NCCR wapinga mgao wa Majimbo UKAWA

NCCR wapinga mgao wa Majimbo UKAWA

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
360
Reaction score
525
Nimeattach gazeti lenye tamko la chama cha nccr mageuzi wilaya ya Tarime kikipinga mgawanyo wa majimbo ndani ya Ukawa.

Ni dhahiri kuwa kuna tatizo kubwa ndani ya ukawa na viongozi wetu hawawi wakweli kuhusu kinachojiri ndani ya vikao, wanachoeleza kwa umma kinatofautiana na uhalisia.

Ni wakati sasa viongozi wa ngazi za Taifa wakawa wanaratibu mambo yao na viongozi wa ngazi za chini. Unafiki unaofanywa na viongozi ngazi ya Taifa hautasaidia kuwa na muungano imara, maana hadi sasa kuna sintofahamu na kujenga juu bila kuwa na msingi mzuri ni sawa na kujenga nyumba yenye paa zuri bila kuwa na msingi imara.
===============

06 MAY 2015
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha NCCR-Mageuzi wilayani Tarime, imepinga uamuzi wa umoja wa vyama vya upinzani unaofahamika kama Ukawa wa kukipa Chadema hadhi ya kusimamisha wagombea katika asilimia 50 ya majimbo nchini.

Imedai kuwa, kwa kufanya hivyo ni sawa na kuibeba Chadema na kuviua vyama vingine vya upinzani.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Tarime, Nelson Chacha Makaranga, Katibu wake, Julius Andrea na kushirikisha baadhi ya wajumbe kutoka wilaya za Rorya na Serengeti, mkoani Mara.

Wakitoa maazimio hayo katika kikao hicho, walisema kwa pamoja wanapinga taarifa inayodai Chadema imejichukulia 114 kati ya 227, huku CUF kikigawiwa majimbo 80 sawa na asilimia 35, NCCR majimbo 33 sawa na asilimia 15, na NLD ambacho haikuoneshwa idadi ya majimbo yake.

“Tujiulize, kama wakishinda asilimia 50 ya majimbo yote si ndio watakuwa na wabunge wengi bungeni na kuchagua Waziri Mkuu kutoka chama chao? Sisi wa NCCR-Mageuzi Tarime tunaazimia kupinga. “Tunaamini kwa staili hii wenzetu wanataka kutuburuza na kukwamisha juhudi za vyama vingine vya siasa kukua.” Ilikuwa sehemu ya maazimio ya kikao hicho.

Wajumbe hao walitoa mfano wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana 2014 NCCR Mageuzi kiliweka Wagombea katika Vijiji vya Nyarutu, Mjini Kati, Nyabichune na Nyangoto Nyamongo, lakini Chadema nao waliweka wagombea wao na hivyo kukiuka makubaliano ya Ukawa, hali iliyochangia kushindwa kufanya vizuri katika maeneo hayo.

Maazimio hayo yaliwasilishwa kwa Katibu Mwenezi wa NCCR Mageuzi ngazi ya Taifa, Faustin Sungura (pichani), ambaye mara baada ya kuyapokea, alisema: “Nimepokea Mazimio yenu haya ambayo hata mimi nimeona yana Hoja za Msingi na nitayafikisha katika Uongozi wa Juu wa Chama chetu na kufanyiwa kazi , ili kuweka wazi muungano huu wa UKAWA usiwe wa kuvihujumu vyama vingine Maazimio haya ya Tarime tutayapeleka katika Vikoa vya vyama vingine vya Upinzani ili kuweka Wazi Hoja yenu hii.”

Chanzo:
Habari Leo
 
Mkuu umenena ni kweli kuna haja kabisa
Ila sijui nisemejehili la kugawana majimbo mimi silihafiki hata kidogo
Kuna jambo naliona mbele kuhusu kugawana majimbo
 
ni kweli usemacho ushirikiano unatakiwa kuanzia chini....
 
Nilisema mwanzo huu muungano haupo kwa ajili ya kusaidia wananchi ni muungano wa wataka madaraka tu, ndio sababu wanafukia kila shimo bila maelezo mradi tu waonekane hawana tatizo ndani, lakini ukweli haujifichi ndani ya ukawa wao kwa wao pia hawaaminiani,

hapa nawaambia mwisho wa ukawa itakuwa siku ambayo chama chochote kitateuwa mgombea urais kwa nafasi hiyo, hapo ndio wamekaa kutegeana kwa sababu wote ni wapenda madaraka
 
ni kweli usemacho ushirikiano unatakiwa kuanzia chini....
Ni kweli kabisa, lakini pia tuangalie hali ya chama hicho wilayani Tarime ikoje? Nashawishika kuamini kuwa tamko hili lina msukumo toka nje ya UKAWA. Ningewaelewa zaidi kama tamko lingetoka, kwa mfano, kwenye moja ya majimbo mkoani Kigoma siyo Mara. Huko walijifia Marando alipoondoka.
 
NCCR mageuzi wanajua taratibu za kuzifuata kungekuwa na matatizo wengefuata taratibu za kichama.

Hayo mapingamizi ya kwenye magazeti ni ya magazeti,yataendelea kuwa ya magazeti na yataishia kuwa ya magazeti hivyo hivyo.
 
Kazi ya kuitoa CCM madarakani ni ngumu kama kumuondoa shetani duniani. Imejaa vikwazo, majaribu na kukata tamaa kwa baadhi ya washiriki.
Kila jambo lililo jema lazima likutane na vikwazo na hao CCM sio kuwa wameugua Polio kwamba watakaa tuu kuangalia wanavyo achia madaraka
 
Ni Mungu ndiye anatuepusha na matatizo yatakayotokana na UKAWA. Mungu ajua kila kitu cha jana , leo na hata kesho. Mungu anaona ni bora CCM kuliko gilba za CHADEMA na wale anaotaka kuwafundisha gilba hizo.
 
NCCR mageuzi wanajua taratibu za kuzifuata kungekuwa na matatizo wengefuata taratibu za kichama.

Hayo mapingamizi ya kwenye magazeti ni ya magazeti,yataendelea kuwa ya magazeti na yataishia kuwa ya magazeti hivyo hivyo.
Jifarijini sana tu lakini muwe wangalifu msije kumbuka shuka alfajiri.
 
Mimi ni chadema dam dam na kadi yangu ni namba 2308533,
Kitu kitakacho ivuruga ukawa ni UROHO WA MADARAKA ngazi ya ubunge na udiwani. Haiwezekani mimi mchadema niliyetymikia chama miaka 8 leo eti ukawa imteuwe kiongozi wa nccr kuwa mgombea wa udiwani kwenye kata ya ngu.

Rai yangu:
Chadema makao makuu simamieni hili jambo kwa umakini mkubwa kuondoa mkanganyiko huu.
 
Nimeattach gazeti lenye tamko la chama cha nccr mageuzi wilaya ya Tarime kikipinga mgawanyo wa majimbo ndani ya Ukawa.

Ni dhahiri kuwa kuna tatizo kubwa ndani ya ukawa na viongozi wetu hawawi wakweli kuhusu kinachojiri ndani ya vikao, wanachoeleza kwa umma kinatofautiana na uhalisia.

Ni wakati sasa viongozi wa ngazi za Taifa wakawa wanaratibu mambo yao na viongozi wa ngazi za chini. Unafiki unaofanywa na viongozi ngazi ya Taifa hautasaidia kuwa na muungano imara, maana hadi sasa kuna sintofahamu na kujenga juu bila kuwa na msingi mzuri ni sawa na kujenga nyumba yenye paa zuri bila kuwa na msingi imara.
Wee kijana usiwe na akili za kushikiwa!!

NCCR Tarime kupinga ndiyo unapakazia NCCR nzima?!

Kwanza hao waliopinga wana ushawishi gani NCCR?! Kumbuka kila mwanachama ana haki ya kuunga mkono au kupinga lakini mwisho wa siku mawazo ya walio wengi yatashamiri!!!
 
Gazeti lenye ni Uhuru...siku zote lipo kwa ajili ya propaganda za CCM
 
Chanzo HabariLeo..!!!

Ningeshangaa sana iwapo chanzo hiki kingeunga mkono juhudi za UKAWA kugawana majimbo ili kuwezesha chama chakavu kuondoka madarakani. Tumieni kila propaganda ili kuidhoofisha UKAWA kinyume na hivyo, mtaondoka mwaka huu taka msitake..!!!

Sasa kama kunawatu wanastahili pongezi za dhati ktk kufikia makubaliano haya ni Chadema,Ni ukweli uliowazi kwa jinsi Chadema walivyofanya harakati za kisiasa tangu mwaka 2010, walistahiki asilimua 75 ya majimbo yote Tanzania nzima. Sasa maadam ktk kuungana ni lazima ukubali kusalimisha kilicho chako kwaajili ya wengine then hakuna anayelalamika.

Nyie andaeni wahuni na kuwavisha mashati na Magwanda ya vyama vya UKAWA ili waonekane ni wanaukawa wanaopingana na viongizi wao. Ninahakika huyo mliyemnukuu akiambiwa atoe majibu ya uchaguzi serikali za Mitaa kwa hapo Tarime, hana.!!!! Akiambiwa ataje viongozi wa chama chake kwa mkoa wa Mara hawajui..!!! Halafu ati anakuja kupinga Mgawanyo wa majimbo kwa wana UKAWA kwa hoja za kumezwa na kupunjwa..!!!!! Hivi pale Bungeni Nccr wako wangapi? Mbona hatujawahi kusikia huyo jamaa akilalamika kumezwa kwa Nccr kwasababu za uchache wao? Mbona hapo awali Chadema waliunda kambi ya upinzani peke yao na Wapinzani hawakuwamo. humo na huyo jamaa katu hajawahi kutanua mbavu zake kupinga kupunjwa kwa wabunge wa chama chake.? HIVI MGUU WAKO NI SAIZI 30 UNAG'ANG'ANIZA KUVAA SAIZI 70!!!!!

Mtupishe na propaganda zenu uchwara hapa!

BACK TANGANYIKA
 
Mkuu umenena ni kweli kuna haja kabisa
Ila sijui nisemejehili la kugawana majimbo mimi silihafiki hata kidogo
Kuna jambo naliona mbele kuhusu kugawana majimbo
Lakini NCCR mnalalamika nini? CHADEMA walishapotea pale walipoanza mgogoro na ZITTO na ndiyo maana wakaamua kuotesha Mbegu mpya ya CHADEMA HYBRID wakaiita UKAWA . NCCR mnatumiwa tu kama Karai la zege mwisho wa siku mtatupwa tu.
 
Ni Mungu ndiye anatuepusha na matatizo yatakayotokana na UKAWA. Mungu ajua kila kitu cha jana , leo na hata kesho. Mungu anaona ni bora CCM kuliko gilba za CHADEMA na wale anaotaka kuwafundisha gilba hizo.
Mungu wa kweli hawezi akamuona ni bora mwizi(CCM)wakati anajua kuwa mwizi adhabu yake ni kuchomwa moto kama mzinzi na mlevi,labda mungu shetani ndiye anae weza kuona CCM ni bora kwa kuwa wanacheza kwenye anga moja.
 
Back
Top Bottom