NCCR Mageuzi na wafuasi wake, Mbatia anatakiwa kuwa makini sana na waliyo karibu naye

Dr Shekilango

Senior Member
Dec 30, 2013
192
117
Moja ya vyama vikubwa vya sisasa hapa Tanzania ni NCCR Mageuzi, hiki chama pamoja na ukongwe na ukubwa wake kimeshindwa kulea Vijana na kuwaandaa kuwa viongozi wazuri hapo baadaye kama ambavyo tumekuwa tukiona kwenye vyama vingine. James Mbatia ni miongoni mwa Wanasiasa wa muda mrefu na mwenyekiti wa chama hicho ila ameendelea kuwa mwenyewe kama icon ya chama huu ni udhaifu mkubwa sana kwa kiongozi kushindwa kulea wengine ni ubinafsi pia, Moja ya Icon katika chama hicho kwa muda wa miaka kama sita, mitandaoni na kwenye media ni aliyekuwa mwenyekiti wa Vijana Nicolas J Clinton na baadaye wamekuja wengine kama Edward Simbeye na walikuwepo wengine pia wazuri lakini chama hiki kimeshindwa kuwalinda, kuwalea na kuwaona wa thamani, hakuna kabisa program ya kuwalea Vijana zaidi ya kuwatelekeza tu, hii ni hatari sana kwa chama.

Kwa miaka sita Mbatia na Clinton ndo waamekuwa icon ya chama kabla ya ujio wa wanachama wengine, nimsikitie Clinton sana na vijana wengine ndani ya chama hicho kwa sababu hawana thamani kabisa zaidi ya kuonekana maskini, Clinton ni mwanasiasa kijana, kwa taarifa nilizonasa ni kwamba anaondoka ndani ya chama hicho hivi karibuni, hii ni baadaya Vijana wengine kuandika barua za kupumzika akiwemo Binti Kiffu mwansiasa kijana pia, baadaya ya mabadiliko dhaifu ya uongozi wa Vijana na kuonekana kundi jipya la wanachama wanajaribu kuwafutilia mbali viongozi wote wa zamani akiwemo Clinton na makada wengine, wakati huo Mbatia ajiandae kufurushwa kwa aibu kwa sababu ya kundi hatari kwenye chama hicho likiongozwa na Kamishina wa DAR na Mgombea Urais wa chama hicho mwaka 2020.

Mbatia anatakiwa kuwa makini sana na waliyo karibu naye, wapo Viongozi wanavujisha siri za chama kwa mademu zao na mademu zao wanasema wazi, vya kale ni dhahabu, Mbatia acha kuwatelekeza Vijana wako walee kama ulivyolelewa wewe na leo umefanikiwa kwenye siasa, unaowathamini leo kesho watakuumbua sana, usikichome moto kichaka kilichokuifadhi wewe miaka 30 iliyopita jitaidi pia usiwe sehemu ya kundi lolote ndanin ya chama hicho, Viongozi wa wanawake nao wamefanyiwa mambo ya ajabu na hao wanaojaribu kukuendesha wewe kwa kufikiri wao ni bora kuliko makada waliyo vumilia wakati chama kinapitia wakati mgumu.
 
Back
Top Bottom