Nazama, naombeni ushauri wadau

Nazama, naombeni ushauri wadau

MarianaTrench

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
1,212
Reaction score
942
Wapendwa poleni na mihangaiko ya kila siku katika kulijenga taifa. Mimi nimekuwa na uhusiano na kijana mmoja mtanashati msomi kwa muda wa miaka miwili sasa. Hatujawahi onana tunawasiliana kwenye mtandao/simu. Lakini mpendwa amebadilika mapenzi yake sio kama zamani, nikimpigia simu hapokei na akipokea ni kama hajisikii , usiku yuko busy mpaka saa sita akipokea anachomeka neti alale. Kwangu ni wa kwanza ila alishakuwa na mahusiano na watu kama wawili kabla yangu. Nikiwaza kumwacha naumia, nifanyeje? Na ansema bado annifeel,
Mimi.
Sengerema(nakuruhusu kucheka mdau)
 
Long distance relationship works best if mna commitment yenye nguvu na upendo mkuuuubwa sana!!usishangae sanana,ukiona manyoya...,ujue ashachinjwa!
 
Kwanza una uhakika ni msomi na mtanashati???!

Tuanzie hapo......
 
Hahahahahahaaaa..... ngoja nicheke kwanza! sasa kinachokufanya usimwache nn na mnaishia kwa simu, mweh usikute wachati na mzee wa miaka 60, afu anakutumia pic za mwanae, buhahahahahhahaha......
 
Naona umejiunga na jf muda mfupi uliopita kuwa makini tarehe mbaya hizi ukicheza mwaka ujao wote kwako utakua unahangaika na mapenzi.
 
umesema hamjawah kuonana???? asee una moyo kumpenda mtu usiemjua
 
Mna mpango wa kufunga ndoa kwenye simu.? Mbona kujitafutia jubilee za uchumba Jamani, 2 years unaishi na picha ya Mtu mweeeh
 
Wakuu nilikuwa nafahamina nae sio kwamba simjui, lakini wakati huo hatukuwa wapenzi wala marafiki. Kwa hiyo swala la kujua kama msomi au mtanashati ninuhakika nalo, kuhusu mwandiko nitabadilisha uwe wa kike. Na mnaoniuliza nampendaje nisie mwona nimewajibu, ila swali kwenu "mbona nyie mnampenda Mungu msie mwona?"
 
hahahaa dah haya.mwaya endendelea kuumia kwa mtu ambae haujawah kumuona
 
Pole kwa unayopitia Mariana.
Ukiwa kwenye jukwaa hili kuwa mvumilivu na usiwe mwepesi ku-panic.
Nimesoma majibu yako kwa baadhi ya wachangiaji hapa na nina mambo machache tu ya kukuuliza

1. Kuna mahali umesema mmeshawahi kuonana kabla hamjawa wapenzi, nini kinawazuia kuonana kipindi hichi ambacho ni ''wapenzi'' kwa njia ya simu,e.t.c? Kama yupo nje ya nchi je yupo kimasomo au anafanya kazi?

2. Unafikiri mtaendelea na mapenzi hayo kwa namna hiyo ya kuwa mbalimbali mpaka lini?

3. Mna ahadi za kuona hivi karibuni?

4. Umewahi kuongea naye kuhusu badiliko la tabia yake? Alikujibu nini?

5. Kuna mahali umeandika kuwa ''ukiwaza kumwacha unaumia''....Yapi maumivu makali zaidi kuwa na mtu anayeku-ignore au kuamua kuvunja mahusiano ili upate muda wa kutafakari maisha yako yajayo?

Pole kwa maswali mengi.

Wapendwa poleni na mihangaiko ya kila siku katika kulijenga taifa. Mimi nimekuwa na uhusiano na kijana mmoja mtanashati msomi kwa muda wa miaka miwili sasa. Hatujawahi onana tunawasiliana kwenye mtandao/simu. Lakini mpendwa amebadilika mapenzi yake sio kama zamani, nikimpigia simu hapokei na akipokea ni kama hajisikii , usiku yuko busy mpaka saa sita akipokea anachomeka neti alale. Kwangu ni wa kwanza ila alishakuwa na mahusiano na watu kama wawili kabla yangu. Nikiwaza kumwacha naumia, nifanyeje? Na ansema bado annifeel,
Mimi.
Sengerema(nakuruhusu kucheka mdau)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom