Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe - Pasco

Safi Pasco kwa ungwana huo.

Binafsi nimefurahishwa na uamuzi wako wa kiungwana, kwani siku zote muungwana hukubali kukosolewa na kujifunza kutokana na makosa yake. BIG UP !!

Lakini pia bado hujamuelewa vizuri Mh. Mbowe kuhusu kumtambua Rais.

Mh. Mbowe alisema kwa mujibu wa katiba JK ndio Rais na hawawez kupinga popote kutoka na katiba ya sasa, na wao wanAchopinga ni mfumo mzima uliompa ushind JK na sio urais wa JK. hiki ndicho walichotokea bungeni..KUPINGA MFUMO MZIMA ULIOMPA URASI JK NA SIO KUPINGA URASI WA JK. Hili Mh. Mbowe alishalirudia kulisema mara kwa mara, hata kwenye mdahalo na Mh. Hamad alilisema hili. Pia Dr. Slaa alilisema hivyo hivyo. Hii ina maana kwamba shinikizo la kutoka bungeni ni kushinikiza mabadiriko ya mfumo wa uchaguzi,uundwaji wa tume na kubadirishwa kwa katiba, ..KUTOKA KULE BUNGENI HAKUKUWA KUSHINIKIZA JK AJIUZULU..Pasco naomba ULEWE VIZURI HAPO.

Pamoja ktk mchakato wa mabadiriko.

MWANGAZA.
 
marytina, hili pia nililitegemea ndio maana nikasema, natumaini msamaha wangu utaeleweka lakini sio lazima ukubalike. Unapofanya kosa na ukatambua ni kosa, unaomba msamaha na liability yako inaishia hapo, it is up to anayeombwa msamaka kukusamehe au la, ndi maana nikakubali, kuna watakao kubali na kusamehe, na kuna ambao hawatakubali na hatawasamehe ila mimi nimetimiza wajibu wangu.
 

....Marytina,

Ndio mind yangu ilivomsoma mkuu hapo juu......! hajakubali kuteleza kabisa, kaleta siasa tu hapo!
 



Mbona uliisha eleweka! na wala hukustahili kumuomba mtu yeyote msamaha. lakini hapo kwenye red impliedly una send the same messege!
 
Pamoja na angalizo hilo, haikusaidia watu kunielewa
Hii sentensi ndo ilovuruga uombaji radhi wote! Ni sawa na kusema naomba radhi kwa sababu that's what is expected of me ili kuishi kwa amani JF lakini mimi ndie ambae watu walishindwa kumuelewa
 
Pasco, wenye kusoma tumesoma.. lengo lako limeeleweka na sidhani kama kunahaja ya kulumbana na yeyote yule

An apology is an apology... sometimes justifications are not needed
 
Pasco, mwenye macho haambiwi ona...Huwezi kumuita mtu rais kama sio rais au mke wangu kama sio mke wako. Binafsi sijaona ulipokosea..
Mapambano, kwenye kutomtambua rais, kuna mambo matatu, Disown, Disregard na Disrespect.

Disown ni kukana, kama inapotokea wazazi wakana watoto wao, yaani hakutambui tena kama wewe ni mwanae, lakini haindoi a fact kuwa yeye ndiye mzazi wako.

Disregard ni kutotambua uwepo wako/mtu au rais- Hii ni japo upo, wao wanakuchukulia kama haupo na ndipo hapa ilikuja ile hoja ya kudoka nje.

Disrespect, ni ile ya kutambua uwepo wako lakini hawakuheshimu, huku kutokuheshimu ndicho kiliwatoa Chadema nje siku ile, na kutafsiriwa ni dharau kwa rais.

Kauli ya Mhe. Mbowe, ili defeat hoja hizo zote tatu, kwanza ilionyesha wamekubali kuwa JK ndiye rais, hata kama wao hawamtambua, this is fact, rais ndiye yeye na ile kuapishwa tuu, ndio kumlegalize, wether unamtambua, unatambua uwepo wake, its immateria, iwepo wa rais is a fact na yupo, no one can deny that.
Walibakiza mambo mawili, kumdis regard na kum dis respect na hapa ndipo na mimi nilipochanganya, kwa kumshukuru na kumpongeza, nilidhani ndio regarding na kumrespect, but I was wrong.

Chadema hawataki njia ya mkato, kwao uhalali kwa rais aliyeingia madarakani, ni njia alizotumia kuingilia huko madarakani, this is not a fact, its a morals standards kutumia principle ya 'The means justfiy the end', if not the right means, hata the end is not right.
The realy true facts ni 'The end justfy the means', na huu ndio ukweli uliopo na usio pingika, tumefanya uchaguzi, no matter how horrible the means zilizotumika, at the end, tukampata rais, this is fact, sasa kwa vile huyu rais, yupo, yeye ndie rais no matter how bad means zimetumika kumpatia ushindi.

Uchaguzi wa 2005, JK aliingia madarakani kwa kutumia more crude means kuliko hata huo uchakachuaji wa matokeo. Watu waliuliwa, wakapigwa picha za photoshop na marehemu na waliofanya haya wakawa rewarded!. Kagoda was alsio the means! lakini ndio kwanza tukamwimbia nyimbo za shangwe na mapambio, ya Chaguo la Mungu!.
 
Pasco, mwenye macho haambiwi ona...Huwezi kumuita mtu rais kama sio rais au mke wangu kama sio mke wako. Binafsi sijaona ulipokosea..

mbowe anamtambua jk kama rais wa jmt, ila dr.slaa yeye hamtambui jk kama rais wa jmt. Matendo na kauli za hawa viongozi 2 wakuu wa cdm yanadhihirisha wazi kukinzana kwao, mkubali au mkatae ukweli unauma japo mambo yako wazi tena sana, peupe hadharani! Natoa changamoto kwa mbowe na dr.slaa, kama wanabisha jambo hili basi waitishe pc kwa pamoja, na watoe kauli yao kuthibitishia umma wa tz msimamo wao wa kutomtambua jk kama rais wa jmt.
 

Kwa faida yangu hebu nifahamishe kwa lugha nyepesi zaidi kwa nini 'you were wrong'.
 
We need people like you in this country.
Ni ukomavu mkubwa sana uliouonyesha.
Utazidi kuheshimika hapa jamvini.
 

Hiyo kwenye red inanipa taabu saana kuamini 'kauli na matendo' yao, napata saana kigugumizi kutanabahi mlengo wa siasa & wanasiasa wa Tanzania kwa demands zao ni nini hasa ili tujue, wanatufaa kimageuzi ama ndio ileile hadithi ya kugeukana na kusigana?
 
we pasco huna lolote... Umeomba radhi gani sasa hapo?? Wakati msimamo wako ni ule ule??? Huo ni unafiki na kuwachora chadema,,, bora ukae kimya... Na nyie uma mzima wa jf mnakaa mnaompongeza kwa kuomba radhi ya kinafiki na kizandiki??? Kueni great thinkers..
 
Hongera mkuu! huuni uungwana, wachache hufanya hivyo, ingawa ukweli utabaki palepale wamemtambua Raisi kikatiba.
 

Safi. muungwana halisi
 
Mkuu Pasco nimekupata vizuri sana.Nimesoma between lines na kukulewa.Binafsi nimefurahi sana na kufarijika sana kwa hatua hii.Kwa hakika wewe ni mwanaume tena wa shoka.Ni nadra sana kwa watu hasa wanaue kuomba msahamaha iwe kwa kweli au kwa kebehi huwa ni ngumu,nakusifu sana na kukupongeza sana.Hata kama umejitahidi kujitetea lakini kitendo cha kutamka naomba radhi mimi kwangu ni msamaha tosha.Hata heading tu inatosha kujiridhisha kwamba umeomba radhi.

Narudia tena nimefurahishwa na maamuzi yako kwani msingi wa mimi kuanzisha sredi hile ilikuwa ni kuondoa dhana potofu iliyojengwa kupitia sredi yako.Kama ulivyosema tunauelewa tofauti,na katika hili bado misimamo ya watu inatofautiana kutaokana na uelewa.Mazingira ya siasa Tanzania ni magumu sana hivyo ukiwa nje ya siasa ni ngumu kuelewa kwa undani,tulioko ndani tunafahamu na kuelewa vizuri.Uhondo wa ngoma ni uingie ucheze sio kutazama tu. Na kwa bahati mbaya sana watu wengi hasa tulioko nje ya siasa au tunaofuatilia siasa za vitabuni huwa tunadakia sentensi moja moja bila kukaa na kutafakari kwa kina na mazingira yenyewe ya kisiasa na ukweli halisi.

Mkuu kwa sredi yako hata wale wanoishia kusoma vichwa vya habari peke yake ujumbe umefika.Tupo kwenye line moja.

Thank You once again.

Aluta Continua
 


Mh. Regia,
Nimefurahi kuona umeikubali apology ya mwenzetu Pasco, daima tudumishe uungwana kwa mustakabali mzuri wa ustawi wa taifa letu. Nakutakia wajibu mzuri bungeni na inshallah hoja zako za kupewa umeme jimboni mwako lifanikiwe, hoja yako bungeni juu ya kutupiwa jicho walemavu nakutakia usikilizwe na upate kuungwa mkono.
Kheri njema kwako Mheshimiwa.
 

Mkuu hapo kwenye bluu sina swali!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…