Nawaza hivi kuboresha barabara zetu

Nawaza hivi kuboresha barabara zetu

MLALE

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
220
Reaction score
423
Ni kwa nini tuliowaajiri kutuongoza wasifanye yafuatayo kuboresha barabara zetu?
1.(a)Kutumia wafungwa waliofungwa vifungo vya muda mfupi kutujengea barabara zetu korofi? (As cheap labour)

1(b)Kutumia malighafi tulizonazo kama mchanga, kokoto, saruji na wakandarasi wetu wazawa kutujengea barabara za lami?

2.Kwenye kilimo....kama Misri wanafanya vema kwenye kilimo cha matunda na mboga mboga, ingawa wapo jangwani, sisi tufanye yafuatayo........(ngoja niendelee kuwaza kwanza).
 
Hayo yote yanawezekana, shida wakifanya hivo watapata wapi njia ya kuchota mapesa kwa manufaa yao wenyewe.

Viongozi, viongozi, viongozi.

Mungu aingilie kati tuu.
 
Tuendeleeni kuwaza na kutafakari Watanganyika wenzangu.
 
Yaani ulifikiri zaidi mfungwa huyo kafanya makosa badala nasi tuwatumie watuzalishia vitu eti tena tunaingia gharama kuwatunza kweli
Waangalie namna nzuri ya kufaidika na makosa yao ata kwa kuwachukua wale wenye makosa madogo madogo ili wasaidie kazi za kujenga nchi yetu aisee
 
Katika kufanikisha jambo usiwaze kutesa WATU .

Wafungwa wanabidi kujikita katika masomo na kufanya
kazi ndogo ndogo ambazo kama kilimo cha mboga mboga ,kupalilia bustani .nk sio za kumkomoa mfungwa

Kuwafanyisha kazi ngumu wafungwa haifai.

Gerezani ni sehemu ya kujifunza na sio kutesa.
 
umesema vema kiongozi,toa sasa mawazo yako ya ni kitu gani kifanyike ili tuwe na barabara zilizo bora?
 
Back
Top Bottom