Nawezaje Kutoandikiwa Disco?

Nawezaje Kutoandikiwa Disco?

Yani ushalipa ada yote na bado wanakukazia pole sana dogo! Ungetakiwa tu kuomba ku postpone af mwezi wa 11 urudi tena kusoma kama first year! Af mbona semester ya pili ndo inaelekea kuisha ila unazungumzia mambo ya semester 1?? Pole tena mdogo angu Mungu atakusaidia yatapita!
Nili-postpone second semester, mkuu, Kama watanikubalia, Lakini pia niliandika barua, ya kuflash, kwahiyo niliandka barua mbili, Barua yoyote Itakayaojibiwa Sawa tu, wasiwasi wangu ni muda mkuu
 
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza Hapa UDSM, nasoma LLB,

Mwaka wangu hapa chuoni umekuwa mchungu kimasomo, Loan Board wamenilipia Tsh 400500 pekee kati ya 150000, ya ada kwa mwaka.

Hali iliyofanya nishindwe kufanya mtihani wa UE semester ya kwanza, Sasa nimefatilia kuomba Special Exams, Kwa wakuu wa Idara, bahati mbaya majibu yamekuwa Negatively, Kiufupi wameninyima special licha ya kueleza matatizo yaliyonikuta ya kifedha, (nimeandika barua ya special Mara mbili)

Yote, hayo, sijakata tamaa nimeamua kuandika barua ya Kurudia mwaka, Yani nianze Kama fresher Mwakani 2022/2023, Bahati mbaya majibu bado sijarudishiwa Na nipo Mkoani kila nikiwapigia simu, wananijibu majibu.

Wasiwasi wangu ni kwamba Ikiwa majibu ya kukubaliwa kurudia mwaka yasipokuwa mazuri itamaanisha nitakuwa nimeDISCO, kwakuwa sikufanya mitihani wa semester ya kwanza.

Au kuna utaratibu mwingine?

pole sana, I feel u bro[emoji1431]

MUNGU akuvushe salama
 
Sasa mkuu ukirudia mwaka hela ya ada utaitoa kwenye nini,matako
 
Sasa mkuu ukirudia mwaka hela ya ada utaitoa kwenye nini,matako
Daah kwani kama huna cha kuchangia si unyamaze kuliko kuendelea kumuongezea kijana machungu! Binadamu sikuhizi mmekuwa wa hovyo sana🤮
 
Nili-postpone second semester, mkuu, Kama watanikubalia, Lakini pia niliandika barua, ya kuflash, kwahiyo niliandka barua mbili, Barua yoyote Itakayaojibiwa Sawa tu, wasiwasi wangu ni muda mkuu
Sawa Mungu atakusaidia
 
Pole sana mkuu, tatizo mnachagua vyuo kwa mihemuko wakati uwezo hamna iyo course mbn ata mikoani wanatoa mfano mzumbe mbeya ungeishi fresh tu sifa zinawaponza.

Ushauri nenda bodi ya mikopo kawaelekeze kila kitu, wasiliana kwanza na loan officer wa chuo kwenu andika barua ya Ku post pone mwaka kupitia kw cr adi ifike kwa mkuu wa chuo huwa hawaondoki kimya na ukifanya ivo ina maana umedisko cha kufanya ni kwenda TCU wafute jina uanze mchakato upya good luck.
Sure kabisa
 
Back
Top Bottom