Jinsi ya kuandaa mpango wa biashara (Business Plan)

The Consult

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
220
252
shutterstock_162866975.jpg

Mpango wa Biashara (Business Plan), ni nyenzo muhimu katika mafanikio ya biashara. Mpango wa Biashara humsaidia mjasiriamali ku-shape wazo lake la biashara na kulifanya kuwa fursa (Opportunity).

FAIDA ZA KUWA NA MPANGO WA BIASHARA
  • Hutoa taarifa za msingi juu ya biashara; zinazomuwezesha mjasiriamali kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara.
  • Huweza kutumika kwa ajili ya kuvuta rasilimali watu.
  • Humsaidia mjasiriamali katika kutafuta na kupata mshirika/washirika katika biashara (Strategic Partiner/Suppliers)
Mpango wa Biashara hupaswa kujikita katika maeneo ya msingi (critical aspects) za mfumo wako wa biashara (business model) na kutoka hapa ndipo tunapata mtindo au "format" ya Mpango wa Biashara.
Busara (wisdom) ni kuamini kwamba Mpango wa Biashara ni nyaraka iishiyo "living document" maana ya dhana hii ni kwamba; kadiri siku zitakapokuwa zinakwenda, Mpango utakuwa unahuishwa kutokana na mabadiliko ya kimazingira katika biashara.

MTIRIRIKO/MUUNDO WA MPANGO WA BIASHARA/BUSINESS PLAN FORMAT

(A) THE COVER
Sehemu hii; inapaswa kujumuisha JINA LA KAMPUNI, MTU WA KUWASILIANA NAE (CONTACT PERSON), ANUANI, n.k

(B) EXECUTIVE SUMMARY
Hii ni sehemu muhimu sana katika Mpango wa Biashara, ikiwa hutoweza kuvuta "attention" ya msomaji katika sehemu hii, basi hata sehemu za mbele hutoweza pia. Ni kama ilivyo katika kitabu; siku zote msomaji huvutika na kitabu baada ya kusoma machache ndani ya jalada la kitabu (cover). Kimsing; sehemu hii, inapaswa kujumuisha vitu vifuatavyo;
  • Ufafanuzi juu ya fursa (Description of Opportunity)
  • Dhana ya biashara (Business Concept)
  • Hali ya biashara (Industry Overview)
  • Soko lengwa (Target Market)
  • Faida ya kiushindani (Competitive Advantage)
  • Mtindo wa biashara (Business Model)
  • Timu (Team)
  • Muhtasari wa masuala ya fedha (Financial Snapshot)
Kumbuka kwamba, vipengele hivii vinapaswa kuelezewa kiundani zaidi katika sehemu za mbele.

(C) TABLE OF CONTENTS
Hii ni sehemu muhimu pia katika Mpango wa Biashara, na ni ramani "road-map"; kwa maana ya kwamba inaonyesha "major sections/sub-sections" za Mpango wa Biashara

(D) INDUSTRY, CUSTOMER AND COMPETITOR

Industry: Lengo la sehemu hii, ni kuelezea fursa na namna utakavyo ikumbatia (capturing). Pia unapaswa kuelezea aina na ukubwa wa soko kwa wakati husika na namna unavyotaraji ukuaji wa soko hilo. Historia inatuonyesha kwamba; fursa (best opportunities) hupatikana zaidi katika masoko yanayochipukia (emerging markets). Kwa mfano; miaka ya 1980 soko la kompyuta (Personal Computers) lilianza kuchipuka, hivyo likapelekea uwepo wa makampuni kama Apple, Microsoft, Intel n.k. Pia katika miaka ya 1990 soko la mtandao (Internet) lilianza kuchipuka, hivyo likapelekea uwepo wa makapuni kama Google, Facebook, eBay n.k

Customer: Baada ya kuwa umeainisha sehemu yako ya soko (market space) unayotaraji kuiingia, ni wakati sasa wa kufanya uchambuzi wa kina juu wateja wako (examining your customers' details). Uchambuzi wa wateja unapaswa kuzingatia kipengele cha saikolojia na makundi ya watu (psychological and demographic factors). Fahamu kwamba kadiri unavyozidi kuwachambua wateja wako, ndivyo uwezekano wa kuwapelekea bidhaa wazitakazo unakuwa mkubwa,.epuka kuwa na dhana ile isemayo KILA MTU MWENYE NJAA BASI ATAKUWA MTEJA KATIKA MGAHAWA WAKO.

Competition: Tayari umeshatambua soko lako (market segment) , umekusanya taarifa za kina za wateja wako (customers' profile) pia umejua ni nini hasa wateja wako wanahitaji. Kinachofuata nikuangalia kwa namna gani mshindani wako, anatimiza mahitaji ya wateja husika. Hapa utakuja kujua udhaifu wake (weaknesses) na umadhubuti wake (strengths)

COMPANY AND PRODUCT DESCRIPTION
Katika sehemu hii, utapaswa kutoa maelezo juu ya kampuni yako ikijumuisha jina la kampuni, mahala ambapo kampuni imesajiliwa, lakini pia na sheria iliyotumika kusajili kampuni hiyo, pia utapaswa kuelezea dira na malengo ya kampuni yako.. Mbali na uelezaji wa taarifa za kampuni; sehemu hii pia hutoa maelezo juu ya bidhaa/huduma zako, katika bidhaa/huduma, utapaswa kuelezea sifa za bidhaa/huduma yako (features) pia utofauti uliopo kati ya bidhaa/huduma yako dhidi ya za wengine.

MARKETING PLAN
Katika sehemu hii, unapaswa kuonyesha ni kwa namna gani utaingia katika soko, lakini pia mbinu gani utazitumia katika kukuza biashara yako na hatimaye kufikia malengo uliyojiwekea. Sehemu hii; kimsingi inapswa kujumuisha mbinu zifuatazo;
  • Mbinu juu ya soko lengwa (Target Market Strategy)
  • Mbinu juu ya bidhaa/huduma (Product/Service Strategy)
  • Mbinu juu ya bei (Pricing Strategy)
  • Mbinu katika usambazaji wa bidhaa/huduma (Distribution Strategy)
  • Mbinu za mawasiliano kimasoko (Marketing Communications Strategy)
  • Mbinu katika mauzo (Sales Strategy)
OPERATIONS PLAN
Sehemu hii inapaswa kuonyesha namna shughuli za biashara zitakavyoongeza thamani kwa wateja wako. Mbali na hivyo; sehemu hii pia inapaswa kuonyesha muda ambao kampuni itatumia katika uzalishaji wa bidhaa/huduma.

DEVELOPMENT PLAN
Katika sehemu hii, utapaswa kuonyesha mbinu katika uendelezaji na ukuaji wa biasharai yako. Katika sehemu hii utapaswa kuja na "Development Strategy" ambayo itazingatia "risks" ambazo biashara inakutana nazo, vitu vinavyopaswa kuwepo ili kutokee maendeleo ya biashara n.k

TEAM
Hapa unapaswa kuonyesha timu ya rasilimali watu ambayo inahitajika katika kuhakikisha malengo ya biashara yako yanatimia. Ni vyema ukachagua watu wenye sifa stahiki na wenye ubunifu. Katika kampuni nyingi, muanzilishi mara nyingi hujipa cheo cha CEO., ikiwa wewe kama muanzilishi huna uzoefu wa kutosha au labda unamajukumu mengine, basi ni vyema ukamtafuta mtu mwenye uzoefu akakalia nafasi ya u-CEO.

CRITICAL RISKS
Biashara yoyote hukabiliwa na vikwazo au hatari, ili biashara yako iweze kusonga mbele, ni vyema hatari katika ukuaji wa biashara yako (risks) zika-ainishwa na kisha ukatengenezwa mpango wa kukabiliana nazo "Risk Mitigation Measures".

FINANCIAL PLAN
Hapa ndipo kulipo na uti wa mgongo au sehemu ya msingi zaidi katika Mpango wa Biashara, hususani Mpango huo unapotarajiwa kutumika kwa ajili ya kutafuta mtaji. Sehemu hii huonyesha makisio ya mapato na matumizi ya biashara yako, na ndio sehemu ambayo huangaliwa sana na wafadhili hasa mabenki.

Ahsante

The Consult
Mob: +255 719 518 367
E-mail; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam, Tanzania
Home of Project Management, Strategic Management & Fundraising
 
Asante Nimepata Picha .... Now I have an Image About how to write Business Plan,Thank your.... BeBlessed

BettingClick here---> 1xbet.com
 
.
asante sana kwabkazi nzuri sana uliyofanya,mie nataka kufanya hii kitu nitakutafuta kwa ajili ya elimu
 
Business plan zipo za aina tofauti tofauti lakini vitu ulivyovitaja ni vya muhimu sana ...
Naona sehemu ya milestone and traction (sehemu ulipofikia kama hiyo business plan inahusisha mradi ambao upo katika maandalizi au umeshaanza kufanya kazi)..
Hapa utaweka aina ya matumizi uliyofanya pamoja na vitu vingine ambavyo umeshavifanya ili kuhakikisha mradi unaonesha uelekeo ... Hii ni sehemu nzuri kama utahitaji financers, kwa siku za usoni ni ngumu kumshawishi mtu akupe pesa ilhali wazo lako zima lipo kwenye karatasi tu....

Salute lakini mkuu
 
Asante mkuu kwa moyo wako wa kushare, hebu tafadhali tushushie hapa sample business plan aka mfano halisi kwa ajili ya ufahamu zaidi.
 
Ingia website ya Bplans... niliijua kupitia jf na nilijifunzia kuandika vitu kama business propasal na business plan.ipo katika lugha ya kiingereza lakini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom