Nawezaje kuwa mzalendo?

kidaganda

JF-Expert Member
Aug 26, 2013
2,991
2,564
Kama title inajieleza ni vipi naweza kuwa mzalendo wa nchi yangu?

Naombeni msaada
 
Sifia tu viongozi walioko madarakani, hata mfalme akikaa uchi ww mpigie tu makofi. Haikugharimu chochote kuw mzalendo
Nikiwa msingi tuliimba

Idd Amin akifa
Mimi siwezi kulia
Nitamtupa Kagera
Awe chakula ya mamba

je uzalendo wa aina hii uliisha baada ya Idd Amin kufa??
 
Kama title inajieleza ni vipi naweza kuwa mzalendo wa nchi yangu?

Naombeni msaada
Uzalendo ni jambo, kitu, imani au hitikadi.
Uzalendo huweza kufamnya mtu kuzika haki za watu ama makundi mengine, ilimradu tu anatetea, kulinda ama anaendeleza au kutukuza na kukipenda kile anacho kiamini....
 
Ukipewa kazi yoyote, hapo umeaminiwa na hiyo jumuiya iliyokupa kazi, sasa uzalendo wa kweli ni wewe kujitoa mhanga kwamba hiyo jumuia utaifanyia nini na sio jumuia ikufanyie wewe. Huo ndio uzalendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa msingi tuliimba

Idd Amin akifa
Mimi siwezi kulia
Nitamtupa Kagera
Awe chakula ya mamba

je uzalendo wa aina hii uliisha baada ya Idd Amin kufa??
Wazalendo wapo wengi sana, had wana gazeti lao linahusu uzalendo. Uzuri wa nchi yangu nikwamba wazalendo wapo chama kimoja tu, wengne wote ni wasaliti
 
uzalendo upi? kwa mujibu wa Yohana Alcohol na wenzie,Tundu nk au?
 
Ikiwa unahitaji kuwa mzalendo wa kweli, basi kuwa mtu wa haki uovu, kemea na uzuri sifia/pongeza. Lakini kama unataka kuwa mzalendo feki sifia/kubaliana na wanasiasa wachumia tumbo.
 
Back
Top Bottom