Kigoma 2015
JF-Expert Member
- Sep 19, 2011
- 371
- 93
Kuna utaratibu ndani ya benki ya NBC kwamba Mteja anapokwenda kufungua akaunti kwa Mara ya kwanza anaambiwa ni lazima aache pesa kwaajili ya kugungulia akaunti, fedha hiyo unaambiwa uache kuanzia shilingi elfu kumi na kuendelea, kwamba akaunti ikishafunguka wanaiweka. Hata Mimi wakati nafungua akaunti mwaka 2012 niliambiwa hivyo, tatizo linakuja pale akaunti inachelewa kufunguka inachukua zaidi ya wiki moja ndo unapata simu au sms kua akaunti yako imegunguliwa. Fikiria umeenda kufungua akaunti, unaacha hela yako na bado muda wa kufunguka unachukua zaidi ya wiki.
Lakini pia Kuna baadhi ya wafanyakazi siyo waaminifu, hela wanazoacha wateja wanazitumia kwa shughuli zao binafsi, hii imetokea kwa dada wa rafiki yangu ninafanyanae kazi, anasema mwezi Wa pili anasema alikwenda Kinondoni branch kufungua akaunti halafu akasafiri kwenda mkoani baada ya akaunti kuchelewa kufunguka na akaacha shilingi 250,000, lakini kutokana na majukumu hakuweza kurudi dar es salaam mpaka hivi karibuni, amekwenda kufatilia akaunti yake anakuta ile pesa haipo, anamuuliza in charge hana majibu na siku anaacha hela alikuwepo, meneja nae anaonekana hana majibu au anawalinda watumishi wake, mpaka hivi Leo toka mwezi Wa pili hakuna jibu analopewa likaeleweka, kila siku anapigwa danadana.
Kuna mchezo mchafu unachezwa kwenye hela za watu, unaacha hela wanachelewa kufungua akaunti halafu hela yako wanazitumia siku wakijisikia wanazirudisha
Sasa sielewi kama huu ndiyo utaratibu kwa benki zote tofauti na NMB au ni NBC peke yake.
Rai yangu:
Ondoeni huo utaratibu Wa wateja kuacha pesa kabla ya akaunti kufunguka mnawafaidisha wachache wasiokua waaminifu.
Wasalaam
From Buzebazeba Kigoma