Nchi haina mipango thabiti?

RealTz77

JF-Expert Member
May 18, 2009
738
40
Kwa mara nyingine tena kama kawaida ya nchi hii janga likitokea ndio tunaanza kuangalia nani kasababibisha na kuweka sera za zima moto, zisizodumu. leo hii kulipuka kwa mitungi ya gas katika maduka kwanini itokee?hawa wauzaji wa gas wanapewa training ya kuhandle milipuko?
Na watu wa leseni wanaangalia kitu gani ili kumpa mtu afanye biashara hiyo? Jijini Dar sasa kila kona ni mitungi ya gas, hata pembeni ya majiko ya chips etc kuna jirani anauza mitungi jsmsni, standards ziko wapi?mambo yanaenda kiholela tu, tunafukuzana majanga wakati tungeweza kuyawekea mikakati.hapa kama kawaida tena je ni watawala au na wananchi pia?

Ni mwananchi gani alienunua au anaetumia gas na kabla ya kufanya hivyo alipata japo katraining kadogo?aambiwe ipo na pressure gani, na inaweza kulipuka vipi! ikae umbali gani na moto wazi(open flame)! nini cha kufanya incase moto unatokea!mtungi gani bora!wasiliana na wapi incase utasikia au kuhisi unavuja? tunaenda tu kama tumekatwa vichwa? watu wengi sana tunatumia gas nyumbani, im sure inakuja disaster ya kutisha kama haya mambo yasipozingatiwa.

Mdau mkubwa wa kufanya hivi ni makampuni ya gas, na kusimamiwa na local governors! simple! hivi sasa uliza hata takwimu ni watu wangapi wanatumia gas majumbani, hutapata,zinakaa ktk mazingira gani hutapata! sasa hii nchi ya Tanzania au gheto la Tanzania?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom