Nchi iko salama, hiki pia kinaweza kuwa tishio kwa usalama wa nchi

Kama amani imetamalaki hofu ya nn mara Kenya mara uberigiji mbona mmeanza kuhaha damu za watu zina walilia.
 
Damn we have bastards in this country!!..The level of disrespect to the people of this country is beyond recall.
 
Daah mleta mada Mungu akubariki kwa maono hayo, lakini tuombe Mungu hayatafika huko wenyewe watakujibu, umewaza mengi kwa manufaa ya nchi, uliyaona mengi kaa nayo, wenyewe wanasema We 'll Never be silent and loose Tanzania or turn into turmoil, never on earth macho yanawaangalia sana hata wale waliopo pale.God bless us, but why us.
 
Wee msukuma mleta mada umejikamuuuua mwenyewe mpaka kimba la mwisho limekutoka wakati ishu ni ndoogo tu...MWAMBIE BWANAKO AACHE UDIK UCHWARA AHESHIMU KATIBA NA AFUATE MAAMUZI YA BUNGE NA ATOE HAKI SAWA KWA WATU WANAOMKOSOA...zaidi ya hapo mutalialia mpaka mukome na kutafuta mchawi mpaka ubelgiji. Kwani musingempiga lissu risasi nani angeenda ubelgiji...#akatubufasta# mengine yatarudi kwenye mstari kama zamani.
 
Ushauri wako ni mzuri kulingana na upeo wako ulipoishia juu ya jambo hili.Lakini ungejiuliza kwanza umakini wa jamaa waliyemmiminia Lisu kitu.Je ujasiri huo waliupata wapi kwenda kufanya shambulio sehemu yenye ulinzi?Je ni wazowefu wa ushenzi walioufanya?Je kwanini hawajapatikana? Baada ya maswali haya ndipo ungejiuliza kuwa ni kwanini alipelekwa Nairobi na si Rwanda wala Uganda au sehemu nyingine yoyote.Pia umesema kuwa vyombo husika viwe jirani sana na hao unaowashuku,kwaufupi tu ni kwamba vyombo husika vipo kazini toka kuumbwa kwa Tanzania.Marekani kuna baadhi ya vyombo vyao ili uweze kupata nafasi ya mafunzo unapimwa asilimia za IQ yako na si makaratasi.Pia ifahamike kuwa wale watu wenye tabia ya Extrovert huwa hawapewi kabisa nafasi,bali wale wenye tabia ya Introvert ndiyo hupewa nafasi baada ya kukidhi viwango vya IQ. Mwisho niseme tu kauli hii;To every action there is an equal and opposite reaction.
 
Salaam....

Nchi yetu chini ya Amiri jeshi mkuu Dr Magufuli imekuwa salama na hali ya utulivu imekuwa juu sana kwa kipindi chote cha utawala wake. licha ya changamoto za hapa na pale kama vile mauaji ya Kibiti, uvamizi wa vituo vya polisi, na mambo mengine madogo madogo yenye kughasi usalama wa watu na mali zao ni ukweli kwamba nchi iko salama na wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu. Hongera sana Mheshimiwa Rais.

Naipenda nchi yangu, kwa miaka miwili sasa nimetokea kumpenda Mheshimiwa Rais na serikali yake na nishakula yamini ya kuwa mtiifu kwake na serikali yake milele. Hata hivyo ninayofuraha kuwasilisha mawazo yangu yafuatayo kuhusu usalama wa nchi kama ambavyo naweza kutoa maoni kuhusu siasa, utamaduni, nk.

SIASA ZA NCHI.
Hofu yangu kuu ni juu ya siasa za nchi miaka kadhaa ijayo, upinzani wa nchi unaweza kugeuka kuwa tishio kuu la kiusalama kama juhudi za kijasusi za kisiasa hazitachukuliwa.

TUNDU LISSU
Kapigwa risasi kaenda kutibiwa Nirobi, kuna maswali kadhaa ya kujiuliza...
1. Kwanini apelekwe Kenya sio nchi nyingine?
2. Ulinzi wake pale Nirobi hospital uliratibiwa na serikali ipi? ya kenya au Tanzania?
3. Kama ni Kenya, Kidiplomasia Tanzania na Kenya zikoje?
4. Kidiplomasia mtu anayeituhumu serikali ya nchi yake kumpiga risasi na kuhifadhiwa na Taifa jingine kwa kupewa ulinzi mkali ikoje?
5. Mahusiano ya Rais Kenyatta na Upinzani wa Tanzania yamejegwa katika misingi ipi? wanashirikiana katika mambo yapi?
Tahadhari hapa inahitajika, turejee jinsi watu waliowahi kuhatarisha usalama wa mataifa yao na hata kupindua serikali zao walikuwa na mahusiano kama hayo. Mobutu alipinduliwa na akina Kabila waliopata sapoti toka kwa mataifa rafiki ikiwemo Tanzania nk.

SAFARI YA UBELGIJI
Hapa yapo maswali kadhaa ambayo tunaweza kujiuliza maswali kadhaa.
1. Nani alipendekeza kupelekwa Ubelgiji?
2. Mahusiano ya Kenya na Ubelgiji kidiplomasia yakoje?
3. Kama ni Marafiki, kunauhusiano gani kati ya Lissu na kwenda Ubelgiji? kwanini Ubelgiji na sio Taifa jingine?
4. Tunajua mwenendo wake huko Ubelgiji?
5. Mazungumzo anayofanya na taasisi kubwa kubwa kama EU nk tunayafahamu? yamejikita kwenye nini na kwanini?
Tahadhari hapa ni juu ya mtu kuonekana kaenda kutibiwa ulaya kumbe kaenda kufanya mipango mikubwa ambayo hatma yake isiwe njema kwa Taifa.

SAFARI YA ZITTO UBELGIJI
Zitto kaenda Ubelgiji juzi na kafanikiwa Kumtembelea Lissu hospitalini, baadaye tunajua matamko yake na maandishi yake kwenye mitandao ya kijamii. Maswali Kdhaa tunaweza kujiuliza.
1. Tunajua ziara yake ililenga nini na hao watu aliokutana nao akina nani?
2. Kwanini Ubelgiji kipindi hiki ambacho Lissu anaumwa?
3. Zitto na Lissu walikuwa watu mahasimu, Urafiki wao umekolezwa na nini?
Tahadhari hapa ni juu ya Zitto kuwa sapota katika mambo yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi. Linapokuja suala la Connections na Funding Zitto sio mtu wa kumpuuza.

NINI KIFANYIKE?
Kunahitajika wataalamu makini wa kiusalama na kidiplomasia kuwaweka karibu sana watu hawa juu ya mienendo yao katika kipindi cha miaka 3 kuanzia sasa nk.

Mapambano ya Rushwa yasiishie katika taasisi za kiraia yaende mbali zaidi mpaka kwenye taasisi za kijeshi. Maafisa na wakuu wa vikosi na kamandi mbalimbali wanapaswa kuwekwa under Critical investigation juu ya masuala yao kiuchumi kuliko kipindi chochote, RUSHWA ndio hatare zaidi kuliko jambo lolote lile kiusalama.

Udahili wa vijana wa kujiunga na jeshi la Kujenga Taifa, Mgambo na mafunzo yoyote ya kijeshi yafanyike kwa umakini ikiwezekana yasitishwe hasa yale yanayofanyika na kuwaacha vijana hao mtaani. Mfano hakuna haja ya kuendesha mafunzo ya mgambo bila mpango wowote wa kuwaendeleza kiuchumi. Vijana wa JKT Wasajiliwe kulingana na malengo na uwezo wa nchi kiusalama, nachomaanisha hapa ni kupunguza uwezekano wa kuacha vijana wenye mafunzo ya awali ya kijeshi Uraiani wasiofahamika mienendo ya maisha yao. vijana wasomiwasomi wanaokwenda JKT wasirudi kwa wingi Uraiani, usajili wao uendane na uhitaji tu. utashangaa kijana kamaliza mkataba JKT january mwaka huu sasa hivi anasafiri safiri mara Nirobi, mara Uganda, Mara South Sudan jambo ambalo linazua maswali mengi.
kupunguza matukio yanayowafanya wapinzani kuonewa huruma na mataifa ya nje, hapa naeleweka vema.

Idara ya uhamiaji ifanye kazi vema na itazame hasa mienendo ya kusafirisafiri kwa vijana wengi kwenda nje ya nchi, mpaka wa Tanzania Kenya utazamwe kwa macho mawili mawili.

MWISHO nikumbushe tu kwamba DRC iko hoi kiusalama kwasababu ya Taifa la Ubelgiji. Kwangu binafsi ni Taifa hatari kuliko mataifa yaliyozoeleka vinywani mwetu. Naviamini vyombo vya Ulinzi na Usalama na naamini viko macho daima.

Mambo ni mengi kichwani nisiwachoshe kwaleo, siwezi kuwa na wazo lenye manufaa kwa Taifa nikakaa kimya otherwise kuna sehemu mahususi ya kuwasilisha maoni hayo. asanteni
Yaan wewe ni mpumbavu kama huyo unayemsifia, tutatumia manati kushughulika naye kama Daudi alivyoshughulika na Goliathi
 
haya maswala ni kuyaangalia kwa jicho la tatu sio tu tunakurupuka na kuanza kulaumu kwani sasa hivi kama nchi tuna maadui wengi ndani na nje hasa baada ya kuingia vita ya kiuchumi tujifunze kwa wenzetu wa Lyiba na Irak tuache tofauti zetu za kisiasa tuilinde nchi yetu kwani wanaouawa ni watanzania ndio maana kuna wengine kwa akili fupi wanasema nchi iwekewe vikwazo au tuje tupigwe mabomu
 
Mauaji ya polisi na raia wewe unayaita mambo madogo madogo? Wewe ni kiumbe wa ajabu sana. For your information Mungu alipomuumba mwanadamu alitumia utaalamu uliotukukakiustadi wa hali ya juu mno na kwa mfano na wake. Ktk hali a single blood she'd of a human being's touches God straight. Take care
 
God showed you His almighty when you failed to kill TAL again you have failed to assassinate mbowe and co instead mmemwaga damu ya innocent lady ambayo you will be required to pay for much more sooner than later
 
Unaleta uharo hapa eti ubelgiji ulitaka hyo zito asiende kumwangalia mgonjwa?nyie km babayenu amewazuia unafikir wengne wamezuiliwa km nyie.ww utakuwa kwnye kundi lile la wasiojulikana umekuja kupima upepo huku
Kumbe UADUI WA KISIASA huwa si wa KUDUMU aseee .... leo Zito na Lissu ni marafiki tena .... hadi wa kutembeleana ....

Obviously I now believe the TODAY'S DEVIL is really the TOMORROW'S ANGEL
 
Salaam....

Nchi yetu chini ya Amiri jeshi mkuu Dr Magufuli imekuwa salama na hali ya utulivu imekuwa juu sana kwa kipindi chote cha utawala wake. licha ya changamoto za hapa na pale kama vile mauaji ya Kibiti, uvamizi wa vituo vya polisi, na mambo mengine madogo madogo yenye kughasi usalama wa watu na mali zao ni ukweli kwamba nchi iko salama na wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu. Hongera sana Mheshimiwa Rais.

Naipenda nchi yangu, kwa miaka miwili sasa nimetokea kumpenda Mheshimiwa Rais na serikali yake na nishakula yamini ya kuwa mtiifu kwake na serikali yake milele. Hata hivyo ninayofuraha kuwasilisha mawazo yangu yafuatayo kuhusu usalama wa nchi kama ambavyo naweza kutoa maoni kuhusu siasa, utamaduni, nk.

SIASA ZA NCHI.
Hofu yangu kuu ni juu ya siasa za nchi miaka kadhaa ijayo, upinzani wa nchi unaweza kugeuka kuwa tishio kuu la kiusalama kama juhudi za kijasusi za kisiasa hazitachukuliwa.

TUNDU LISSU
Kapigwa risasi kaenda kutibiwa Nirobi, kuna maswali kadhaa ya kujiuliza...
1. Kwanini apelekwe Kenya sio nchi nyingine?
2. Ulinzi wake pale Nirobi hospital uliratibiwa na serikali ipi? ya kenya au Tanzania?
3. Kama ni Kenya, Kidiplomasia Tanzania na Kenya zikoje?
4. Kidiplomasia mtu anayeituhumu serikali ya nchi yake kumpiga risasi na kuhifadhiwa na Taifa jingine kwa kupewa ulinzi mkali ikoje?
5. Mahusiano ya Rais Kenyatta na Upinzani wa Tanzania yamejegwa katika misingi ipi? wanashirikiana katika mambo yapi?
Tahadhari hapa inahitajika, turejee jinsi watu waliowahi kuhatarisha usalama wa mataifa yao na hata kupindua serikali zao walikuwa na mahusiano kama hayo. Mobutu alipinduliwa na akina Kabila waliopata sapoti toka kwa mataifa rafiki ikiwemo Tanzania nk.

SAFARI YA UBELGIJI
Hapa yapo maswali kadhaa ambayo tunaweza kujiuliza maswali kadhaa.
1. Nani alipendekeza kupelekwa Ubelgiji?
2. Mahusiano ya Kenya na Ubelgiji kidiplomasia yakoje?
3. Kama ni Marafiki, kunauhusiano gani kati ya Lissu na kwenda Ubelgiji? kwanini Ubelgiji na sio Taifa jingine?
4. Tunajua mwenendo wake huko Ubelgiji?
5. Mazungumzo anayofanya na taasisi kubwa kubwa kama EU nk tunayafahamu? yamejikita kwenye nini na kwanini?
Tahadhari hapa ni juu ya mtu kuonekana kaenda kutibiwa ulaya kumbe kaenda kufanya mipango mikubwa ambayo hatma yake isiwe njema kwa Taifa.

SAFARI YA ZITTO UBELGIJI
Zitto kaenda Ubelgiji juzi na kafanikiwa Kumtembelea Lissu hospitalini, baadaye tunajua matamko yake na maandishi yake kwenye mitandao ya kijamii. Maswali Kdhaa tunaweza kujiuliza.
1. Tunajua ziara yake ililenga nini na hao watu aliokutana nao akina nani?
2. Kwanini Ubelgiji kipindi hiki ambacho Lissu anaumwa?
3. Zitto na Lissu walikuwa watu mahasimu, Urafiki wao umekolezwa na nini?
Tahadhari hapa ni juu ya Zitto kuwa sapota katika mambo yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi. Linapokuja suala la Connections na Funding Zitto sio mtu wa kumpuuza.

NINI KIFANYIKE?
Kunahitajika wataalamu makini wa kiusalama na kidiplomasia kuwaweka karibu sana watu hawa juu ya mienendo yao katika kipindi cha miaka 3 kuanzia sasa nk.

Mapambano ya Rushwa yasiishie katika taasisi za kiraia yaende mbali zaidi mpaka kwenye taasisi za kijeshi. Maafisa na wakuu wa vikosi na kamandi mbalimbali wanapaswa kuwekwa under Critical investigation juu ya masuala yao kiuchumi kuliko kipindi chochote, RUSHWA ndio hatare zaidi kuliko jambo lolote lile kiusalama.

Udahili wa vijana wa kujiunga na jeshi la Kujenga Taifa, Mgambo na mafunzo yoyote ya kijeshi yafanyike kwa umakini ikiwezekana yasitishwe hasa yale yanayofanyika na kuwaacha vijana hao mtaani. Mfano hakuna haja ya kuendesha mafunzo ya mgambo bila mpango wowote wa kuwaendeleza kiuchumi. Vijana wa JKT Wasajiliwe kulingana na malengo na uwezo wa nchi kiusalama, nachomaanisha hapa ni kupunguza uwezekano wa kuacha vijana wenye mafunzo ya awali ya kijeshi Uraiani wasiofahamika mienendo ya maisha yao. vijana wasomiwasomi wanaokwenda JKT wasirudi kwa wingi Uraiani, usajili wao uendane na uhitaji tu. utashangaa kijana kamaliza mkataba JKT january mwaka huu sasa hivi anasafiri safiri mara Nirobi, mara Uganda, Mara South Sudan jambo ambalo linazua maswali mengi.
kupunguza matukio yanayowafanya wapinzani kuonewa huruma na mataifa ya nje, hapa naeleweka vema.

Idara ya uhamiaji ifanye kazi vema na itazame hasa mienendo ya kusafirisafiri kwa vijana wengi kwenda nje ya nchi, mpaka wa Tanzania Kenya utazamwe kwa macho mawili mawili.

MWISHO nikumbushe tu kwamba DRC iko hoi kiusalama kwasababu ya Taifa la Ubelgiji. Kwangu binafsi ni Taifa hatari kuliko mataifa yaliyozoeleka vinywani mwetu. Naviamini vyombo vya Ulinzi na Usalama na naamini viko macho daima.

Mambo ni mengi kichwani nisiwachoshe kwaleo, siwezi kuwa na wazo lenye manufaa kwa Taifa nikakaa kimya otherwise kuna sehemu mahususi ya kuwasilisha maoni hayo. asanteni
Wewe ndo yule waziri wa madini? Vp ushamaliza likizo ya uzazi?
 
Back
Top Bottom