Nawachukia sana WATANZANIA!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawachukia sana WATANZANIA!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kigarama, Feb 25, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sisi watanzania tunaendekaza sana ushabiki kwenye siasa na kuigeuza fani hii muhimu kuwa ni jukwaa la wahuni kurushiana maneno na kupiga porojo badala ya kuwa chanzo cha fikra jadidi za kutanzua matatizo yetu. Tumebobea kwenye kutabiri chama gani kitaibuka mshindi kwenye chaguzi huku tukiwa hatujishughulishi kabisa na jinsi wanasiasa hao walivyo na misimamo kwenye mambo ya msingi yenye faida kwa nchi yetu.

  Hata humu kwenye jukwaa letu tukufu la JF ni nadra sana kwa mada zinazohusu Uchumi au zile zisizo na ushabiki au kutaja majina ya watu tunaowapenda au kuwachukia kupata mapokezi yanayostahili. Hivi ni wangapi leo hii bado tunafuatilia nini kinatokea IPTL,Symbion,Buzwagi,NSSF,TRA,TICS na kwingineko? Na ndiyo maana siku hizi humu JF watu wamekuwa wazito sana kuchangia mada zinazoletwa na Mzee Mwanakijiji kwa sababu tu zinatutaka tutumie mbongo zetu wakati sisi TUMEBOBEA kwenye USHABIKI wa kuzifurahisha nafsi zetu!!

  Mwezi huu habari zitakuwa ni kuhusu Arumeru kama vile Arumeru ndiyo nchi nzima. CCM itapeleka viongozi wake waandamizi, CHADEMA nao hawatakuwa nyuma. Lakini ni wakati gani mwingine huwa tunawaona viongozi wetu hawa wa kisiasa wakiwekeza nguvu zao na rasirimali za vyama vyao kwenye shughuli zingine zaidi ya wakati wa uchaguzi?

  Nawachukia sana watanzania (mimi nikiwemo) kwa kupenda sana ushabiki na kuacha kushughulika na mambo ya msingi ya kisiasa yanayohusu nchi yetu.
   
 2. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unawachukia sana Watanzania, wanaokufurahisha ni watu wa nchi gani?
   
 3. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135

  Kusema unawachukia sana, naamini haijakutoka katika utashi wa kweli, tafakari vizuri!
   
 4. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,929
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  swali la msingi hili,nasubiri majibu yake ndo tujadili mada
   
 5. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu umeongea ukweli, sisi wa tz ni mbayuwayu tu, kama prezida wetu alivyotuita.
  I am pretty sure, kwa matatizo waliyotuletea hawa viongozi wa ccm, ilitupasa tufanye mass movement ya ku- over through this government. Lkn tumebaki kama mazezeta tu, tunawaacha hawa majambazi wanakomba kila kitu kilichopo mbele yao.
  Hata mimi nawachukia sana wa tz, we are not serious kuhusu nchi yetu.
  Tumekuwa watu wa kulalamika tu!
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kumchukia mtu flani si lazima umpende mwingine.
  Hii thread haizungumzii kumpenda mtu, inazungumzia 'uzezeta' wetu sisi wa tz.
  I am sure ukichanganya na za kwako utaelewa, kwani mbayuwayu wa ki tz mna upeo mdogo!
   
 7. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hujitambui bado ndugu kwa kuwachukia watanzania.Maana kila matatizo/kitu unachotaka kijadiliwe hapa kimesababishwa na siasa na bado hiyo hiyo siasa ndiyo inayoendelea kuharibu hivyo basi watu wengi lazima wapitie huko huko kwenye siasa kupambana.
  Au wewe ulitaka wapitie wapi kupambania haki zao zinazosababishwa na siasa/serikali ya nchi hii ambayo imeimeza mihimili mingine ya nchi kama Mahakama na Bunge?
  :juggle::juggle:
   
 8. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii ni kwa sababu Nchi ni Tajiri lakini Wananchi tu mafukara, tunawazawaza sana na kuendekeza njaa zetu, likitokea jambo la kuchukua hatua, tunawaza polisi wakinipiga risasi ntaendaje kupiga dili sehemu, watakula nini, mke wangu watapita naye wenye nazo, watoto wangu watasomeshwa na nani wakati mimi ndo wananitegemea, ntakufa kwa njaa maana bila mishe mishe bongo huishi, tunawaza mambo mengi sana wakati mwingine tunajifariji ujinga eti huu utajiri wa nchi siku moja lazima nitoke, kwanza hii kazi niipata kwa kuchakachua cheti pia tunawaza nafasi iliyopo inaniwezesha kula rushwa mpaka mshahara sijui kama bado unaingia benki!

  Mtu akisha waza hayo, huwezi kumuona anachukua hatua, wanaoweza ni wale waliojiajiri tena wanaofanya shughuli zao kwa taabu kama wamachinga. Lakini wengine wa maofisini labda waandamane kuisifia CCM kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kura rushwa na kufisadi pesa za umma!

  TTUKITAKA KUFANYA MABADIRIKO, tutathmini kama Taifa kule tulikotoka, tulipo na tunakokwenda kwa kulinganisha na nchi zingine na maendeleo ya Dunia kwa ujumla-TUACHE kufikiri mambo ya KIBINFSI-Tuone hapa tulipo sipo tunapostahili kuwepo! Tujiulize nani ametubakiza hapa-TWENDE TUKAMFUNDISHE ADABU full stop!
   
 9. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Huna hoja.Kwani uchaguzi si mwanzo wa maendeleo?
   
 10. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Nadhani ukichunguza kwa makini vyote ulivyoorodhesha hapo juu ni siasa tupu. Hata huyo mzee mwanakijiji hoja zake ni siasa tupu!

  Siasa ndiyo maisha, siasa ni maendeleo. Kama huwezi kujadili siasa bora usiishi!
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu mbona shallow sana
  Unafikiri Wahindi, Mafisadi baadhi ya wanasiasa wanaofaidika na mfumo, wanachuki kama wewe?
  La hasha.
  Mwisho wa siku angalia kile chako kinaenda vipi, tuliwacheka jirani zetu Kenya kuwa mnyag'au, MAN-EAT-MAN society, wanadundana lakini maisha yanaendelea mbele.
  Angalia mkate wako kwanza unaenda vipi.
   
 12. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Sioni cha ziada zaidi ya ile tabia yetu ya kuishia "kulalamika" tu bila kutekeleza..Utaishia kulalama viongozi wetu na wageni/wawekezaji wakijichotea resilimali zetu. Siasa muhimu....
   
 13. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Halafu kila hoja ya msingi ikiletwa watu wataihamishia kwenye malumbano ya siasa na kidini badala ya kutoa facts na opinion zao kulingana na hoja husika!JF inaelekea kuwa comedy aisee!Sijui wabongo tumelogwa?
   
 14. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Siasa zinaongoza maisha yetu kuliko baadhi yetu tunavyodhani.Mafanikio ktk maeneo yote mengine,kama vile uchumi, yanategemea kwa kiwango kikubwa ufanisi wa michakato ya kisiasa.
  Siasa (politics), kwa tafsiri ni "authoritative distribution or redistibution of scarce resources"
  Ktk mchakato wa utengenezaji wa bajeti ,mathalani ,bunge ndilo lenye jukumu la kujadili ,kubadilisha,kupitisha ama hata kukataa mapendekezo ya bajeti ya serikali kulingana na vipaumbele, matakwa na mahitaji ya wananchi.
  Tunapofuatilia michakato ya kisiasa, ikiwemo chaguzi mbalimbali, tunalenga hatimaye kuathiri michakato ya kiuchumi kupitia maamuzi ama maazimio yatakayofanywa na wanasiasa (wabunge) kwa kuwa bunge ,pamoja na majukumu mengine,lina play an oversight and advisory role na hili ni jukumu linaloweza kufanywa vyema na na watu makini, mahiri na wadilifu.
  Kwa kifupi,huwezi kupata ama kutarajia maendeleo ya kiuchumi pasipo kuwa na credible political processes.
   
 15. mjombo's

  mjombo's JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mi napita tuuuuuuuuuuuuu, huyooooooooooooooooooooooo,....................................................
   
 16. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,101
  Likes Received: 1,199
  Trophy Points: 280
  Siwachukii ndugu zangu wa TZ ila wananiboa sana. Sisi kila kukicha kazi yetu ni kushupalia tu viongozi badala ya kufanya mapinduzi nchini kama nchi za wenzetu tunaridhika na manyanyaso ya viongozi wetu na kila chaguzi tunawachagua viongozi wale wale. Chama Cha Majambazi (CCM) lazima kifanyiwe umafia kwani ni hawa ndiyo wanatulostisha sie watanzania. Toka tumepata uhuru 1961 mpaka hivi sasa hakuna chochote cha maendeleo huku majirani zetu wanapaa na kutuacha mbali. Miundo mbinu yetu finyu, utendaji kazi katika sekta zote ukiondoa NGO's finyu, umeme ziro, kilimo ziro, maadili ya nchi finyu. Sasa tujiulize; tunashupalia masuala ya vyama wakati wananchi wanateseka huku hawa viongozi wanatuibia tunapata faida gani? Hii serikali imesaini mikataba ya kishenzi hili wajinufaishe wao na familia zao huku watoto wao wakisoma nje ya mchina watoto wetu hapa TZ wengine mpaka leo bado wanasoma chini ya Mibuyu, je ni haki? Kikwete si mjinga kwani anaona vinavyofanyika lakini anajifanya kiziwi na kipofu kwa sababu kwa namna moja ama nyingine yeye pia ni muhusika mkubwa wa Wuxi wa Mali zetu hapa Tanzania. Hii nchi ipinduliwe na viongozi wataifishwe Mali zao la sivyo tutabaki kuwa wajinga wa kudanganywa kila siku huku majirani zetu wakitucheka. Ule uwongo Wa eti watanzania ni wapole ni ****** na umepitwa na wakati. Watanzania tuna hasira na we just don't care anymore, tunataka mabadiliko kwa njia ya mapinduzi.
   
 17. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Je kuwachukia watanzania ni jibu? Je wao wanakupenda? Naona wewe ni mtanzania. Kumbe unajichukia mwenyewe? Je chuki yako inajenga au kubomoa? Je chuki ndilo jibu wanalohitaji watanzania kuachana na hicho kinachofanya uwachukie?
  Je hii si ushahidi kuwa umeishiwa hata mawazo kiasi cha kuwekeza kwenye chuki? Heri kumpenda adui yako ili uweze kumbadilisha kuliko kumchukia naye akakuchukia mkaishia kumalizana bila sababu. Kaka au dada, jifunze kufikiri kwa faida badala ya kuendekeza chuki. Mie ni mtanzania. Ingawa unanichukia na watu wangu ukiwemo wewe, sikuchukii. Na laiti ningekujua vilivyo, ningetaka kukusaidia kwa kukukomboa toka kwenye ziwa la chuki. Badilika kabla ya chuki zako hazijaanza kukutafuna.
   
 18. A

  Ahakiz Member

  #18
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tumia lugha ya taifa swali la msingi ajibu anapenda watu gani? Mie nachukia wazungu sana na nawapenda watanzania
   
 19. yakowazi

  yakowazi JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 1,170
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  jamani KIGARAMA naomba usituchukie sisi watanzania wenzako***********
   
 20. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  cccm ndo walisababisha haya yote
   
Loading...