Nawajua wanaosaidia kukwepa kodi TRA - Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawajua wanaosaidia kukwepa kodi TRA - Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 3, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  2009-03-03
  Na Joseph Mwendapole


  Rais Jakaya Kikwete amesema ana orodha ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wasio waaminifu ambao wanashirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

  Alisema anaifanyia kazi orodha hiyo na akishamalizana nayo atamkabidhi Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, ili achunguze na kuwafukuza kazi wafanyakazi watakaothibitika kujihusisha na vitendo hivyo.

  Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na wadau wa bandari Tanzania alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni ufuatiliaji wa agizo alilotoa mwezi uliopita kupunguza msongamano wa makontena.

  Alisema serikali haiwezi kuvumilia watu wanaoikosesha mapato.

  Akitoa mfano namna wizi huo unavyofanywa, Rais Kikwete alisema wanaweza kuendesha zoezi hilo kwa simu ambapo mtu aliyeko Dubai anapewa maelezo namna atakavyojaza fomu ili mzigo wake usipite kwenye scanner, hali inayoweza kupitisha mizigo haramu kama dawa za kulevya.

  Alisema wafanyakazi na wafanyabiashara hao wanatumia udanganyifu kuwa kontena hizo zimebeba mitumba, kumbe ndani ya mitumba hiyo wakati mwingine inatumika kufunika magari.

  ``Ninayo orodha ndefu na nitaikabidhi kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kitilya ili awafuatilie na ahakikishe anawatimua kazi mara moja wale watakaobainika wanahusika na mchezo huo ili tuanze upya,`` alisema.

  Alisema serikali haiwezi kuvumilia kuwa na wafanyakazi wanaokula njama za kuipotezea mapato.

  Kikwete alisema bandarini kuna uzembe mkubwa ambao hauvumiliki na aliuagiza uongozi kuondoa matatizo yaliyopo badala ya kukaa na kunung`unika.

  Alisema msongamano wa makontena umekuwa ukiisababishia serikali kukosa mapato mengi na alisisitiza kuwa bandari ni sehemu muhimu ambayo serikali haiwezi kuiacha iwe ya hovyo.

  Akiwa katika kitengo cha kuchunguza bidhaa katika kontena, Tiscan, Rais Kikwete alisema maelezo aliyopewa na TPA yanatofautiana na yale aliyopewa na viongozi wa Tiscan.

  ``Hapa mbona mimi sielewi naomba mnieleweshe, hawa Tiscan wanasema wana uwezo wa kuchunguza hata makontena 200 kwa siku ila wanasema tatizo ni nyinyi hamleti kontena za kutosha... Jamani fanyeni kazi na muachane na visingizio na malalamiko,`` alisema Kikwete.

  Aliagiza mamlaka hiyo impe taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa upunguzaji wa makontena ndani ya wiki mbili zijazo na aliahidi kutembelea tena bandari hiyo.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Forodha, Otieno Igogo, alimweleza Rais Kikwete kuwa wadau wa Bandari ya Dar es Salaam walikubaliana kulipa dola 30 ikiwa ni gharama za kuhamishia kontena moja katika bandari kavu.

  Igogo alimweleza Rais kuwa ingawa wadau wote wamekuwa wakichangia, Kampuni ya Kimataifa ya Kupakua Kontena Bandarini (TICTS), imegoma kutoa fedha hizo.

  Alisema dola 30 ambazo TICTS walipaswa kulipa kwa kila kontena linalohamishiwa bandari kavu kama wanavyolipa wadau wengine, zimekuwa zikitolewa na TPA.

  Baada ya kauli hiyo ya Igogo, Rais alisema anashangaa kuona jeuri hiyo ya TICTS na kusema kuwa TPA ina mamlaka, lakini haitaki kuyatumia.


  Kikwete alisema TPA imefanya vizuri kulipa gharama ambazo TICTS imekataa kuzilipa, lakini aliagiza mamlaka hiyo ihakikishe TICTS inazirudisha mara moja.

  ``Nyinyi mnashangaza sana, mna mamlaka, lakini hamyatumii... Sasa hizi gharama lazima walipe na wakiwashinda mwelezeni waziri na waziri akishindwa niambieni mimi,`` alisema.

  Wakati huo huo, Kikwete alikataa maelezo marefu ambayo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraem Mgawe, alitaka kuyasoma mbele yake na badala yake akamtaka amweleze sababu za msongamano kutoma lizika.

  Baada ya kuelezwa hivyo, Mgawe alimweleza Rais Kikwete kuwa kikosi kazi kilichoundwa kufuatia agizo lake kinaendelea kujitahidi kuondoa msongamano uliopo.

  Alisema Mamlaka inatarajia kuwa utekelezaji wa mikakati iliyowekwa itafanikisha kupunguza hali ya msongamano mwezi Machi mwaka huu.

  Mgawe alisema katika kipindi cha mwaka 2007/08, TPA ilihudumia tani milioni 6.239, ambalo ni ongezeko la tani 227,222 au asilimia 3.8 ikilinganishwa na tani milioni 6.003 zilizohudumiwa mwaka 2006/07.

  Alisema katika kipindi hicho mamlaka ilipata ziada ya Sh. bilioni 37.879 kutokana na mapato ya Sh. bilioni 168.789 na matumizi ya Sh. bilioni 133.909.
   
 2. Y

  YE JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama anawajua si awachukulie hatua. Yeye ndie kiongozi mkuu, au anataka waunde tume tena?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu, hii ni siasa tu, na pengine nathubutu kusema kuwa ni usanii tu, hali inayotawala vita nzima dhidi ya ufisadi. Kuna kelele nyingi za dhamira kuhusu kuwashighulikia mafisadi, lakini results zinakuwa hakuna, au kama zipo ni za ubababishaji tu.

  Rais alitakiwa amwite mkuu wa TRA kimya kimya na kumkabidhi list yake ya hao wakwepa kodi na kumwambia mkuu huyo kwamba anachotarajia ni results toka kwake. Wananchi tungetangaziwa tu hizo results – kwamba "fulani na fulani wako mbaroni na watafikishwa kortini."

  Mfano mwingine: Miaka michache iliyopita, wakati Magufuli akiwa waziri wa miundombinu, alihutubia mkutano wa wafanuakazi wa Tanroads. Alisema kuwa amegundua ufisadi katika idara hiyo kuhusu ununuzi wa magari – yaani kulikuwapo magari yamenunuliwa kwa bei maradufu ya ile halisi.

  Huo pia ulikuwa usanii – alitaka tu atangazwe katika vyombo vya habari kwamba yuko makini katika vitendo vya ufisadi. Hata hivyo issue iliishia hapo hapo, wananchi hatukuelezwa tena kilichotokea, bila shaka hakuna kilichotokea.

  Kimya kimya Magufuli angeamrisha uchunguzi mkali ufanyike na wahusika kukamatwa na kufikishwa katika vuyombo vya sheria – na hapo ndiyo angetangaza kuwa "fulani na fulani, wamekamatwa katika ufisadi ndani nya Tanroads na tayari wamefikishwa mahakamani."

  Wananchi tumechoka na kelele za dhamira tu, tunahitaji vitendo na hasa hasa results.
   
  Last edited: Mar 3, 2009
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ....majina, majina, majina, orodha, orodha, orodha, ahadi ya kuwashughulikia, ahadi ya kuwashughulikia....Surely we have heard all this before?? Time someone ACTED!!!!!
   
 5. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwani majina na orodha ya watu wanaojihusisha na madawa ya kulevyo imeishia wapi? na hii orodha nyingine tena ambayo itakuwa yaleyale.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naamini hata orodha ya majina ya wanao uwa maalbino na vikongwe pamoja na ya majambazi anaijua.
  Ila Kikwete ana maradhi ya kuogopa kuonyesha kuwa yeye ni Raisi,kuonyesha kuwa yeye ni Jemedari ,na hili ni kuogopa kuchukua hatua kwani huenda aliyonayo yeye ni makubwa kuliko au yanalingana na hawa waliomo kwenye orodha ,hivyo basi endapo atachukua hatua baada ya kumaliza miaka yake mitano ,atakaekuja hatashindwa kumchukulia hatua kama anavyozichukua kwa wenzake ,ndio anaendelea kuwasitua na kuwatahadharisha tu ,kuwa wapunguze kasi.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ..............heartbreaking!!!!!!!!!! especially coming from the top
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wakwere hupenda porojo!
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ama kweli unanishangaza, wewe mpaka sasa unangoja kuiona action gani? mawaziri wamejiuzulu, wengine wameionja keko, vigogo wengi wapo keko, na wengine tumbo joto, duhhh, unanishangaza! Na hao wanapewa warning, first hand, wakae chonjo, JK naamini atawashughulikia kama kawaida yake systematically na sio kukurupuka tu ki-dikteta kama mlivyozwea.
   
 10. Y

  YE JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mjomba ndio maana ukaona neno usanii likisemwa, hivyo vyote ulivyoandika ni kama ngoma za kibisa, yaani joka linachezewa na watu lakini haling'ati.

  Tanzania nchi yangu, tutaacha lini maigizo?
   
 11. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Tusikate tamaa. Tumpe nafasi ila ajue porojo zake zitamponza.

  Alisema ana orodha ya majina ya wanaohusika na madawa ya kulevya na kuahidi kuitoa hadharani,mpaka leo kimya.

  Leo anayo majina ya bandarini! Alienda kufuata nini kama anajua kwamba hao wakwepa ushuru na wababaisha bado wapo hapo? Si angeagiza waondolewe halafu akaangalie ufanisi baada ya wazembe na wakwepa ushuru kuondoka. Au amewatahadharisha kama alivyofanya kwa wala rushwa wakati akiandaa 'script' Igizo linaloendelea sasa?
   
 12. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #12
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata wauza madawa ya kulevya orodha anayo miaka mitatu sasa, lakini story ndo hiyo tu mpaka amalize muda wake wa kutawala. angalia yesijewafikia ya mwenzao Chiluba na wengine. yangu macho na masikio...
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Ana list ya wauza unga kaikalia mpaka leo. Ana list ya waliorudisha shilingi 70 billioni za EPA kaikalia hadii hii leo sasa pia ana list ya wafanyakazi wa TRA wanaowasaidia mafisadi kukwepa kodi hii nayo kama kawaida ataikalia.

  Kikwete hatufai Watanzania miaka mitano aliyokaa madarakani inatosha kabisa sasa CCM waanze mikakati ya kumtafuta mgombea wao wa 2010 maana wapinzani nao hawataki kuungana ili kuunda chama chenye nguvu na kuichukua nchi. Lakini Kikwete asiruhusiwe tena kugombea maana uongozi umemshinda kabisa.
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Pia ana orodha ya MAFISADI iliyotolewa na Dr. Slaa - bahati mbaya na yeye yumo !!! Jamani mwataka akate mti alioukalia ???
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Naam hakuna ubaya wowote akifanya hivyo.
   
 16. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkulu, mi nadhani mkulu hajui kazi yake. labda kama alivyosema mkulu hapao juu, wakwere ndivyo walivyo. Jamaa anapenda kusautana na sio kuonyesha uhai wa madaraka yake
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mnataka iweje? ukikosowa utoe na ushauri kifanyike nini?

  Tuwe waa kweli kidogo. ni Raisi gani aliyeshughulikia ufisadi Tanzania zaidi ya Kikwete? na bado anaendelea kazi yake haijesha, lakini tukubali kuwa Kikwete sio Dikteta na anafanya kazi zake kufata sheria, sasa nyinyi mlitaka akamate hovyo, aweke ndani hovyo, kama alivyofanya yule mmasai? enzi za Nyerere? au ule ndio mnaona utawala bora? wa kusweka watu ndani hovyo?
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280

  Ufisadi gani alioushughulikia Kikwete? Wakati wa kampeni aliahidi kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini.

  Tangu aingine madarakani huu ni mwaka wa nne hajatimiza ahadi yake. Tune ya Mwakyembe ilishauri kuondolewa kazini Mkuu wa PCCB Edwards Hosea na Mwanashria Mkuu Mwanyika hadi hii leo wako kazini. Chenge na Idrissa Rashid kuna ushahidi wa kutosha kwamba walihusika na ufisadi wa Rada wote bado wanapeta kama mbunge na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO. Wabunge walishauri mkataba wa TICTS usitishwe lakini hadi hii leo Mkuu wa nchi yuko kimyaaaa. Alituambia kwamba mafisadi wa EPA walirudisha 70 billioni lakini hadi hii leo majina na kiasi kilichorudishwa na kila mmoja amefanya siri au labda hakuna hata senti tano iliyorudishwa ndiyo maana wanashindwa kuitoa hiyo list hadharani.

  Matatizo Bandarini, ATCL, TANESCO, Kiwira, Vitambulisho vya uraia, TRL. Hao waliofunguliwa kesi kama angeona kuna umuhimu wa kuzishughulikia kesi hizo haraka basi angeweza kabisa kuamuru kesi hizo ziendeshwe kwa siku tano kwa wiki au hata zaidi ili zimalizike mapema lakini zinapigwa kalenda tu na mwishotutaanbiwa hakuna ushahidi wa kutosha watuhumiwa wote wako huru.

  Ni ufisadi gani huo anaoshughulikia Kikwete? Kama una ushahidi wa kuthibitisha hilo basi uweke hapa jamvini vinginevyo Kikwete nchi imemshinda na kuinusuru inabidi aweke maslahi ya Taifa mbele ili asigombee tena 2010. Wakati wa kuoneana haya na kumuweka tena kiongozi madarakani hata kama kuna ushahidi wa kutosha kwamba uongozi umemshinda umepitwa na wakati.

  Tuwe wakweli kwa viongozi wetu na kuwa tayari kuwaambia kaa pembeni wapishe wengine wewe umeshindwa.
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kamishna na bodi nzima walikuwa wanasubiri wapate kalui yako ndio wafukuze......JK mimi naomba uanze nao hao hao makamishna.......
   
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ziara ya Kikwete – Bandarini na TRA (Je ni yeye au wasaidizi wake wameshindwa kazi?)

  Jana, Mh. Rais alifanya ziara ya ‘kushtukiza’ katika maeneo ya Bandari na TRA. Swali la kujiuliza; je, inamaanisha wasadizi wakuu wa rais wameshindwa kutekeleza majukumu yao? Kumbuka: Tunajua ya kwamba rais anamajukumu mengi ya msingi yanayosubiri utekelezaji wake katika kuendesha taifa letu.

  Kufikia rais kuacha shughuliza zake na kuingia mtaani kusimamia utekelezaji wa shughuli za idara za serikali yetu ni hatari kwa ufanisi wa maendeleo ya taifa.

  Swali la kujiuliza je Mh. Rais kazi ya usimamizi haiwezi? Au anaiweza lakini hawezi kukemea na kuchukua hatua kwa viongozi wazembe? [Mfano kwa kutoa orodha ya ‘mafisadi kodi’ pale bandarini na TRA]
  Au Rais ameshakata tamaa kwamba sikio la kufa alisikii dawa ([kwamba wasaidizi wake hawarekebishiki]

  Nikichukulia model za uendeshaji wa serikali katika eneo letu la kusini mwa bara la Africa, Mfano mzuri wa utawala bora ni Afrika ya Kusini, Hivi mfano itamchukua siku ngapi rais kuzungukia watendaji wake hili kujionea utendaji? Je kuna haja ya hawa viongozi wetu kuwa wanapimwa kutokana na utendaji na uzalishaji wao?

  Nimeshindwa kumweka fungu lipi Mh. Rais kati ya hayo hapo juu.

  Shadow.
   
Loading...