Nawajua wanaosaidia kukwepa kodi TRA - Kikwete

Sijaisoma thread yote... nimeiona kama ni upuuzi ule ule.

Anapotuambia anayo orodha ni ujinga KAMA kweli anayo tunataka kuwaona watu wakijibu tuhuma zao sio kujisifia tu mbele za watu. Haya hiyo orodha imemsaidia nini mpaka sasa?? Na ya madawa ya kulevya anaifanyia kazi mwaka wa sita sasa.... Kikwete CHIZI kama machizi wengine tu.
 
Ama kweli unanishangaza, wewe mpaka sasa unangoja kuiona action gani? mawaziri wamejiuzulu, wengine wameionja keko, vigogo wengi wapo keko, na wengine tumbo joto, duhhh, unanishangaza! Na hao wanapewa warning, first hand, wakae chonjo, JK naamini atawashughulikia kama kawaida yake systematically na sio kukurupuka tu ki-dikteta kama mlivyozwea.

Kuna tofauti kubwa mnooooo kati ya mahabusu na mfungwa!!!!!! Aliyefungwa katika uongozi wa kikwete ni mume mwenzie tu.... walioingiliana.

Na ni kwa kuwa haki haikutafutwa.

Wengine ni siasa. Na wewe unachukua murungula ili umuenezee maneno haya... kifupi huku sio mahala pa kumsifia KIONGOZI MLEGEVU sampuli ya kikwete.... kwani walioko huku wanaona na kujua kila kitu.
 
Nchi haiongozi na Kangoroo court. Hata kama rais anajua watu itabidi vyombo vya mamlaka husika zichukue sheria.

sasa rais anaripoti kwa mkuu wa TPA,amesema eti akimaliza kuifanyia kazi ataipeleka kwa mkuu TPA ndo awatimue kazi. Hapa tungekuwa na rais anayejitambua angerudisha list iyo TPA ifanyiwe kazi na ndo ataharifiwe kuwa watu kadhaa ndo wako matatani. Sasa rais anayeanza kazi ya mgambo ya kukamata kamata na kupeleka kwa mkuu TPA ni aibu! Na je wanaohusika kupeleka majina kwa Rais wa wabadhirifu TPA si mamlaka ya TPA au imeshindwa kazi?au kuna watu nje ya mamlaka wameamua kuwaharibia wenzio kazi?wanapeleka jina kwa rais,rais akae kwenye benchi na kupekua ukweli kisha akaripoti kwa Mkuu wa TPA ndo akawafukuze kazi. Ama kweli Tanzania inahitaji rais mweledi.
 
Tunakwepa kodi kwa sababu ni kubwa na mzunguko wa kutumia njia sahihi uchukua siku nyingi sana kitu cha siku 3 unapata kwa mwezi.
kwa upande mwingine tazama kigali cha mil 5 unaweza kulipa mpaka mil 4 hii ni kodi kubwa sana na ukiwa wewe ni mfanyabiashara lazima ujitahidi kuikwepa ili ubaki kwenye biashara yako la sivyo hasara tupu
 
Hivi zile orodha za ;
  1. wauza madawa ya kulevya,
  2. wala rushwa,
  3. wakwepa kodi
  4. wezi wa magari,
zimeenda wapi ?
 
Huu uzi unanikumbusha enzi za raha ya kuanzia Jambo forum.

Mbarikiwe wadau tuliotoka mbali ndani ya JF, bila kusahau na wengine pia waliojiunga, walitutangulia, etc
 
Back
Top Bottom