Nawaombeni tumshauri huyu mtanzania mwenzetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawaombeni tumshauri huyu mtanzania mwenzetu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by UZEE MVI, Oct 31, 2012.

 1. U

  UZEE MVI Senior Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Salama wakuu. Habari za jioni na poleni sana na majukumu ya ujenzi wa taifa? Natumai mu wazima. Niko karibu na kijana mmoja hapa anahitaji ushauri juu ya shida iliyomkuta ndani wiki mbili zilizopita. Hebu nivae koti lake na kuwaeleza kilichomsibu.

  Naitwa X naishi na kufanya kazi mkoani Mbeya. Nina mchumba wangu aitwaye Y mabaye tulianza urafiki tangu mwaka 2009 ambaye kwa sasa anaishi Dar. kutokana na sababu ambazo wote hatukuzielewa mapema tulijikuta tuna mtoto mmoja amabaye sasa ana anakaribia kufunga mwaka wa pili. Tumeendelea kushirikiana kumlea huyo mtoto hadi leo na tumeendelea kupendana na kuheshimiana kama kawaida japo kuna mambo madodo madogo ambayo yalitufanya tugombane lakini tuliyaongea yakaisha.

  Kutokana na hali ya kipato kuwa duni nimechelewa kukiri mbele ya wazazi wake kuwa mtoto ni wangu na kwamba mama yake(yaani mchumba wangu) nitamwoa, Japo wazazi wake wote wananifahamu na nahusiana nao vizuri lakini nilikuwa sijafanya ile mila.

  Mara chache nimejaribu kufanya hivyo lakini nilishindwa kwa sababu ya kipato.(mimi ni fundi seremala) Miezi michache iliyopita nimejikusanya na kujikaba kila kona ili niweze kutimiza mila na hatimaye niweze kukabidhiwa mke na mtoto. Wazazi wangu wote wawili na wazazi wake wanajua juu ya maandalizi haya na kwa upande wa wazazi wangu, wameshajiandaa kwenda dar kutekeleza hili jambo. Mawasiliano yameenda vizuri lakini wiki mbili zilizopita mchumba wangu Y amesema tusitishe hii safari, unless kama naenda tu kuona mtoto wake, ila kwa upande wake yeye tayaria na mtu mwingine.

  Sasa nimechanganyikiwa. nadhani hii imekuwa ghafla kwangu.

  Naomba ushauri wenu, nifanyeje?
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kaa chini na kumshukuru Mungu kwa kuliruhusu hilo likutokee, BARAKA au LAANA ni Mungu pekee ajuaye!
   
 3. charger

  charger JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Baba gani wewe? Yani sababu ya kipato ndio inakufanya umkane mtoto wako?Umechanganyikiwa nini sasa?wacha wanaojua majukumu waoe bana,you are not a right candidate for her.
   
 4. charger

  charger JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Baba gani wewe? Yani sababu ya kipato ndio inakufanya umkane mtoto wako?Umechanganyikiwa nini sasa?wacha wanaojua majukumu waoe bana,you are not a right candidate for her. Ndio nyie mnakimbiaga familia mambo yakienda kombo.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  dah, pole zake sana.
  Hamna cha kufanya zaidi ya kutulia kwanza au kushirikisha wazazi wake.
   
 6. s

  seriyamfongo Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna kuchanganyikiwa acha aolewe kuwa na mawasiliano namwanao zichange badili aina ya maisha
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kamkomboe mwanao, kuolewa kwa huyo mwanamke hakubadilishi kuwa wewe ndo baba wa mtoto
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Mkuu hajamkana ila amesema tuu hajakiri kwa wazazi wa mke kuwa atamuoa mtoto wao na atamchukua na mtoto
  Hilo lilikuwa kosa lake
  Mkuu mpe ushauri tuu kuwa mambo ndo yamekuwa hayo na amshukuru Mungu kwamba limetokea wakati bado hajakamilisha kile alichotarajia
  na kwa upande wmingine huyo mwanamke al;ikuwa na huyo mtu wake mapema tuu kama ni kuzuga alikuwa anam,zuga jamaa kuwa mambo yako sawa wakati huku kashapanga mamo mengine
  Amshukuru Mungu wake aendelee na masuala mengine haki ya mtoto wake iko pale pale hata kama huyo mama yake ataolewa na mwanaume mwingine
  Na anaweza kuanza taratibu za kumpata mtoto wake iwapo ana uwezo wa kumlea na yeye ajipange kimaisha sasa kupata mke mwingine
   
 9. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mbona iko poa, mchukue mwanao mwache aolewe.
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anyway haikua rizki yako,
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Usijali wala usichanganyikiwe ni bora ame kwambia ukweli kuliko unge muoa alaf atoke nje!

  Kubali matokeo we endelea kupeleka matumizi ya mtoto!
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Heshimu maamuzi yake, shika hamsini zako.Lipitalo hupishwa kwani mchama ago hanyeli,huenda akauya papo na zaidi ya hapo, mtoto akililia wembe mpe.

  Ukilazimisha unaweza kukutana na makubwa, madogo yana nafuu.

  Heri nusu shari kuliko shari kamili, na asiyekubali kushindwa si mshindani. Vile vile tafuta mwingine wako kwani kila chombo kwa wimbile, ibilisi wa mtu ni mtu, pia dawa ya moto ni moto na avumaye baharini papa kumbe wengine wapo.Usihofie mwanako kwani kuku havunji yai lake, wala usimtelekeze kwani damu nzito kuliko maji, na juu ya yote mshale kwenda msituni haukupotea.Kumbuka mtupa jongoo hatupi na mti wake na mwana mpe mwanga kulea.

  Usiwe na kisebusebu wala kiroho papo kwani kwa kila asemaye mla mla leo mla jana kala nini kuna jeshi la kusema ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.

  Mwapiza la nje, hupata la ndani ilhali usije kushangaa mwenda tezi na omo kurejea ngamani na ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.

  Kwa sasa ni hayo tu
   
 13. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  waeleze wazazi wako na muwaziliane na wazazi wake juu ya mtoto wako maana tayari ameshapata mtu mwingine na tulia utampata aliye chaguo lako maana mke ni mipango ya mola
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mtoto huyo wa mme mwenzie
   
 15. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  lea mtoto anatosha huyo moja
   
 16. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kubali yaishe...ubadhani dar ndio mbeya...wanaume walishakamatia bby huyo na wanampiga raha za mujini bana....mapenzi ya mbali hayapo ndungu zanguni...watu wanapitiwa mbavuni wakiwa wanaishi ndani ya nyumba moja ndio iwe mikoa tofauti.
   
 17. U

  UZEE MVI Senior Member

  #17
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa niaba ya X nashukuru sana kwa ushauri wenu. Mungu awabariki sana. samahani kwa kukaa mbalia na jukwaa tangu jana. Hii ni changamoto tu ya shughuli za maisha.

  Namfikishia ushauri huu wa awali ili achanganye na zake kabla ya kuamua nini cha kufanya.

  Thanks all. Thanks JF.
   
 18. N

  Natalia JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hela ya kumuoa unadunduliza .nani Anataka kuolewa na mdunduliza.Get rich fast trust me money matters.mimi nilikuwa sidate mwanaume maskini.na nimeolewa na very wealth men.
   
 19. N

  Natalia JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kuna mtu anataka mwanaume anaedunduliza?
   
 20. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,926
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280


  kabisa
  dada kampata muungwana anaekutunzia had mwanao unaleta tambo??
  Punguza basi hashuo,,omba mungu utapata chaguo lako
  ila ndio ujifunze sasa,kumjali mtoto sio lazma uwe na kipato,wangapi wanaish maisha ya labda vijijin lakini wana familia zao?
  Tulia endelea kuranda mbao mkono uende kinywani nduguu
   
Loading...