Nawezaje kujua kama VAT niliyokatwa imefika TRA?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,015
114,360
Nimempa kazi mkandarasi anijengee mjengo wangu kwa mkataba wa milioni 30 na ndani yake kuna kodi ya VAT ambayo ni milioni 5.4 ambayo kimsingi nimeilipa mimi!Mjengo umekamilika na malipo nimemalizia juzi.Nataka kujua kama mkandarasi kapeleka kodi yangu TRA,nifanyeje kujiridhisha kama imefika au imebanwa?
 
Akikupa receipt ya mashine(efd receipt) itaonesha hiyo kodi ya VAT hapo usiwe na hofu kodi inakuwa imesajiliwa
 
Akikupa receipt ya mashine(efd receipt) itaonesha hiyo kodi ya VAT hapo usiwe na hofu kodi inakuwa imesajiliwa
ok,nakuelewa,kuna malipo ya awali kama installment 3 hivi alitumia manual,ila 5m ya mwisho ni EFD
 
Anatakiwa akupatie risiti ya efd yenye dhamani ya fedha zote ulizokwishamlipa. Kama amekupatia efd receipt ya 5m atakuwa ameshakupiga VAT ya 25m ambayo ni pesa nyingi tuu.
 
Back
Top Bottom