitufai kwani wanaongea kwenye majukwaa tu angali sheria hawazisimamii. Hawa viongozi hawajishughulishi na maslahi ya watanzania kwa mwendo huu, hivyo ndugu zangu tushirikiane katika katika kutetea watanzania na rasilimali zetu.
  Karibuni
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Mhhhh! Inasikitisha kwa kweli. Kule kwa majirani zetu huwezi kukuta kampuni kama hii iliyojaza Wabongo katika nafasi karibu zote za juu.
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa ynagu alifanya kazi pale central glass. Walimsakama jamaa kuwa yeye ni Mtanzania nk mpaka akarudi zake Tanzania. Mbaya zaidi naye aliporudi Tanzaia akafanya application nyingi kwenye institutions hapa nyumbani bila mafanikio. Jamaa aliishia kuwa dereva wa daladala hadi alipopata zali flani sasa ni lecture kule Brown University.
  wakenya ni wabaguzi kupita tujuavyo! Ila pia Watanzania tuna sijui tuite ka uoga fulani! Pia baadhi sio creative! Akipata kazi tu basi hata hajali tena. Note ni bbadhi na sio wote!
   
Loading...