Nazungushwa kesi, Mpelelezi anapost Whatsapp picha anakula bata na dada ninayemtuhumu

Marashi

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
2,774
4,269
Wakubwa shikamoni na wadogo hamjambo?

Nilitukanwa na jirani yangu, dada tu wa miaka 23 mfanya biashara. Kosa langu ni kumdai achangie bili ya maji, akasema mimi kimbelembele na akashusha matusi lukuki ambayo JF hairuhusu kuweka hapa.

Nilipoondoka kumuepuka alibadili mbinu akaanza kuvurumisha meseji za matusi ya kunisindikizia. Niliripoti polisi, nikalipia mafuta polisi wakamfuata na defender. Kesho yake akapewa dhamana.

Mwenendo wa upelelezi wa kesi hii haueleweki...nazungushwa. Tangu juzi naona mpelelezi anapost kwenye status ya whatsapp picha mbalimbali akiwa na yule dada kwenye maeneo ya starehe.

Kesi yangu hapeleki mahakamani nimetembea sana kwenda polisi lakini sioni chochote kinachoendelea. Kesi haijafika mahakamani miezi minne sasa na ushahidi upo wazi kabisa meseji zote za matusi ninazo sijafuta.

Naomba ushauri haki yangu inapotea mimi ni mtanzania mnyonge, au nikamuone Rais wetu anisaidie. Naomba ushauri
 
Cc Mohamed Said

THE GODFATHER By Mario Puzo

Hii nimekopi kutoka KWA Mzee wangu mohamed said....

VYOMBO VYA HAKI VINAPOSHINDWA KUTOA HAKI NINI MATOKEO YAKE?

Nimepata kuandika hapa kisa cha Amerigo Bonasera na Godfather Don Veto Corleone mkasa maarufu katika kitabu cha Mario Puzo, "The Godfather."

Binti ya Amerigo Bonasera alitaka kubakwa na wahuni vijana wenzake aliodhani ni watu wema.

Binti alijitetea na wahuni wale hawakufanikiwa lakini walimpiga wakamvunja taya na kumuumiza vibaya usoni.

Amerigo Bonasera akakimbilia mahakamani kutafuta haki ya mwanae.

Hakuipata.

Vijana wale wahuni wale wabakaji wakaachiwa wakawa huru kuendelea na upuuzi wao mitaani.

Amerigo Bonasera akaenda kwa Mafia Don, Veto Corleone wa New York ya mwaka 1945 kutafuta haki yake.

Don Veto Corleone akamwambia Amerigo Bonasera, "Wewe umekwenda polisi na mahakama imekupa haki yako kwa nini hukuja kwangu toka mwanzo?"

Sasa hapa ni pa kushangaza kidogo.

Yaani Amerigo Bonasera kakosea kwenda mahakamani?

Ilitakiwa mashtaka yake ayapeleke kwa jambazi wa Mafia Don Veto Corleone?

Naam mashtaka yake sasa kayafikisha kwa Don Veto Corleone anasubiri mahakama yake itoe hukumu.

Kesi hii kwa Hakimu Don Veto Corleone ilikuwa nyepesi sana kwani ushahidi wote ulikuwa wazi.

Hapo hapo akaamuru askari wake mfano wa askari shirikishi wa huku kwetu wawatafute wale wahuni wabakaji wawaadhibu.

Amerigo Bonasera alifurahi sana akamuomba adhabu ya wale vijana wahuni wabakaji iwe kifo.

Don Veto Corleone alikataa akamwambia mwanae yu hai.

Siku ya pili hukumu ilipita.

Magazeti yale yale yaliyoandika stori ya vijana wale wahuni kuachiwa na mahakama wakaja na stori nyingine ya kuwa vijana wale wamepigwa vibaya sana jana usiku unaweza kusema wamegongwa na treni wako hospitali mahututi.

Watafiti na waandishi wa makala za uchunguzi wakagusia wakasema kuna uwezekano mkubwa kupita kiasi kuwa kuna mahakama nyingine ya hakimu muadilifu kapelekewa shauri lile na hakimu huyo lau kama si kutoka mahakama rasmi kaisikiliza upya ile kesi na katoa hukumu inayostahili.

Waandishi hawa wakaonya kuwa ni muhimu mahakimu wakatenda haki vinginevyo watawaponza watuhumiwa wanaowaachia ingawa wana makosa kufikwa na yale yaliyowafika vijana wale wahuni wabakaji.

Wazazi wa wale wahuni walipofika hospitali kuwatazama watoto wao waliona bora wangefungwa kuliko yale yaliyowafika kwa maana walikuwa hawatazamiki.

Wote walikuwa na vilema vya kudumu maisha.

Jamii zote zenye dhulma jamii hujitengenezea yenyewe njia zake za kujikinga na madhalimu.

Hizi mahakama zisizo rasmi huenda na kufanya kazi sambamba na mahakama za serikali.

Don Veto Corleone alifahamu kuwa alikuwa anashughulika na majambazi kwa hiyo kumshauri Amerigo Bonasera kurejea mahakamani kukata rufaa ni kazi bure.

Dawa ilikuwa kuwafungulia mbwa wake wakali Dobermann wakawashughulikie.
 
Wakubwa shikamoni na wadogo hamjambo?

Nilitukanwa na jirani yangu, dada tu wa miaka 23 mfanya biashara. Kosa langu ni kumdai achangie bili ya maji, akasema mimi kimbelembele na akashusha matusi lukuki ambayo JF hairuhusu kuweka hapa.

Nilipoondoka kumuepuka alibadili mbinu akaanza kuvurumisha meseji za matusi ya kunisindikizia. Niliripoti polisi, nikalipia mafuta polisi wakamfuata na defender. Kesho yake akapewa dhamana.

Mwenendo wa upelelezi wa kesi hii haueleweki...nazungushwa. Tangu juzi naona mpelelezi anapost kwenye status ya whatsapp picha mbalimbali akiwa na yule dada kwenye maeneo ya starehe.

Kesi yangu hapeleki mahakamani nimetembea sana kwenda polisi lakini sioni chochote kinachoendelea. Kesi haijafika mahakamani miezi minne sasa na ushahidi upo wazi kabisa meseji zote za matusi ninazo sijafuta.

Naomba ushauri haki yangu inapotea mimi ni mtanzania mnyonge, au nikamuone Rais wetu anisaidie. Naomba ushauri
Hapo wilaya ulipo, nenda kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali ukatoe hii taarifa.

Namna ya kuipata ofisi hiyo nenda mahakama ya wilaya ukaulize kwa karani watakuelekez.

Hii kesi inaweza kuhitimisha kibarua cha huyo mpelelezi asiyezingatia maadili
 
Yaani ukamuone Jiwe kwa mambo kama hayo?

Kweli umekosa kazi za kufanya

Shukrani sana kaka. Nitafanya hivi.
Sasa pale nikaeleze nazubgushwa polisi au nikashtaki polisi anakula starehe?
 
Back
Top Bottom