Nawachukia Sana mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania............!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawachukia Sana mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania............!!!

Discussion in 'Sports' started by Sajenti, Mar 2, 2012.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hivi tatizo lenu nini? ulimbukeni au ndio bendera kufata upepo?? Nimesikia leo asubuhi RFA eti mashabiki wa soka Dar waliamua kuandamana kushinikiza kocha wa timu ya Taifa ajiuzuru atafutwe kocha mwingine. Mi nadhani hawa watu hawana kazi za kufanya na huenda hata uwezo wao wa kufikiri nina mashaka nao...Eh!! Hivi kweli kwa mtu mwenye akili timamu kushindwa kwa timu ya taifa ya Tanzania linaweza kukufanya mtu mzima uache shughuli zako ukaandamana?

  Mi nadhani hayo maandamano yalitakiwa yawe ya kushinikiza uongozi wote wa TFF na Wizara ya Michezo uondoke madarakani mara moja. tatizo la kushindwa Tanzania katika medani ya soka jamani si kocha....jamani eh! Kwani tukijikwaa na kuanguka tunakimbilia kulaumu tulipoangukia badala ya kulaumu tulipojikwaa ambapo kumelekea sisi kuanguka?

  Hakuna kitu kinachonikera kama kuona TFF na huyo Raisi wake na wengine wanavyokosa ubunifu na hasa katika kipindi hiki cha utandawazi....Leo eti wana weka mashindano ya Copa Coca Cola mashindano yakiisha wanatajwa wachezaji wazuri waliochaguliwa sijui kunatokea jinamizi gani mwisho wa siku kila kitu ...kimyaaaaa!! Hivi Tanzania tunategemea kupata mafanikio bila ya kuwa na mipango endelevu kuanzia ngazi ya chini jamani? Hivi kweli hata leo akiletwa kocha kama Alex Ferguson, Pep Guadiola, Morinho ndio mafanikio yatapatikana? Mi nasema "NO"...Watanzania tunapenda mambo mazuri bila kuvuja jasho...hapa namaanisha mipango, gharama na kujitoa kikweli....Kwani akija Mbwna Samata au huyo Thomas Ulimwengu ndio nini?

  Juzi Clouds fm kwenye kipindi cha sports extra alihojiwa Zamoyni Mogella.alisema kitu kimoja kuwa wachezaji wa Tanzania kwa kizazi cha leo hawajitambuai, hawajui wajibu wao uwanjani, hawajitumi, wavivu na hawana malengo....Sasa hapo linaongezeka na hilo la TFF na Wizara ya michezo mbovu isiyo na mipango. Mtaandamana Sana na kubadirisha makocha lakini vichapo ni pale pale!!! wameniboa sana...:ballchain::smash:
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hilo nalo neno yaani hawa tff ndio hamna kitu kabisaa hiyo wizaro ipo kwa ajili ya posho tu mkuu sajenti
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..naona jamaa wamegeuza ka-mradi kao ka kujipatia posho za kuendelea kuishi mjini...bure kabisa!!
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,975
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 280
  Mpira Tz 0 kabisa.
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,457
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Tulichoweza ni kuwa ati BEST LOSERS......An accolade ambayo siipendi kabisa kuisikia
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  TFF ni kimaslahi mnooooo, hamna chama cha michezo ambacho kipo kwenye mrija wa pesa kuliko hao jamaa.

  Wanachojua wao ni kupeleka timu uwanjani wakusanye mapato tu!

  Nashangaa timu ya wasichana Twiga inafanya vizuri lakini hata hawaisaidii inakuwa omba omba!!!
   
 7. Mutta

  Mutta Senior Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuna mipango ya zima moto.Wale watoto waliokwenda Brazil wakachukua kombe la dunia kwa watoto wako wapi? Mipango mibovu.Kuna kiongozi mmoja pale TFF anapokuita kwenye timu ya taifa anataka 10% usipompatia huitwi wala hupangwi.TEGETE,KIGI,NGASA ndo waliipeleka Stars CHAN leo wapo nje.Sasa nguvu zote kwa Mademu,wanajituma kuliko Waume.Nchi yenye Wanaume takriba milioni 20 hatuna timu ya taifa?TFF Wajiuzulu hawawezi kazi.
   
 8. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndiyo maana mimi nimeamua kuwa mshabiki wa MANCHESTER
   
 9. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ni chelsea
   
Loading...