Nilifika NBC Mlimani Branch kuomba kubadilishiwa kadi baada ya kadi yangu kumezwa. Kumbe wao wana utaratibu kuwa wakitaka kubadili kadi zinamezwa kisha unazunguka ndani na kupewa nyingine. Kuingia ndani, naambiwa saa hizi saa tisa na dakika Ishirini, mwisho wa kutengeneza kadi ni saa 8. Nikawauliza ni kwa sababu process ni ndefu au kuna lingine. Nikapewa jibu kuwa hapana, process si ndefu bali tunasema mwisho saa 8 ili tuweze kupata muda wa kufanya kazi nyingine vinginevyo hatutamaliza kazi zetu. Nimwambia mhusika, nadhani mnahitaji kutangaza nafasi za kazi na si kuwaambia wateja waje wakati ambao ni convenient kwa benki. Akasema kuna maamuzi yatafanyika.
Mtazamo wangu; Hizi benki kama zilivyo biashara nyingine zimezoea kufanya kazi kwa mazoea. Unawezaje kumwambia mteja uje nikiwa nina nafasi, maana hiyo ndio maana yao.
Watanzania tujifunze kuwang'ang'ania hawa jamaa kwenye kila huduma bila kulialia au kutoa rushwa. Huyu muhusika hakuwa na kosa, bali anapelekeshwa na mfumo. Wakishindwa kubadili mfumo, tuhamie kwa wanaotusikiliza. Pale ndani kulikuwa na foleni ya ajabu saana na bado wateja wale wanaendelea kupanga foleni kila mwaka. Hizi kampuni za simu hazijawatia adabu. Wameshindwa kutafakari wanapoteza pesa kiasi gani na kutafuta namna ya kufight wanazidi kudorora. Hakuna ubunifu na sababu zinafahamika; kujuana, kubebana, kuogopana, uzembe, kutokuwa na uwezo wa kazi na mazoea.