Nchi hii tunalisha mbwa chakula cha watoto

Nchi hii tunalisha mbwa chakula cha watoto

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,905
Miaka ya karibuni tumekuwa tukiwapa mbwa chakula cha watoto. Hili ni kosa kubwa mno labda kama unathamini mbwa wako zaidi kuliko watoto. Nchi maskini kama Tz tumeacha vipaumbele vya kujenga uchumi na kwenda kuiga mataifa makubwa namna wanavyofanya kutokana na kuwa na uchumi mkubwa.

Kukopa sio kosa au umaskini kwani hata USA wanakopa matrilioni benki ya dunia, China n.k. Tumekwenda kununua ndege za mabilioni kwa cash money, ambapo hata mashirika makubwa kama KLM na Lufthansa hukopa na kulipa polepole.

Tumeweka matrilioni mengi kwenye miundombinu kama vile bomba la mafuta na reli bila ya kushirikisha private sector, hata Marekani na pesa zao, miradi mikubwa kama hii inakuwa ni public-private-partinership yaani PPP.

Tumejifanya matajiri wa cash wakati hatuna kitu. Mkuu amejifungia ndani hajawahi fika mbali zaidi ya Ethiopia. Hata akina Trump, Angela Merkle, Ji Ching, Putin na wengine hutembelea mataifa mengine kuzungumzia uchumi na kutafuta wawekezaji. Mkuu wetu anafikiri ataweza mwenyewe, hata Ujeruman na China hawawezi wenyewe. Kikwete alitafuta wawekezaji wengi sana na alijua huwezi kulisha mbwa chakula cha watoto.
 
Ni uhuru wake na hela zake, kuna watu hawagharamii mbwa kabisa ila bado wanatumia fedha kwenye vitu ambavyo havina ulazima na vya gharama kubwa kuliko hata kulisha mbwa, kama safari za nje za gharama, magari mbalimbali ya gharama kubwa, pombe za gharama kubwa, nguo za gharama kubwa ambazo hukuta anaivaa mara moja tu.

Halafu kuna watu wanakufa kwa njaa, wanatembea uchi, wanashindwa kumudu gharama za matibabu

Ndio Dunia ilivyo, jifunze tu namna ya kuikabili na sio kulaumu maana hao watoto masikini ni responsibility ya waliowaleta Duniani
 
Back
Top Bottom