Nawaonea wivu wakenya

Nawaonea wivu wakenya

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,549
Sio kila wivu ni mbaya kuna nyivu zinazoleta faida na kuna nyivu zinazoketa magonjwa ya moyo na kadhalika.

Hatimaye wakenya wamefanikiwa kuwa na usafiri wa ndege moja kwa moja kutoka Nairobi(Kenya) mpaka New York(Marekani) Hongera sana kwa Uhuru Kenyata na wakenya kwa ujumla.

Haya mafanikio hayajanipa wivu...kilichonifanya niwaonee wivu wakenya. Ni hulka yao ya kupongeza maendeleo kwa mstakabali wa nchi yao.

Sijasikia wala kuona wapinzani (Kina Odinga na wenzake) wakipinga au kukosoa maendeleo haya.

Wakenya wote, matajiri kwa maskini wamefurahia na kuimba nyimbo za uzalendo. Kwa kweli nimeona wivu.

Ingekuwa hapa kwetu, kuna watu wapinga kila kitu wangetukana na kukejeli. Cha ajabu watanzania wengi wamempongeza Uhuru Kenyata wakati huo huo wakiponda shirika la ndege la Tanzania.

Wameshindwa kukumbuka kuwa kabla ya Magufuli kuwa rais, serikali haikuwa na ndege za abiria za kuaminika na shirika lilikufa.

Sasa shirika limenunua ndege kutoka Canada na Marekani watu wanakejeli eti hazitadumu mara mapanga...

Kwa kweli aliyeturoga kafa...




MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA.

MUNGU MUBARIKI MTUMISHI WAKO MAGUFULI MKOMBOZI WA TAIFA KUBWA LA TANZANIA.


IMG_20181029_232358.jpeg
View attachment 4f1b6f96d6318ad64878839e8162ce51.mp4
IMG_20181029_232403.jpeg
 
..kitanda usichokilala hujui kunguni wakeee....nyasi upande wa jirani huwa zaonekana kijani muda woteee.....time will tell
 
Nafikiri uone wivu jinsi mpinzani Odinga anavyoheshimiwa na utawala. Hapa kwetu usipopatwa na risasi basi ni rumande kila siku.
Heshima ni jambo la bure, ukijiheshimu, utaheshimiwa!
Kweli heshima ni jambo la bure.
 
Madeni ya taifa ya Kenya navya kwetu hayajapishana sana. Lakini Kenya kuna flyovers sisi tumepata darasa la Mfugale juzi. STD gauge inakaribia kukamilika. Kenya Airways inatekenya mawinguvya Trump.
 
Madeni ya taifa ya Kenya navya kwetu hayajapishana sana. Lakini Kenya kuna flyovers sisi tumepata darasa la Mfugale juzi. STD gauge inakaribia kukamilika. Kenya Airways inatekenya mawinguvya Trump.
Naona unajaribu kubadili gia angani hovyo kabisa
Deni LA Kenya ni Mara 3 ya tz
 
Back
Top Bottom