Nayakumbuka siku ile ya tar 29.

Nayakumbuka siku ile ya tar 29.

Mimi nakitupia lawama kubwa chama kinachotuongoza.
 
Hii siku nilikuwa na usafiri wangu wa Pikipiki nikielekea Katoro, mara baada ya kuingia mji huo nilikuta watu kadhaa wamekaa kimakundi punde si punde umbali kama wa mita mia tatu niliona gari la polisi likija kwa kasi, nilipunguza mwendo kwa haraka sana maana hao polisi walikuwa wakirusha risasi hovyo hovyo, nikapaki kwenye mkusanyiko wa watu kumbe pale palikuwepo na vijana ambao nao wanapambana kwa kuchoma moto matairi ili kuwazuia hao maaskari wasifanikishe kupiga raia.
Palikuwa na vituko vingi nilivyoshuhudia kuna Mama alikuwa anasubiri asafiri akapigwa risasi, kitu hicho kiliniogopesha sana, si hivyo tu ilinipasa niombe msaada wa kuifadhi usafiri wangu nikafanikisha kule mtaa wa kilimahewa nami nikatembea kwa njia za uchochoroni hadi nikafika nyumbani nyakati za usiku sana,kesho yake ilipofika mida ya saa nne asubuhi raia wakiwa wametulia walianza tena hao askari kupiga risasi zisizo na idadi hadi majumbani kuna kijana mdogo sana naye ilimpiga risasi nikishuhudia Mama wa huyo mtoto alichukua mwili wa kijana wake na kuanza kulia pale sebuleni, maaskari walifuata na kuuliza nanyi mnafanya nini hapa, wakatoa maelezo askari wakawaambia nyamazeni kimya la sivyo nanyi tutawafanya kama huyo.
Mauaji yalikuwa mengi mno ndani ya mji wa katoro na Buseresere walikuwa awaangalii mkubwa au mdogo, ibada zilisitishwa kwa waumini wa Islam kwa muda wa takriba siku nne.
Ndugu zangu mlio wa mijini tarehe 7/7 kama hali itarejea hivyo basi kazi tunayo, elewa hata ndani si salama.
Lakini ni nani aliyetufikisha hapa? Na kwa nini?
Sa100
 
Naichukia ccm na Samia, nilienda kumuona mtoto wa mjomba wangu pale ccm katoro alikuwa amepigwa risasi kichwa kimefumka ubongo upo nje, hakuwa na kosa alikuwa ametumwa mahitaji ya nyumbani tu!!. Yeyote anayetetea polisi na ccm hii ya Samia hajakutwa na baya la Samia na ccm!.
Kumekosekana watu mhim wakutufanya kuwa na watu tutakaoungana kulipa kisasi hiki😭😭😭.... Ila Iko siku tutalipa tena kwa Bunduki nzito naamini hili.
 
Shukuru sana Mungu ulisalimika wengine risasi ziliwafuata hukohuko ndani kwao
 
Back
Top Bottom