Faru Jenny
Senior Member
- Dec 29, 2016
- 101
- 71
Habarini za jumapili ndugu zangu? Natumaini mko salama na mnaendelea vizuri na maisha ya kila siku. Tafadhali naomba nichukue muda wenu kidogo kuwaeleza shida niliyonayo kama mtanzania mwenzenu mtakaowiwa muone namna ya kunisaidia.
Mimi ni mtanzania mwenzenu mzaliwa wa pili kwenye familia ya watoto sita. Kwenye familia yetu kwa sasa tuna mzazi mmoja baada ya baba kufariki mwaka 2009. Na la mwisho kwenye utambulisho mm ni mtoto pekee wa kiume katika familia yetu.
Sasa naomba niingie kwenye kilichonifanya kuna hapa kwenu wana JF kuwalilia. Mwaka 2008, dada yangu alichaguliwa kujiunga kidato cha tano katika moja ya shule za sekondari za serikali zilizopo kaskazini mwa nchi yetu. Baada ya kusoma kwa miezi kama mitatu akawa ameanza shida ya kuchanganyikiwa..( psychiatric) kama inavyotajwa kitaalam mm sina uelewa sana. Shule ilichukua jukumu kumfikisha katika hospitali ya mawenzi mkoani Kilimanjaro na baadae familia ilichukua jukumu la kumsafirisha Dar kwa kuwa kipindi hicho baba alikuwa hai na alikuwa anafanya vishughuli vyake huko Dar es salaam. Dada alitibiwa katika kitengo cha magonjwa ya akili cha hospitali ya taifa ya muhimbili kwa kipindi chote cha ule mwaka 2OO8. Alirudi shuleni kuanza kidato cha tano upya mwaka 2OO9, mwaka ambao pia mzee alifariki.
Tokea hapo tatizo limekuwa likimrudia mara na akawa anaahirisha masomo kila wakati hadi akafanikiwa kuhitimu chuo kikuu mwaka 2O15. Katika kipindi chote hicho tulikuwa tunajitahidi kama ndugu kujichangiana kumtibu. Kwa miaka kumi hiyo hadi sasa tulitumia resources nyingi kumtibu kwa kweli ukizingatia hata kwa waganga tulienda kutokana na ushawishi na shuhuda za watu . Aisee ukiwa na shida kubwa unaweza kulishwa hata mavi na binadamu.
Kinachotuumiza zaidi ni kuwa tangu alipo hitimu chuo kikuu mwaka 2O15 ameugua mfululizo hadi sasa. Tangu shida hiyo ilivyomuanza hajawahi kuugua kwa kipindi kirefu mfululizo kama hiki. Tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu katika kila jambo lakini haki yake ndio ikazidi kuwa mbaya yani anakuwa kichaa zaidi kila kukicha. Kwa kweli imefika mahali hadi ndugu wa karibu wakajitoa kwa kuchoka kuhangaika. Nikabaki mm Na mama kama Mtoto wa kiume nikawa napambana hivyohivyo. Mm nipo mbali na nyumbani nakofanyia shughuli zangu so nikiwa napata madeni makubwa kwa akili ya kumfuatilia na kumuuguza.
Sikukata tamaa. Ilivyofika mahali usalama wake ukawa hatarini kutokana na kutoroka nyumbani usiku mara kwa mara na kwenda kusiko julikana. Baada ya kufikia hatua hiyo nikafahamishwa kuwa kuna hospitali inaitwa Lutindi ipo korogwe Tanga, pale usalama wake unaweza kuwa wa uhakika maana ni kwa ajili ya watu kama hao. Wanakaa hostel za hospital wanakula wanatibiwa kwa dawa na ushauri wa kisaikolojia.
Jamani nilijitahidi nikamchukua nikaenda nae huko na ndiko aliko sasa TATIZO NIMEZIDIWA MALIPO NDUGU ZANGU. KULE NATAKIWA KUTOA ELFU 6O, kila wiki kitu ambacho kwa kubangaiza kwangu note sijaona nikifaulu. Mambo yananiendea mrama sana nimejitahidi kulipa wiki 2. Kwa sasa nimezidiwa na hakuna tena msaada mwingine nilionao.
Ninawaomba mnisaidie chochote. Anatakiwa kukaa hospital kwa miezi mitatu . Sitaweza tena mwenyewe nipigeni tafu mlionacho kidogo nitawashukuru sana. Hata ukitaka kutuma chochote cha msaada hospitali moja kwa moja nita shukuru karibu DM nitatoa mawasiliano ndugu zangu.
Asante kwako wewe uliyechukua muda kusoma ingawa naweza kuwa sijaweza sana kujielezea naamini mtajitahidi kunielewa. Wasaalam.