Nawakumbusha; Umakini ndio nguzo ya mafanikio

Nawakumbusha; Umakini ndio nguzo ya mafanikio

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Amani kwenu,
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka,nimeona niwakumbushe wanajamvi hili kwamba umakini katika kila jambo ndiyo nguzo ya mafanikio.

Ukiwa kazini,kwenye biashara, mchezo hasa ile ya watu wazima, na hata unapozungumza au kuchangia hoja humu jukwaani weka akili yako hapo,au kama unaona hujatulia acha wengine wachangie au wazungumze,

Kwanini ufanye kitu ambacho hujakielewa? Hata wanafunzi wanaofeli mitihani siyo eti hawajui majibu sahihi ila tu mara nyingi hawakuwa makini katika kuelewa swali.

Ushauri wangu, fanya mambo machache kwa ukamilifu kuliko kufanya mambo mengi ndivyo sivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ukumbusho, ila mafanikio yana nguzo nyingi ikiwemo juhudi na busara pia.
 
Back
Top Bottom