DissDotCom
JF-Expert Member
- Mar 31, 2014
- 395
- 268
Kwanza napenda kawapongeza BASATA kwa kuufungia wimbo wa Nay Wa Mitego "SHIKA ADABU YAKO" kwa kuwa una maudhui ya kiuchokozi, jambo la pili ni kuona haitoshi msanii huyo ametoa video ya wimbo huo na kuirusha ktk mitandao. Wito wangu kwa BASATA kama mmeweza kuufungia radioni naomba muufungie na ktk mitandao ya kijamii kwani mnaweza weka masharti ya kutoshare video hiyo kwani ina picha za kichochezi..Mfano pale anapomuimba msanii Sheta na kuonesha ishara baada ya kupewa gari na chief kiumbe akashikwa makalio (matako) je huo si uchochezi? Ushauri wa bure kwa msanii Nay wa Mitego sio kwamba kila mtu anafurahishwa na tabia yako ya kujiona mbabe ni muda wa kubadilika kaka..
Baadhi ya picha katika video hiyo ambazo ni za uzalilishaji.....
Baadhi ya picha katika video hiyo ambazo ni za uzalilishaji.....