Nchi hii imenichosha kabisa

Jamani samahanini sana, ni uchungu tu ndio ulioniponza!
 
Ukitaka serikali na wahusika wa huo uwanja waje haraka hapo' piga simu na uwaambie kuwa kuna maandamano makubwa sana
ya wafuasi wa vyama vya upinzani na wanafunzi wa vyuo hapa ndani ya uwanja wa JK nyerere. utaona within 5 mns watakuwa
hapo na mabom,bunduki,maji ya kuwasha,virungu nk. Lakini zaidi ya hapo hesabuni imekula kwenu daima
 
Ndg zangu hapa ndipo CCM ilipoifikisha Nchi ye2. Unajua kwa Nchi yoyote ambayo Viongozi wake wa ngazi za juu, kama Rais na wasaidizi wake watakuwa hawana msimamo ni dhahiri nchi itayumba kwa kila eneo! Ndio maana umeona hata sisi wananchi tumelazimika kuharalisha Rushwa ili kurahisisha matakwa yetu, Viongozi wa chini mf. Watendaji wa kata na vjj kujifanya Miungu watu, Wakuu wa Idara mbalimbali za serikali kujiamini kupita kiasi hata kama wanakosea, Polisi kuua watu ovyo, nk, haya na mengine mengi ni matokeo ya Siasa mbovu. We unavyoona kwa nchi kama Tanzania 'nani anamwogopa nani?' Hii yote ni sababu ya serikali kukosa msimamo.
 
Inapotokea shida kama hiyo, kila mtu anatakiwa kuwajibika kutokana na nafasi yake na kazi yake. Ina maana kuwa hata abiria hao nao ni wahanga wa mabomu hayo kwa njia fulani. Kinachotakiwa kufanyika ni wao kupatiwa taarifa kamili kutoka kwa anayehusika na usafiri kuhusu hali hiyo. Kusingizia tu chanzo cha tatizo ndio mwanzo wa kutokuwajibika na uzembe kuenea.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…