MarianaTrench
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 1,212
- 942
- Thread starter
- #21
Pole kwa unayopitia Mariana.
Ukiwa kwenye jukwaa hili kuwa mvumilivu na usiwe mwepesi ku-panic.
Nimesoma majibu yako kwa baadhi ya wachangiaji hapa na nina mambo machache tu ya kukuuliza
1. Kuna mahali umesema mmeshawahi kuonana kabla hamjawa wapenzi, nini kinawazuia kuonana kipindi hichi ambacho ni ''wapenzi'' kwa njia ya simu,e.t.c? Kama yupo nje ya nchi je yupo kimasomo au anafanya kazi?
2. Unafikiri mtaendelea na mapenzi hayo kwa namna hiyo ya kuwa mbalimbali mpaka lini?
3. Mna ahadi za kuona hivi karibuni?
4. Umewahi kuongea naye kuhusu badiliko la tabia yake? Alikujibu nini?
5. Kuna mahali umeandika kuwa ''ukiwaza kumwacha unaumia''....Yapi maumivu makali zaidi kuwa na mtu anayeku-ignore au kuamua kuvunja mahusiano ili upate muda wa kutafakari maisha yako yajayo?
Pole kwa maswali mengi.
Nashukuru kwa maswali yako yenye akili na pia utangulizi wako pale juu ni mzuri.
1. Nilienda kusoma sasa nimerudi na tupo mkoa mmoja ila kila nikimwambia kuonana anataka out za usiku na mimi siziwezi kutokana na mazingira ya nyumbani.
2. Muda umefika nadhani wa kuyaacha mapenzi ya simu.
3. Hapo sijui ulikuwa unamaanisha kuonana au kuoana?
kama kuona hapana,tulisema baada ya miaka kadhaa na haijafika bado na kama ni kuonana ndio kama hivyo mkaka anataka mambo ya night.
4. Kila nikitaka kumwambia nashindwa, naishia kuongelea swala lingine...:thinking:
5. Maumivu makali ni kua na mtu anae kuignore