Nawasilisha maombi kwa kila mwenye huruma kuiombea Kyela

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,554
223,065
Nikiwa kama Mtanzania na Mzaliwa wa Kyela mkoani Mbeya nawasilisha maombi kwa kila mwenye huruma kuiombea kyela .

Barabara inayozunguka soko kuu ambayo kwa ujumla wake haifiki hata kilometa 5 iko kwenye ujenzi kwa zaidi ya mwaka ! Haya ni maajabu ! Wananchi na wafanyabiashara wanaendelea kula vumbi kwa kipindi chote hicho , hata namna ya utengenezaji wake unatia shaka kubwa sana , ama ni wa kisasa zaidi au ni wa kizamani sana , wanamwaga kwanza rami halafu ndio kokoto zinawekwa juu yake , sijawahi kuona !

Kipande kidogo namna hii kinajengwaje kwa kipindi kirefu namna hii ? Ikumbukwe kwamba vifusi vilimwagwa miezi kadhaa kabla ya uchaguzi baada ya kishindo kikubwa cha UKAWA Kupitia mgombea wake wa ubunge Abraham Mwanyamaki , Sasa hivi wameziba njia kutoka mafura soap hadi mjini , hatufahamu ukarabati wa kipande hicho utakamilika lini kama hili tu limechukua zaidi ya mwaka na bado hatujui litaisha lini .

Nimetembelea eneo la ukarabati , nilichokiona ni aibu ! Mafundi wanatumia sululu kuchimbua barabara ili waweke viraka ! Ukiangalia barabara ya kyela kutoka mjini hadi Nkuyu , njia panda ya ipinda , imejaa viraka mithili ya ubao wa kuchezea draft ! Wako wapi viongozi wenye uchungu na kyela ? Ni lini magari ya abiria yataacha kupita kwenye vinjia hatarishi vilivyojaa vumbi na mawe makubwa ambayo ni hatari kwa usalama wa magari na abiria ?

Mungu ibariki Kyela .

........... Itaendelea .......
 
Mfalme anaihujumu Kyela kwa maslahi yake yake yaasiyojulikana na wengi....watu wanakunywa maji ya vyura wakati zaman tulikuwa tunanywesha ngo"ombe maji ya nomba(Danida).
 
Mfalme **** anaihujumu Kyela kwa maslahi yake yake yaasiyojulikana na wengi....watu wanakunywa maji ya vyura wakati zaman tulikuwa tunanywesha ngo"ombe maji ya nomba(Danida).
Umeandika jambo ambalo limenichoma sana !
 
Things Fall Apart,No Longer at Ease.
"Utundhu Tunyambanike,Lhukajapo Ulutengano Khangi"...
Mabomu yaliyopigwa kulazimisha ushindi yamesababisha kyela iwe kama pemba , hali ni mbaya mno !
 
Ungapasyaga nnkamu...mfalme ju.ha anachofanya Mungu atamlipa...sawa sawa na hila zake.
Tumerudi nyuma Sana, wilaya ilikua ipo vizuri Sana miaka kadhaa iliopita. Kwasasa mambo ovyo ovyo, mji umepoa saana.
Hongera kwa thread nzuri mkuu.
 
Tumerudi nyuma Sana, wilaya ilikua ipo vizuri Sana miaka kadhaa iliopita. Kwasasa mambo ovyo ovyo, mji umepoa saana.
Hongera kwa thread nzuri mkuu.
Thread siyo yangu mkuu...ni ya Erythrocit mkuu..nafikiri kakerwa sana na hali aliyoikuta...
Anyway_heko wa kaka yetu Mwamnyange kwa Ngonga beach...at least kafanya jambo la maana na kubwa kwa Kyela yetu.
 
Mmefanya nipatamani kyela nikale usipa na mbasa, ila daah mbunge wetu anatuangusha yaan hata kale ka barabara ka kwenda tenende hajakamalizia. Na hawakumtaka hata kidgo nakumbuka mwaka juz nimeenda yaan wazee walikua wanamlaani mbaya
 
Mmefanya nipatamani kyela nikale usipa na mbasa, ila daah mbunge wetu anatuangusha yaan hata kale ka barabara ka kwenda tenende hajakamalizia. Na hawakumtaka hata kidgo nakumbuka mwaka juz nimeenda yaan wazee walikua wanamlaani mbaya
Mkuu , Mungu ni mwema sana , tuendelee kumuomba .
 
Back
Top Bottom