NCCR nayo mbogo sakata la Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR nayo mbogo sakata la Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280

  NCCR nayo mbogo sakata la Dowans

  Imeandikwa na Selemani Nzaro; Tarehe: 4th February 2011 @ 23:40


  CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimepinga utaratibu wa Serikali wa kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC).

  Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa uzembe uliosababishwa na baadhi ya viongozi wasiokuwa waadilifu usisababishe maumivu kwa Watanzania.

  Mbatia amesema kinachotakiwa kufanywa na Serikali ni kwanza kuwatambua viongozi waliosababisha nchi kuingia katika matatizo haya, pili kuwaadhibu kwa kubinafsisha mali zao zote na kisha kuwapeleka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake ili kukomesha wale wote wenye tabia kama hizi na pia kuhakikisha kuwa tatizo hili halitajirudia tena.

  “Lazima Serikali ituhakikishie kuwa nchi haitakuwa Tunisia, Misri au Yemen kwa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote waliolifikisha Taifa hapa.

  Ikiwa Serikali itashindwa kuzuia malipo haya, hali itakuwa mbaya sana” amesema Mbatia. Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya chama hicho, David Kafulila amepewa mikoba ya
  kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuishinikiza Serikali kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuiingiza nchi katika matatizo.

  Mwenyekiti huyo amehoji kuwa kwanini Serikali iharakishe katika kuilipa Kampuni hewa ya Dowans mabilioni ya fedha wakati walimu wanaodai malimbikizo ya mamilioni ya fedha bado hawajalipwa?

  “Kwanini wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa mafao yao lakini Dowans inalipwa kwa haraka?, Wanafunzi wa elimu ya juu je, mbona wanaandamana kila siku hawalipwi” amehoji Mbatia.

  Kuhusu Katiba Chama hicho kimesema matatizo yote yanayoifika nchi ni kwa sababu ya Katiba.

  Kama nchi ingekuwa na Katiba inayoendana na hali halisi ya nchi kusingekuwa na matatizo ambayo yanawatesa Watanzania. Chama hicho pia

  kimemwomba Mbunge wake wa Kasulu Mjini kupeleka hoja binafsi bungeni pindi vikao vya Bunge vitakavyoanza.

  Katika hoja hiyo NCCR-Mageuzi inaliomba Bunge kutunga sheria ya kueleza utaratibu utakaotumika wa kupata Katiba mpya.

  Kuhusu suala la ushirikiano wa vyama Mbatia amesema msimamo wa chama chake ni kutaka vyama vyote vya upinzani vinakuwa na uwakilishi katika kambi ya upinzani.

  “Kinachofanywa na Chadema hakikubaliki kwa sababu hata wao walishirikishwa katika Serikali kivuli ya upinzani bungeni na Chama cha Wananchi (CUF).

  Lazima vyama vyote vishirikishwe katika kambi ya upinzani,” amesema Mbatia.

  Chama hicho pia kimezungumzia migogoro vyuoni na kuitaka Serikali kuwalipa wanafunzi stahili zao haraka ili wawe na utulivu darasani.

  Amewashangaa wabunge kutumia mabilioni ya fedha katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl wakati kuna ukumbi wa Bunge upo Dodoma.

  “Mabilioni ya fedha waliotumia katika mkutano wa wabunge yanatosha kuwalipa wanafunzi wa elimu ya juu, kwanini hawakutumia ukumbi wao wa Pius Msekwa uliopo Dodoma” Amehoji Mbatia.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  PHP:
  "Kwanini wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa mafao yao lakini Dowans inalipwa kwa haraka?, Wanafunzi wa elimu ya juu je, mbona wanaandamana kila siku hawalipwi" amehoji Mbatia
  Hili ni swali ambalo Pinda anafaa aulizwe Bungeni.kwenye kipindi cha kumuuliza maswali tusikie atakavyojikanyaga.......................kanyaga...................
   
Loading...