Nawashukuru wana jf wote kwa msaada wenu!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Siku ya ijumaa tarehe 3 niliwaomba ndugu wanajf kujua hospital nzuri hapa dar, nikaeleza kuwa mwanangu anaumwa anaharisha na kutapika. Pia nilisema kuwa nilimpeleka kwa Dr koya pale Lumumba jirani na chama cha Magamba akapewa dawa bila mafanikio!

Wengi mlitoa maoni yenu nikaahidi kufanyia kazi! Hakika palipo na wengi haliharibiki jambo.

Kwanza nilimurudisha kwa dr koya akambadilishia dawa na nikafuata ushauri wenu wa kupa juice ya machungwa na mapapai na kuhakikisha mke wangu anamnyonyesha vya kutosha bila kusahau kumpa maji!

Mungu si athumani, faizafox, rit, tumaini, magamba wala yericko; dogo kapona na anadunda kijoti!

Idumu JF
 
Katika hali ya uhitaji wa mambo na upatikanaji wake JF yaweza kufananishwa na google, wikipedia au Britannic
 
Kweli asiyeshukuru kafiri. Bora wewe umekumbuka kushukuru maana wengine muh..,......
 
Hapo ndio utaona Baba wa Taifa alifanya kazi kutengeneza hii kitu ya wa Tanzania kujitolea kusaidia mtu yeyote na wakati wowote bila kujali Kabila, rangi, dini..wala jina kama langu la Zumbukuku..
 
Hapo ndio utaona Baba wa Taifa alifanya kazi kutengeneza hii kitu ya wa Tanzania kujitolea kusaidia mtu yeyote na wakati wowote bila kujali Kabila, rangi, dini..wala jina kama langu la Zumbukuku..

Kweli kabisa Nyerere aliweka uzalendo imara!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom