Nimetumia Nissan X-trail huu ni mwaka wa tatu sasa, na naweza kuwahakikishia ni gari nzuri sana. Ni low maintanance, na ukilitunza vizuri utadumu nalo. Tatizo la bongo ni kwamba mafundi wazuri wa Nissan ni wachache, wengi wamezoea Toyota. Wanaweza kukuharibia gari kama na wewe hujui kutafuta information. Gari yangu iliwahi kuharibika sensor ikawa inajizima nikisimama, nikauliza baadhi ya mafundi wa mtaani...mwingine akawa anadai tushushe gear box, mwingine engine, mwingine tubadilishe control box...kumbe hawajui kitu. Nikaingia google nikaandika hilo tatizo nikapata jibu kwamba ni sensor. Nikaenda CFA motors, pale nilimpata fundi wa Nissan akanielekeza kwenye gereji yake mtaani. Haikuchukua dakika kumi kubadilisha hiyo sensor, gharama 100,000 tu, na sasa ni miaka mitatu gari haijawahi kuguswa na fundi. Najitahidi sana kutafuta information mtandaoni kabla sijamuita fundi. Hivi karibuni gari ilikuwa inamiss, na inawaka kwa shida...nikaingia google nikagundua chanzo moja wapo ni plug. Nimebadilisha plug tatizo limeisha. Sasa binafsi siwezi kununua gari mkononi kwa mtu bila kujali aina, maana siwezi kujua alikuwa analitunza vipi. Ila kama matunzo ni mazuri X-trail ni gari mmoja nzuri sana.