Nawashangaa wanaohama CHADEMA kwa sababu za Zitto

cr9

Senior Member
Oct 13, 2010
185
102
Mimi si mwanachama wa CHADEMA lakini ninawashangaa wanaohama chama chao kwa sababu ya Zitto Kabwe wakati Zitto mwenyewe bado mwanachama wa CHADEMA na kasema haondoki.

Sidhani kama hoja ya kuilaumu CC ya CHADEMA juu ya uamuzi kwa ZZK ni sababu ya wao kuhama na kumuacha mtu wanayemtetea akibaki kuwa mwanachama wa CHADEMA tena aliyeapa kutohama chama chake.
 
Wahuni wahuni wa mtaani hao, - nani mtu makini aliyemfuata Zitto so far?

CDM ni msingi na si Mtu. Acha madogo wa mtaani wapate chochote, kufa kufaana!!
 
Hao ni wanachama wa CCM ambao eti wanahama Chadema kwa vile Zitto kafukuzwa. Zitto lini kafukuzwa? Huo ni uhuni tuu.
 
Wahuni wahuni wa mtaani hao, - nani mtu makini aliyemfuata Zitto so far?

CDM ni msingi na si Mtu. Acha madogo wa mtaani wapate chochote, kufa kufaana!!

nakuomba ujipe muda uende mlango wa pili (jukwaa la siasa) kisha usome alichopigania chacha wangwe (r.i.p) - dadavua bila ushabiki kama kinapishana na madai ya wanaoitwa wasaliti leo hii ndani ya chama!!! amini usiamini mbowe ni tatizo ndani ya chama!
 
''Sihami CDM, nitakuwa wa mwisho kuondoka labda waje waniondoe wao wenyewe'' Mhe. Zitto. Mnaohama chadema kwa sababu zitto kaondoka sasa hii ndio iliyokuwa kauli yake kuhusiana na kadhia iliyopo. Mhe. uende wapi wakati chama umekijenga mwenyewe?
 
Back
Top Bottom