EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
BAADA ya Chama cha NCCR-Mageuzi kumfukuza uanachama mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila sasa kinasuasua kulijulisha Bunge kwa barua kuwa mbunge huyo kijana siyo mwanachama wa chama hicho.
Mwananchi pia limebaini kwamba, Kafulila pamoja na wenzake bado hawajakabidhiwa barua za kufukuzwa kwao na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, uamuzi ambao umepata upinzani mkubwa kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali nchini.
Jana viongozi wa NCCR Mageuzi walipoulizwa walitupiana mpira kuzungumzia suala hilo, ikiwa ni wiki moja tangu Nec ya chama hicho kumvua uanachama Kafulila kutokana na kile kilichodaiwa ni kosa la kuzungumza siri za ndani za chama katika vyombo vya habari.
Kafulila alifukuzwa uanachama pamoja na wenzake watatu, akiwemo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka jana, Hashim Rungwe. Katibu Mkuu wa chama hicho Samwel Ruhuza alisema huenda barua hiyo ilipelekwa katika ofisi za Bunge jana huku akishikwa na kigugumizi kufafanua zaidi na kuomba atafutwe Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Faustine Sungura. "Sijui wameshapeleka…, itakuwa wamepeleka bungeni, inawezekana ikawa wamepeleka leo (jana), ila sitaki kufafanua zaidi wala ku ‘confirm' (kuthibitisha) kwa sababu nipo safarini," alisema Ruhuza.
Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Sungura alisema hafahamu chochote kuhusu suala hilo huku akimrushia mpira Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, George Kahangwa. Kahangwa alipoulizwa alisema hawezi kujibu lolote na kutaka iulizwe ofisi ya bunge. "Iulizeni ofisi ya bunge kama barua hiyo wameshaipata ama laa…, unajua hatupendi kuzungumza masuala haya tena, hivi sasa mkitaka maelezo waulizeni wahusika wenyewe, kama chama tumeshafanya kikao na kutoa uamuzi," alisema Kahangwa.