Hata mie nawalaumu, ni ujinga kukubali kugeuzwa na mwenzio kuwa gunia la mazoezi, kuna wanaume wanyanyasaji jamani usiombe kuolewa na mume wa aina hiyo, hasa wanaume wa Bara na kanda ya ziwa, ni wanyanyasaji kitu cha ajabu......... Mie akha, wala siwataki........ Mungu aniepushie nao mbali...............
Mtambuzi wanawake wengi wapo katika disadvantaged situations.... Wanawake tulikua chini saana... Hatuna maamuzi, hatuna sauti wala hatuna pa kukimbilia. Jamii imesukwa mno na mfumo dume kila sector kila mahala na kila ushindako.... Na tokana na the fact kua hatuishi in isolation hio ndo ufanya wanawake wengi kuvumilia mambo ambayo hastahili kuvumilia... I am telling you such a woman Usimjudge... just try to understand her kwanza for unakuta hivi vigezo vyaweza play part...
Taasisi ya Familia...
Kazaliwa katika familia ambayo mtoto wa kiume ndio mwenye say... yeye katika macho ya wazazi wake hana maana wala hana thamani for the simple reason kua ataolewa huyu sio wetu hapa: sad but ukiangalia kuolewa kwenyewe unaenda hadi badilisha surname... waweza mlaumu kaka or baba kusema na kufikiri hivi?? Yahitaji busara kupembenua hili... Hio tayari inamfanya ajisikie she does not belong kwao na hali ndio moja ya sehemu ambao mwanadamu inabidi ajisikie huru kuliko woote.
Taasisi ya Dini...
Inaonesha kabisa kua imesisitizwa mwanamke awe mnyenyekevu na msikuvu kwa mumewe... na kama mumewe anatenda dhambi basi walau afanye maombi na afunge ili kuhakikisha kua mumewe arudi katika mstari.... Mfano dini ya kikristo... Divorce is out of question... Dini ya kiislam as much as wanasema hata mwanamke aweza dai talaka... mumeo asipoandika hamna kuachika; ingawa haipo wazi kua hata mwanamke aweza andika.
Taasisi ya Elimu...
Elimu ya shule ni yakubangaiza... usipofaulu imekula kwako... na hata waweza faulu but shule usinuse pia... Ama ukaendelea vizuri but sababu nature nayo ucheza mkondo wake ukajihusisha na mambo ya ngono na kuishia kupata mimba which in most cases shule inakua kaput! Wamama tuna vikwazo vingi saana vya elimu mpaka ukafanikiwa ukapata degree... Thank God! Hio mara nyingi humfanya mtu maisha mbeleni yawe bleak...
Ukija upande wa tamaduni....
In short jamii zetu zinataka (makabila mila na tamaduni) zinakumbatia saana wanaume na kukandamiza wanawake either directly or indirectly... Ukiolewa mahali utafikir mtoto wa kike unauzwa... Usiombe makabila yale wanayo thamini binti bikira ama weupe... Mahali inayotolewa hapo kuirudisha ni mziki mnene in case ukibadili mawazo. Mwanamke aruhusiwi kabisa kuonekana akienda kinyuma na mumewe hata kama mumewe ni kilaza.... Sad.
Taasisi ya Ndoa...
Ndoa ni moja ya taasisi ambayo yaweza mmaliza kabisa mwanamke asipoangalia... Maisha ni magumu na mambo yaenda yakibadilika kila siku... Tumeona jinsi idadi ya wanawake waloacha career zao sababu tu kaolewa ilivo kubwa.... Mumewe hapo anamshawishiwi kwa maneno mazuri (after all ndoa ni mpya hivo mapenzi moto moto); for wanaume walo wengi anajihisi safe kama mkewe anashinda tu nyumbani akifanya reproduction na kuangalia nyumba... yaani kila akija home amkute mkewe ndio raha yake... By the time maisha yamebadilika na unagundua huna nyuma wala mbele bila kuwekwa in the same line na mumeo... inakua too late...
Note that hili tatizo sio wanawake woote... na sio wanawake wale ambao hata tuna uwezo wa kuingia hapa JF na kubadilishana mawazo hapa... Namzungumzia Mwanamke yule wa Kitanzania wa kijijini... ama kama ni mjini bado hajakomboka... Namzungumzia Mwanamke yule ambae mpaka leo haamini kua mwanamke aweza simama bila mwanaume.... Nazungumzia hao sababu ndo idadi ilotawala hapa inchini kwetu... Hivo basi Please do not judge them... try and understand them... It is not right but ndo reality!! Ni kweli kua sasa imekua ni nafuu but bado tuna safari ndefu....
AshaDii, ahsante kwa uchambuzi wako YAKINIFU....... umenisaidia sana kuisherehesha mada hii kiasi kwamba, naona haya kuikosoa. Hata hivyo, nashawishika kidogo kuweka angalizo. kama umesoma mada yangu vizuri utakubaliana na mimi japo kidogo kuwa sina maana ya kuwashawishi wanawake ambao ni vichuguu kupambana na wanaume ambao ni sawa na mlima Kilimanjaro. La hasha, sikuwa na maana hiyo......lakini hata hivyo ni vyema ikafahamika kwamba inawezekana kabisa kuuondoa mlima mkubwa kwa kuanza na mawe madogo madogo, hapo ndipo dhamira yangu ilipokuwa.
Nilikuwa namaanisha kwamba, wanawake wakatae ule ukatili waliofanyiwa mama zao na baba zao na wakaona hayo ndiyo maisha halisi ya ndoa, ndio maana nikasema wawakatae mama zao. najua sauti yangu ni kama ya mwana mpotevu nyikani, kwa sababu haitawafikia wale kina mama wa Kitanzania hasa walioko vijijini, lakini hata hawa walio na access na mtandao na wanaosoma hapa JF, wanaweza kuwa ni chachu ya kufikisha ujumbe huu kwa wengine, ili kuepusha ubabe huu kuendelea.
Labda jambo usilolijua ni kwamba naandika kutokana na kile nilichokishuhudia, kwa sababau mimi ni mtoto wa mkulima na nimezaliwa na kukulia kijijini..................
Hata mie nawalaumu, ni ujinga kukubali kugeuzwa na mwenzio kuwa gunia la mazoezi, kuna wanaume wanyanyasaji jamani usiombe kuolewa na mume wa aina hiyo, hasa wanaume wa Bara na kanda ya ziwa, ni wanyanyasaji kitu cha ajabu......... Mie akha, wala siwataki........ Mungu aniepushie nao mbali...............
some of us are far too nice for our own distruction kisa kuwa mke mzuri. Uliona ile post ya the boss wanawake tulivyosupport cheating!
wanawake wana safari ndefu sana katika jamii kwani mlolongo ulio kwenye mila, dini, jamii etc wote unawaweka kama watu waliochini au wanaohitaji kushikwa mikono kuongozwa
BPM, kweli tuna safari ndefu sana kwenye hili suala hasa ukizingatia kuwa sisi wenyewe ( including hapa jf) ni mabingwa sana wa kukatishana tamaa! Take example, kuna member alishawahi kupost hapa akielezea nia yake ya kutaka kumsaidid jirani yake aliekuwa ananyanyaswa na mumewe. Maoni mengi aloyapata ni "usijaribu kuingilia ndoa ya watu"/"mambo ya ndoa waachie wenyewe"!! Hivi tumuelimishe nani sasa?? Nachoka kabisaaa......