Nawezaje kubadilika?

Nawezaje kubadilika?

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,997
Habari za jumapili wadau wa jukwaa hili....

Hii tabia imenishinda kuacha, iko hivi....
Iwapo akatokea mtu wangu wa karibu iwe mpenzi/mshikaji/shost ana shida fulani huwa nakuwa mwepesi sana kumsaidia hata kama itanicost kifedha, muda hata nguvu huwa najitahidi sana kumsaidia....

Hata kama niko kazini, niko radhi nitoroke nikamsaidie mtu, kwa mpenzi ndio kabisa nashindwa kujizuia. Nitadanganya hata msiba ilimradi tu nikamsaidie atakacho.

Either kazi flan au kumpeleka mahali fulani au kumfatia kitu fulani. Lakini in returns sasa wananifanyia ndivyo sivyo, huwa napatwa hasira weee nachukia ila baada ya muda nasahau na kuendelea vivyo vivyo.

Unaweza kuwa na shida ukamfata mpenzi, mshikaji / shost kumueleza lakini akadai yuko busy au hana pesa labda, ilhali unafahamu kabisa ana uwezo wa kukusaidia. Mtu huyo huyo hapo baadae anakufata umsaidie wakati yeye huwa hakusaidii ukiwa na shida.

Nifanyeje niiache hii tabia, make inanicost ila nimekuwa kichwa ngumu kuishinda!

Wasalaam

CL
 
kim nana upo kama
mimi yani mtu akilalamika shida zake huwa nakuwa mwepesi.. kwa mimi nafikiri hii kitu hutokea tu na MUNGU huwa ana makusudi yake
 
hiyo ndio asili yako sidhani kama inabadilika
 
me pia nna tatizo hlo tena kwa ndugu huniambii kitu ila wao zero kabisa ila wanasemaga tenda wema wende zako usingoje shukrani.
 
...Ni tabia njema ambazo ni inborn,cha kufanya ni kwamba usitegemee positive returns baada ya kutoa msaada,utakuwa FREE.
 
mm hata kama cna nipo radhi nikakope ili nimsaidie
 
soma alama za nyakati au ukishindwa fungua kampuni ya kusaidia umma 😛
 
"Tenda wema nenda zako" lakini pia usisahau ya kwamba "Kamwe wema haupaswi kuzidi uwezo".

Asante kwa ushauri daddito.. Ila huwa nasaidia kulingana na uwezo. Let say kama mtu anahitaji fedha ambazo ziko ndani ya uwezo wangu nitampa.

Iwapo anataka nimsaidie kazi flani ambayo naiweza nitafanya...
 
"Tenda wema nenda zako" lakini pia usisahau ya kwamba "Kamwe wema haupaswi kuzidi uwezo".

Yani kwangu ni kama vile huo msemo haupo...wakati nipo chuo nlikuwa nagawa bum looote, kiasi kwamba sijui wiki itayofuatia nakula nini....
Mtu akiumwa hostel nitauguza kama me ndo nesi wa zamu, tena kwa gharama zangu...
Sasa ngoja majanga yanifike....simuoni shosti wala ndugu.....! Yani mpaka nabaki nalia tu....!
 
Kama roho yako ni nzuri basi endelea kutenda wema usifanye kotu kizuri kwa kutegemea nawewe kufanyiwa.

Unafanya sababu moyo wako unakutuma n as long as unapata faraja ukimsaidia mtu basi endelea tu.
 
Hii si tabia mbaya hata kidogo. Tunatakiwa kutolipa kisasi. Tunafundishwa kisasi si juu yetu bali Mwenyezi Mungu yeye ndiye mwenye kutulipa na kutulipia!

Kwa hivyo endelea kutenda wema kwani ukifanya hivyo unahisi kupungukiwa chochote? Zaidi unabarikiwa na kikombe chako kinajazwa na kusukwa-sukwa!

Barikiwa
 
mmh kweli hiyo ni inborn character
maana mimi sijui ndo roho mbaya au nini, yaani nikusaidie halafu siku niwe na shida usionyeshe ushirikiano hata wa ushauri tuu
ni bora usahau kabisa msaada wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom