Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,100
- 1,956
Ama kweli upumbavu ni kitu kibaya sana. Tunatengeneza katiba ya nchi na watu wengine wanafikiri tunatengeneza katiba kwa ajili ya msikiti. Aliyewaambia kwamba watanzania wote lazima waishi kwa kufuata desturi za kiislamu ni nani? Kila mtu ana uhuru wa kuishi maisha anayotaka na kuamini anachotaka ili mradi havunji sheria za nchi na wala haingilii uhuru na wa watu wengine. Tanzania sio nchi ya kiislamu mpaka ijiunge na umoja wa nchi za kiislamu duniani! Kweli upumbavu ni mzigo kuliko hata ujinga. Mtu unashindwa kutofautisha masuala ya taifa na masuala ya dini yako, yaani unafikiri eti katiba ya nchi ni lazima iwe ya kiislamu, kwani ina maana watu wa imani nyingine hawana haki katika nchi hii?
Mtu aniambie: Msumbiji ni member wa oic ( for obvious reasons ngoja niiweke in capitals OIC isije ikaleta mtafaruku) ina mafanikio gani? Uganda je?