Nautangaza uoga kama janga la Taifa

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,583
3,181
Nasema kwa uchungu wako wapi mashujaa wetu?

Waliopambana na Nduli Iddi Amin Dadaa mpaka akaikimbia Uganda!

Wako wapi mashujaa wetu walio simama mwembe yanga wakatangaza vita dhidi ya mafisango?

Sio hawa walio shindwa vita ya kisaikolojia toka siku ya kwanza na kuanza kunyea pajama suruali na kanzu zao?

Wako wapi akina Mkwawa,Isike,Chaburuma wa LEO.

Wako wapi mashujaa wetu waliopambana na vita vya kisaikolojia vya dunia, leo tunapigana wenyewe kwa wenyewe kwenye vita vya kisaikolojia kwa kisingizio cha kupolwa mada?

Sitaki kuamini kuwa hayo yote yanatokana na wewe kupolwa semi zako,sio wewe ulietusadikisha kuwa utakapofika pale,utaanzisha wimbo ule uliofichwa zamani wimbo wa uhuru wetu mpya dhidi ya wanyonyaji wetu,wimbo wa matumaini mapya,wimbo wa kutushikisha hatamu zetu upya.

Tukaanza mapambano tukikuunga mkono kwa dhati za mioyo yetu,ingawa ulituletea jemedari mpya toka kwa adui yetu,na ukatuaminisha kuwa utakapofika pale utamrejesha kwenye chumba cha maadiri akae na makungwi na baadae atatufaa kufungua chumba chenye funguo za minyororo yetu lakini bahati haikuwa yetu.

Juzi nikakuona unatuambia eti huyu mrithi wetu pale kwenye jumba letu amethubutu kufungua chumba cha minyororo na KUVUNJA maagano hivyo tutanyolewa bila maji.

Nashangaa mwenye minyororo yake kaja na kutubu ameshautupa wembe oliotuambia anataka tusemezane kama ndugu na atasaidia kutibu majeraha yetu.

kutokana na haya UNATAKA TUKUAMINI TENA?

ILA MIMI NAKUSHAURI RUDI NDANI UVAE NGUO MPYA UPATE KUJISTAHI KWA SASA UKO UCHI
 
19105603_463878947287711_3871826290824140888_n.jpg
 
HAKIKA MKUU WATANZANIA WENGI WETU NI WAOGA NA WATU WA KUSEMA PEMBENI PEMBENI
 
Back
Top Bottom