Nawajua mashoga 5, wote walianza kwa kufanyiwa dhuluma ya kingono utotoni

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182

3.jpeg

Abuu Kauthar

Nianze kwa kuelezea uzoefu wangu katika maisha wa kukutana na kuwajua mashoga. Nianze kwa kuomba msamaha kwa jina hilo kwani sina hakika kama ni rasmi na linakubalika kwao.

Nimepata kujuana na mashoga watano. Najua kuna makundi mengi katika hao wanaojitambulisha kama jamii ya LGBT, lakini nikizungumzia mashoga ninakusudia wanaume wanaofanyiwa mapenzi kupitia tundu la nyuma, ambalo limezoeleka kama ni kwa ajili ya kutolea mavi.

Watu hao watano ninaowajua wana jambo moja linalofanana. Wote waliingia kwenye tabia hiyo utotoni baada ya kunyanyaswa kwa muda mrefu, kingono. Mmoja wapo, nilimjua katika taasisi moja ya elimu, alinambia alifanyiwa mambo hayo na baba yake mdogo, mwingine ambaye ni mdogo wangu wa mama mdogo alinyanyaswa utotoni na jirani ya.

Mwingine ni kijana wa Kiarabu kule Dodoma ambaye alikuwa rafiki wa mjomba angu, akisoma shule ya Mazengo. Mara kadhaa alimfuata mjomba kumuomba amuombee dua aache tabia hiyo na kukiri kuwa ina uraibu mkubwa, kama wa sigara kwa liayezoea kufanyiwa. Kijana huyo naye alianzishwa mambo hayo utotoni na watu wazima katika familia yake. Katika hao watano, kila mmoja alikuwa na hadithi yake.

Sina sababu ya kutowaamini kwa sababu hayakuwa mazungumzo ya kipolisi au ya kuwahukumu bali ya kirafiki kabisa.

Kule Zanzibar na hata baadhi ya maeneo mengine, tunaambiwa, vitendo vya ulawiti wa watoto ni vingi mno. Baadhi vinang’amuliwa maopema, baadhi ya vitendo hivyo havijulikani na vinaendelea na kutengeneza mashoga.

Swali langu kwa watetezi wa LGBT, hawa nao waliingia huku kwa hiari?

Sina tatizo na mtu mzima, walau kwa uchache miaka 18 na zaidi, anayejitambua tayari, kuamua kuingiliwa kinyume akaifanya ni starehe yake lakini kuingizwa huko kupitia unyanyasaji haikubaliki.

Kwa hiyo, wakati wakina Mishy Singano, Fatma Karume na wenzao wanaowatetea mashoga wakiendeleza harakati zao, wachungulie takwimu na kuona hali mbaya ya ongezeko la vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume na kike, wachunguze mchango wake katika kuzalisha mashoga (bila hiari) na wajishughulishe na mapambano hayo.

Katika habari moja niliyoiona imechapwa katika tovuti ya Shirika la Habari la Ujerumani, Deutche Welle (DW) Jeshi la Polisi limenukuliwa kuwa visa vya ukatili na dhuluma ya kingono dhidi ya watoto mwaka wa 2020 ilifikia 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirikodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi jambo ambalo linatajwa kuwa linahatarisha mustakabali wa ustawi kwa watoto nchini humo. Dhuluma hizi za kingono ndio zinazalisha uraibu wa kupenda kuingiliwa kinyume.

Hawa vijana walioingizwa katika ushoga bila kutaka kwa kubakwa mfululizo utotoni wanapitia mateso makubwa mno. Wakienda kufanyiwa vipimo, hukutwa na hali mbaya ya kiafya, wameharibika. Starehe gani hii ya kuvunja haki za watu wengine ya kuwa na afya nzuri, eti kwa kizingizio kuwa ameridhia wakati kumbe wengi wanalazimishwa kwa kuanza kubakwa?

Jambo la pili ambalo nataka kuligusia kidogo ni hii tabia ya kutumia nguvu nyingi kupromote ushoga, jambo ambalo kusema ukweli linaathiri jamii ya LGBT kuliko kuwasaidia.

Jamii ya LGBT ilikuwepo miaka na miaka na ndio maana jambo la kuingiliana kinyume wanaume kwa wanaume au hata kwa wanaume kwa wanawake limetajwa kama dhambi kwenye dini nyingi kubwa. Zamani, hasa huku Afrika, walikuwepo walivumiliwa, kama walivyovumiliwa wengine wenye tabia zisizokubalika katika jamii.

Siku hizi upinzani dhidi yao umekuwa mkubwa kwa sababu wajiitao wanaharakati (ambao wenyewe wanapambana watoto wao wa kuwazaa wasiingie huko) wanatumia nguvu nyingi kulazimisha jamii ipende na ikumbatia tabia hizi.

Mi nadhani kwanza, wanaharakati wa LGBT waanze kuchunguza vijana wengi waliingiaje huko na wana maoni gani kwa hivi sasa? Je wangependa kusaidiwa kutoka (naamini hivyo) kwa sababu wengi wanafanya kwa uraibu, kama ilivyo kwa dawa za kulevya, sio kupenda?

Lakini, nina hakika wanaharakati wa LGBT hawawezi kufanya jambo lolote litakalopunguza idadi ya mashoga, ambao wamewafanya mradi wao wakichuma mabilioni kutoka kwa wafadhili. Wanaharakati wanapenda kutuaminisha kuwa mashoga wote wamekuwa hivyo kwa sababu ya kimaumbil.e.. sijui homoni na kadhalika.

Jamani! hivi ukiwa na homoni za kike ndio uingiliwe kinyume? Kwani kwa hao wanawake huko nyuma ni rasmi kama eneo la starehe? Mi nina hakika wanaharakati nguli wa LGBT, wakina nanihii hawajawahi kutoa ‘tigo’ kwani wanajua madhara yake ila wanahimiza watoto wa kiume wa wanawake wenzao wafyokolewe nyuma! Disgusting!

Wazazi wenzangu nawashauri tuwe waangalifu. Sibishi kuwa huenda homoni fulani huchangia kumsukuma mtu kwenye ushoga, lakini tusisahau sababu kubwa ya watoto wetu kuingia huko ni unyanyasaji wa kingono.

Wazazi, tuwachunge watoto sio tu dhidi ya manyang’au watu wazima wanaowamendea kutaka kuwabaka, lakini tuwalinde watoto wasifanyiane wao kwa wao na kuzoesha na tabia hiyo chafu.

Mwenyezi Mungu atuhifadhi na tabia asizoziridhia! Aaamiin
 
View attachment 2036883

Abuu Kauthar

Nianze kwa kuelezea uzoefu wangu katika maisha wa kukutana na kuwajua mashoga. Nianze kwa kuomba msamaha kwa jina hilo kwani sina hakika kama ni rasmi na linakubalika kwao.
Nimefurahi na hitimisho la mada hii ulivyomhuzisha Mungu kutukinga na ushoga.Kusema kweli roho ya ushoga inatoka kwa shetani ili awapoteze watoto wa Mungu kuiridhi nchi kama apendavyo Mungu.Kwa hiyo sisi wanadamu tunatakiwa kuisikia sauti ya Mungu anataka tuishi vipi.Tatizo letu hatuwezi kumwona au kumsikia Mungu kama binadamu.

Mungu ni Roho tukimtafuta na kuacha ubishi iko siku tutamsikia kwa imani.Ninachotaka kusema hakuna jamii au serkali inayoweza kupambana na ushoga na yanyofanana na hayo kwa nguvu zetu pasipo kumsikiliza Mungu.Asante sana kwa mada yako
 
Mtaa ninaokaa kuna jamaa mwaka juzi amefungwa miaka 30 jela Kwa kosa la kuwaingilia watoto wa kiume wa pale mtaani.Vitoto vidogo vya miaka 6,7,8 alikuwa anavitia vidole alafu anavitisha wakisema atavichinja,siku moja kitoto kimoja kikarudi home kinatmbea huku kimepanua mapaja,mamaake akamuuliza anajibu huku nyuma kunauma,akamkagua alichokikuta.

Jamaa alitegewa mtego Kwa kijana wa miaka 14 ambaye Tyr alishamwaribu kitambo,akawa anamla mzigo kwenye gofu muda akitoka madrasa,kabla hajaanza kumshughulikia watu wakamzingira.Kilichomsaidia asiuawe ni Kwa sababu mshikaji ni wa hapo mtaani,akapigwa huku anakimbizwa polisi.

Kwa kifupi jamaa kawaharibu watoto wengi sn wa kiume pale mtaani,so sad

Now mwaka wa pili yupo nyuma ya nondo.

Niliona Fatma karume anatishia kumblock mtu huko Twitter kisa jamaa kamuuliza utafurahi kuona mwanao anakuwa shoga?.Kwa hiyo hao wanaojiita wanaharakati wanatetea lkn hawapendi watoto wao yawakute mambo ya aibu km haya.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kweli na akili zako timamu unaweza hata kuwasikiliza hao wanaharakati uchwara.

Wanahimiza mambo ambayo wao hawayafanyi wala watu wao wa karibu hawafanyi na wanajua ni mabaya ama yana matokeo hasi.
Ushoga sio jambo zuri hata kidogo, linaharibu kizazi cha mwanaume ambae ni shoga. Itafika kipindi hatokua na uwezo wa kusababisha mimba na hivyo kizazi chake kuishia kwake mwenyewe.
 
Kujifunz kupo kwa namna nyingi sana lakn tunavyoendelea kuupa nafasi ujinga nakudai n haki ya msingi ndio shida,
Kwa kuona
Kusikia
Kufanya
Kuiga

Japo hao wanadai homon , homon huw inachochew na vitendo mwenendo au Tabia (ni kama kipaji vle kam ulizaliw na kipaji huku kifanyia kaz ukubwan huwez kusema na kipaji cha mpira na ukasajiliwa)


This fucking business zitaigharmu jamiii na Taifa, miak hii tuwe makn san na kizaz chetu na watoto wadogo wasisome bwen au hostel lea mwanao

Ubakaji umeham kwa watoto wa kike umehamia kwa watoto wa kiume ambako uzalisha hawa Was****nge zaid Cr-kali hainamkazo kuwalind watoto wa kiume kama wa kike wanavyolindwa



Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Ujue hata huu msururu wa hizi nyuzi zinazo husiana na ushoga humu Jf nao unapromote ushoga.
 
Ujue hata huu msururu wa hizi nyuzi zinazo husiana na ushoga humu Jf nao unapromote ushoga.
huo ukimya wenu umesaidia nini na hali inazidi kuwa mbaya or with your little mind unadhani kuna mtu out there atakuwa shoga kwa threads za jf
 
Ilikua wazazi wanahofia zaidi juu ya malezi ya mtoto wa kike, ila kwa dunia ilipofikia mtoto wa kiume ni kiumbe cha kuchungwa zaidi hadi afikie kujitambua, so sad😒 .Mungu tulindie vizazi vyetu
 
Tatizo jamii imemsahau mtoto wa kiume.....

Mungu atulindie vizazi vyetu
 
Back
Top Bottom