Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
NCCR yadai CCM wameiba kaulimbiu yao
CHAMA cha NCCR Mageuzi kimeitaka CCM kuacha kutumia kaulimbiu ya Pamoja
Tutashinda wakati wa kuhamasisha uchangishaji wa fedha za kampeni zao kwa madai
kuwa kaulimbiu hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kampeni za NCCR za uchaguzi wa mwaka
2010.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa NCCR Mageuzi, David Kafulila alisema chama hicho kinaomba CCM isitishe
mara moja kutumia kaulimbiu hiyo na kubuni kaulimbiu yake kwa kuzingatia Katiba na
sera za CCM.
Kafulila alisema kuwa kaulimbiu ya Pamoja Tutashinda ilipitishwa na Halmashauri
Kuu ya NCCR katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre Desemba 5
mpaka 6 mwaka jana kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2010.
Baada ya kaulimbiu hiyo kupitishwa, ilizinduliwa na Mwenyekiti wa NCCR Taifa James
Mbatia, Desemba 19 mwaka jana kwenye Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma.
Hii ni kaulimbiu iliyopitishwa kwa kuzingatia misingi na itikadi yetu ya
Demokrasia ya kijamii iliyoainishwa kwenye Katiba yetu. Tunapenda kuutaarifu umma
kuwa chama kiliagiza vifaa vyote kwa ajili ya kampeni za uchaguzi 2010 vichapwe
vikiwa na kaulimbiu hiyo, alisema Kafulila.
Kwa mujibu wa Kafulila, NCCR Mageuzi ilishaanza kutumia kaulimbiu hiyo tangu
Desemba mwaka jana katika mikutano yake iliyofanyika katika majimbo ya Kigoma
Kusini, Kigoma Mjini, Kigoma Kaskazini, Muhambwe, Kasulu Magharibi, Kasulu
Mashariki na Buyungu na hadi sasa wanaitumia.
Pia kaulimbiu hiyo ilitumika hivi karibuni katika mkutano uliofanyika katika
viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe ambapo waandishi wengi wa habari walishuhudia
ikitumika wakati Mbatia alipotangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe katika
uchaguzi wa 2010.
Akizungumza na HabariLeo kwa njia ya simu jana, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba
alisema kaulimbiu ya CCM kwa ajili ya kampeni za uchaguzi 2010 inasema Ushindi ni
Lazima na kuwataka NCCR Mageuzi kwenda mahakamani kama wanaona imeibiwa.
Source: Habari Leo