NCCR-Mageuzi-"Hatupo tayari kusikiliza kauli ya msajili wa vyama"

NCCR Mageuzi

Member
Oct 3, 2007
23
63
Sisi NCCR-Mageuzi tumepokea kwa mshangao Mkubwa sana kauli ya Msajili wa vyama vya Siasa, kuhusu kusitisha shughuli za vyama vya Siasa hadi pale anachokiita kikao cha meza ya pamoja kati ya vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na yeye Msajili wa vyama vya Siasa kuitishwa, kikao ambacho hakijulikani nilini wapi na wakati gani kitaitishwa.

Nikweli sisi NCCR-Mageuzi ni waumini wa maridhiano ya kuunganisha nchi na kuirudisha nchi pamoja lakini maridhiano yasiwe sehemu ya kuvunja Katiba kwa kisingizio cha Maridhiano kwa maana hiyo NCCR-Mageuzi hatupo tayari kusikiliza kauli ya Msajili wa vyama vya Siasa kwasababu kubwa zifuatazo.

1. Vyama vya Siasa Vipo kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 3 na sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa. Na kwakuwa ni wajibu wa kila Raia kuilinda Katiba na NCCR-Mageuzi tukiwa sehemu ya Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutailinda Katiba Kwa Kauli hii Msajili amevunja Katiba.

2. Msajili wa Vyama Vya Siasa hana mamlaka yeyote ya Kisheria ya kusitisha shughuli za Vyama vya Siasa , kazi yake ni Kusimamia Usajili wa Vyama na Kuvilinda Vyama kufanya Shughuli zake bila kubughudhiwa wala kuingiliwa nasio Kusitisha, alicho kifanya Msajili ni Kubaka Katiba au Kuipa Katiba likizo katika utendaji wake jambo ambalo sisi NCCR-Mageuzi hatutakubaliana nalo. Kuzuia Vyama visifanye Shughuli zake nisawa na kutangaza hali ya hatari Katika nchi na haya si Mamlaka ya Msajili ni Mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais ni kwa maamuzi ya Theluthi mbili ya Wabunge Bungeni kukubali hoja hiyo, hivyo Msajili asijibebeshe mzigo usio wake.

3. Sisi NCCR- Mageuzi tokea tarehe 28.08.2021 baada ya Jeshi la Polisi kuzuia Kikao chetu cha kamati Kuu ya Chama tupo katika hatua za Mwisho kuwaburuza Mahakamani ili kuomba tafsiri ya Kisheria juu ya Mamlaka ya Jeshi hilo kuzuia Mikutano ya Vyama vya Siasa vya upinzani kwa kinachoitwa Intelijensia ya Jeshi la Polisi.

4. Sisi NCCR-Mageuzi tutaendelea na Shughuli zetu za Kisiasa kama kawaida, na hivi karibuni tutakuwa na Vikao Vikubwa viwili Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama na Kikao cha Kamati Kuu ya Chama kwa maana hiyo hatuta sitisha Shughuli hizi kwa kauli ya Msajili,maandalizi ya Vikao vyote viwili yanaendelea kama yalivyo pangwa.

5. Sisi NCCR - Mageuzi hatupo tayari Kukutana na Jeshi la Polisi kwakuwa si tu kwamba Jeshi la Polisi ni Watuhumiwa namba moja katika kuvunja sheria na Kukandamiza Vyama Vya Siasa bali ni Jeshi hili linaloongoza kwa kubambikiza watu kesi hasa Wapinzani hivyo hatuko tayari kukutana na watuhumiwa.
6. Ikiwa msajili ataona kuna umuhimu wa kukutana kama ambavyo amesema basi tunamshauri busara imuelekeze tukutane na Viongozi wenye dhamana ya Usalama wa Raia na Vyama vya Siasa au Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jeshi la Polisi linafanya wanayofanya kwa mashinikizo ya Viongozi wa kisiasa.

Imetolewa leo 06.09.2021

Edward Julius Simbeye

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma
 
Mpo sahihi kabisa.Msajili wa vyama vya siasa kama angelikuwa hatumiki na CCM kisiasa angelisema "Tanzania sio dola la kipolisi" na amtake IGP awaeleze askari wake wasiingilie shughuli za vyama vya siasa kwa kuwa shughuli hizo zipo kwa mujibu wa katiba na sheria.

Wewe uliona wapi haki za kikatiba zikijadiliwa jinsi ya kutekelezwa? Ni uhuni mtupu!IGP kazi yake ni kulinda utekelezaji wa sheria za nchi na wala siyo kukaa meza moja na wahalifu na kufanya nao maridhiano.

Kama vyama vya siasa vinavunja katiba na sheria kwa kufanya vikao vya ndani pamoja na makongamano si avichukulie hatua za kisheria?Kama vyama vya siasa vinavunja katiba na sheria kwa kufanya vikao vya ndani pamoja na makongamano ya katiba inakuwaje IGP atake kukaa meza moja na wahalifu?
 
Hiyo Mutungi, huwa simwelewi kabisa. Ni kati ya majaji wanaoitia aibu Sana taasisi ya mahakama Tanzania. Ni ngumu sana kuamini kuwa na yeye ni Jaji.
 
Serikali iache matumizi ya anasa, na Ufisadi wa baadhi ya viongozi

Katiba mpya kukomesha matumizi mabaya ya serikali.

Ccm inakamua masikini wanyonge ili waendeshe maV8, na kula posho kubwa kubwa
 
Hakuna kuweka makubaliano ya kuvunja katiba
1630951501707.png
 
Hii ndiyo ile lugha sasa ambayo huyu mwamba

IMG_20210906_175550_845.jpg


huielewa.

Mfa maji haishi kutapatapa.

Hawana magereza za kutuweka wote.

Katiba mpya itafanikishwa na wenye moyo.
 
Hizi ni figisu za CCM.Haya yanayofanyika sio kwa bahati mbaya bali yapo kimkakati kuinusuru CCM.Sasa hivi CCM kisiasa ina Hali mbaya na wao CCM na serikali yake wanajua . CCM ipo ICU!
 
Back
Top Bottom