Nawasihi wa Tz rejeeni katika mila zenu katika kutatua migogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawasihi wa Tz rejeeni katika mila zenu katika kutatua migogoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Barubaru, Feb 9, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi nashauri ni lazima waTz murejee katika mila na desturi zenu na kuachana na hizo za kizungu.

  Nakumbuka toka zamani kulikuwa na kuto kuelewana kunakoweza kutokea katika jamii mbali mbali mfano wakti nipo Chuo kikuu UDSM tulikuwa tuna mogogoro mara kwa mara na chuo au na Serikali.
  Lakin mila zenu ilikuwa wanafunzi woote mnakusanyika pale Nkuruma hall na viongozi wanakuja na kukaa kitako kuanza kujadili matatizo yenu mpaka mnafikia kukubaliana na baadae mnarudi darasani.

  Siku zote viongozi walikuwa wepesi kufika na kuongea na wanafunzi na kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano mezani na sio kuandamana.

  Naona sasa utamaduni huo huko Tz umepotea kabisa. Viongozi wanajiona ni miungu watu hawataki kabisa kuwasikiliza wanaowaongoza na kupenda kutumia ubabe katika kutatua migogoro.

  Hakika ubabe na ubinafsi ni sumu sana katika uongozi. Kiongozi kumbuka bila kuwa na unaowaongoza wewe huwezi kuwa kiongozi. Na mnaongozwa acheni lugha za kebehi na kashfa kwa viongozi wenu. Hishma ni muhimu sana na utii wa sharia zenu mlizojitungia.

  Nawasihi tena waTz rudini kwenye mila na desturi zenu za kukaa kitako na kujadili matatizo yenu mezani na sio kwa kuandamana na kutusiana.

  Loh naifananisha Barza ya JF sawa na Mzee Punch wa Udsm enzi hizo.
   
Loading...