Nawatakieni Kwaresma Njema

Nawatakieni Kwaresma Njema

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Tumeanza safari yetu ndefu na muhimu sana ya mfungo wa siku arobaini (mfungo wa Kwaresma), tunayoianza siku ya Jumatano ya majivu (leo).

Katika kipindi hiki cha siku 40, mama Kanisa anatualika sisi sote kushughulikia kwa jitihada kubwa zaidi uongofu wetu sisi wenyewe.

Masomo matakatifu pamoja na tafakari nyingi, zitatuelekeza kujitafiti katika roho ya ukweli wa ndani, tujifahamu tulivyo ili tujirekebishe pale ambapo hatukwenda sana na tujiimarishe zaidi pale ambapo kwa neema ya Mungu tuliweza kwenda sawa. Daima sote tunaalikwa kuongeza na kuimarisha maisha ya fadhila mbalimbali.

Kwaresma ni kipindi cha kujipatanisha kwanza na nafsi zetu. Kuna nyakati tumejitendea mambo makubwa maovu sana, hata tukaanza kujichukia sisi wenyewe, tumejikatia matumaini, tunajiona hatufai tena na tunahisi kuwa hatupendwi na wenzetu.

Hatua ya kwanza ya wongofu ni kujifahamu, pili ni kujikubali na tatu ni kuwa tayari kujisamehe na kujirekebisha. Acha ya kale, anza upya, songa mbele.

Kwaresma ni kipindi cha kumrudia Mungu kwa mioyo yetu yote. Kwa kinywa cha Nabii Yoeli mwenyewe asema "...nirudieni mimi kwa moyo wote, kwa kufunga, kulia na kuomboleza" Yoel 2:12.

Katika roho ya ukweli wa ndani, kila mmoja katika familia anajua ni namna gani amejiweka mbali na Mungu, na kwa kitendo cha kuwa mbali na Mungu, wewe katika familia umekuwa ndio uchochoro wa shetani, anayeingia katika familia ili kuivuruga. Bwana akuita kwa upole, asema nirudieni mimi kwa moyo wote.

Kwaresma ni kipindi cha kutoa sadaka sana, kusali sana kwa moyo wa toba ya ndani na kufunga (Rej. Mt. 6:1-6, 16-18). Hii ni sehemu ya habari njema inayosomwa siku ya Jumatano ya Majivu. Katika sehemu hii Bwana anatupatia nidhamu ya kutoa sadaka, kusali na kufunga ili kweli tupate mafaa ya kiroho. Na sisi kama familia tunapenda kwaresma hii tuwe na sadaka ya pamoja kama familia, tuwe na sala za pamoja zaidi na tuuchukue mfungo huu kwa pamoja.

Wataalamu wa mambo ya roho wanatuambia, kufunga ni namna bora zaidi ya kufanya kitubio na kujipatia nguvu mpya ya roho.

Kwa ujumla wake katika kipindi hiki cha Kwaresma, sisi wana kanisa la nyumbani yaani familia, tutatafakari sana juu ya tunu za toba na msamaha.

Tutakiri kwamba, katika familia zetu mara nyingi tumekoseana na kujeruhiana vibaya sana, kiasi kwamba tumeathiri vikali ule UZURI wa maisha ya ndoa na familia. Kwa matendo yetu tumeifukuza haki, tumefukuza upendo, tumefukuza amani na furaha ya familia. Dawa yetu ni mmoja tu – toba na msamaha, tufanye toba ya kweli, tusameheane na tuwe tayari kujirekebisha kabisa.

Familia nyingi zimekonda na kunyauka vibaya, hazijui tena kicheko wala tabasamu, wala utani kwa sababu wanashindwa kuombana msamaha wa kweli na kusameheana. Wengi wanapenda zaidi maisha ya ubabe na umame ambayo hayajengi familia kamwe.

Ugangwe, jeuri, kiburi na roho mbaya vinaelekea kutawala katika familia zetu!! Vilio vimezidi katika Kanisa la nyumbani. Nani anyamazishe? Ni MIMI NA WEWE.

Baba Mtakatifu Fransisko anatufundisha, maneno matatu yanayoifanya familia isonge mbele ni NAOMBA, SAMAHANI na ASANTE. Katika Kwaresma hii tutalitafakari sana hilo lihusulo KUOMBA MSAMAHA, KUTUBU KWA MANENO NA VITENDO, na KUFANYA JITIHADA YA KUJIREKEBISHA. Usijitese kwa kutokuwa tayari kutubu, na usijiangamize kwa kutokuwa tayari kusamehe.

Mume jipatanishe na mkeo, mke jipatanishe na mumeo, wazazi jipatanisheni na watoto wenu, watoto, jipatanisheni na wazazi wenu. Msamaha na mapatano mema VINAWEZEKANA. Bwana Mungu atuumbie mioyo safi na atengeneze tena roho thabiti iliyotulia ndani mwetu.

Tunawaweka mikononi mwa Mungu na tunawatakieni nyote Kwaresma njema.

Mwenyezi Mungu Awabariki Nyote...
 
Funga siku ya jumatano ya majivu, usile nyama siku ya ijumaa kuu.
 
Nashukuru kwa kutukumbusha. Mwenyezi Mungu atuongoze kwenye safari hii ya kiroho.
 
kbm tafadhali weka bandiko lako kwenye paragraph
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanaJF leo ni siku ya Jumatano ya majivu tunaanza siku 40 za kifunga kwa kijitahidi kufanya ibada ya Toba
 
Asanteeee Mpwa kwa Mahubiri haya mazuri, I wish na serikali ingeingia Kwaresma kidogo ili watimize ahadi zao
 
Asante kwa somo nzuri na haswa ulivyogusia familia na kwa kua huu ni mwaka wa familia na tunatakiwa kuitanguliza famili kwanza kwani shetani amezismbaratisha familia nyingi kwa kuweka chuki,usaliti na moyo wa kuto kusamehe na kwa namna hio familia nyingi zimesambaratika na zimekosa upendo,hivyo basi ni kwakati huu kanisa lina tualika kumrudia Mungu kama ulivyosema,sala yangu ni mwenyezi MUNGU atuzidishie nguvu ili kuweza kuitimiza nia yetu ndani ya moyo haswa kipindi hiki.kwaresma njema nawe ndugu.
 
Amina sana, mwezi huu tujizuie kidogo hata kuangalia picha chafu na zisizo na maadili, maneno mabaya kwa wenzetu, kunywa pombe na mengineyo yasiyompendeza Mungu.

Huu ni mwezi mhimu sana kwa Wakiristo.

Tusali, tutubu na tuiamini injili!
 
Back
Top Bottom