Nausikilizia mwili wangu Kama simu

Nausikilizia mwili wangu Kama simu

samamba oscar

Member
Joined
May 16, 2017
Posts
20
Reaction score
4
Watu wa Mungu bwana Asifiwe, salaam poleni na majukumu ya jpili.nilikuwa nahitaji ushauri wenu ndugu zangu kuhusiana na maswaiba yaliyonipata. Hi ni week yapili niliyopo kwenye hofu isiyo yakawaida na yakukata tamaa, IPO ivi week mbili zilizopita siku Kama ya Leo nilimtembelea mshakaji saloon,wakati nipo a po msela akanambia nimsaidie kunyoa yeye anaendakula.Alikuja Dogo mmoja mdogo wakati namyoa alikuwa na MBA na vidonda kichwani nikamkwangua Kikawa kinatoa damu kimoja,wakati nilipofikia kumchonga akawa analalamika namuumiza ikabidi niijaribu mashine kwenye mkono ili nivalishe jino gafla ikanikwaruza kidogo, sikuhisi chochote muda ule baada Dogo kuondoka nikaanza hisi maumivu Kwa mbali kwenye mkono kukagua Sana nikahisi kimkwaruzo kidogo ambacho huwezikukiona kiurahisi, sikuwaza kitu Kwa mdaule.ilipofika kesho yake nikaanza piga chafya siku nzima,nikaanza jipaadhabu nakumfatilia yule Dogo ukuaji wake nahistoria yake week nzima (tuko mtaa mmoja).Mama ake ni binti mzuri mweuupe shombe mnene.nikaanza kumbuka wakati najaribu ile Mashine Dogo alishika mdomo kamakushtuka.kilanikikutana nae anabadlisha njia nakukimbia.gafla week yapili Siku Kama yaleo nikaanza pata mafua(sijawahi umwa mafua ya mdamrefu hivi) na koo kuuuma,uchovu,misuli na mifupa kuuma kipele/kidonda kwenye lips ambapo nimedumu nahiyo hali hadi leo nimeamka asubuhi Leo nimetokewa na kipele kidogo kifuan chekundu kinachonga'a navingine vinaonekana Kwa mbali ambapomdawowote vitakuwa vikubwa,sijuhi kesho symptom gan ita develop ndugu zangu nme google sinahaja yakwenda kupima hiv,maana dalili zaawali Flu na Skin rushes maeneo yakifua nidalili za vvu Kwa 85% 1week mpaka 3week tokea kuambukizwa ni kwa kilamtuanayepata maambukizi.Siamini miaka 25ndoto zangu zimeishia hapa,Week hii nimetoka Pima na mpenzi wangu katoka nahappy ilamimi simanzi maana miezi mitatu ijayo majibu yangu yanaenda badilika.Nimemnyima sex nawala ajuitatizo nini sitakimuaribia life,uyu angekuwa mwanamke wa kwanza kusexnae maana siujui utupu wajinsia KE tokanimezaliwa labda kwenye pic ha/video,kujitunza kote huu ugonjwa umenifata Kwa njia nyingine naombeni msaada Kwa hasa wenyehuu ugonjwa jinsi yakuishi maisha mapya natembea huku machozi yanadondoka,mwili wote wa mazoezi umeisha nimekonda week hizi mbili nimebaki fuvu
 
Duuuh,,,,,,punguza hofu mkuu na huwezi kuamua lolote lile wakati huu umetawaliwa na hofu kuu
 
Pima kwa kurudia rudia upate uhakika,kuna magonjwa mengine yanatokana na hofu,hivyo ondoa hofu kwanza!
 
Fanya kama hakuna kilichotokea utakonda buree wakat pia haujathibitisha
 
Asante mi ni Rc Ila week hizi nimejisalimisha kwenye haya makanisa yakiroho Ila bado moyo wangu hauna Amani kabisa
Unafanya kosa kubwa sana kujidhani una HIV bila kupima. Situation kama hiyo iliwahi kunipata mimi! Ngoja nikuambie mkasa mzima. Nililala na mwanamke mmoja bila kutumia kinga. Baadae asubuhi nikagundua yule dada ana kovu kubwa mgongoni kama alama ya mkanda wa jeshi. Kumuuliza akasema aliungua. Na nikagundua zaidi kuwa alikuwa mwingi na mtembezi sana. Nguvu zikaniaishia. Baada ya miezi mitatu tumbo likaanza kujaa gesi na kuharisha. Haikuishia hapo nikapata na vidonda mdomoni. Nikaona tayari nimeshaukwaa. Nikaamua kwenda kucheki lakini kama mara nne nikawa nikienda wakati tuko kwenye foleni nashikwa na hofu na kuamua kukatiza zoezi. Nikawa naugua kadiri siku zinavyokwenda. Ikatokea siku moja nikaumwa sana sana. ie kuharisha, kutapika na homa kali. Ikawa sina tena ujanja. Nikaenda hospital. Dr akaniandikia vipimo kama full blood picture etc lakini hakuandika cha HIV. Matokeo ya full blood picture yakatoka na nikaonekana sina tatizo. Nikapata nguvu. Nikamuuliza dr hivi kama ningekuwa na HIV si ningeonekana nina hitilafu kwenye haya matokea ya full blood picture? Dr akasema ndio lakini vilevile unaweza usijue. Akanishauri nipime. Kupima nikakuta negative! Kumbe ni hofu tu ilinishika na nilikuwa na typhod! Ushauri wangu nenda kapime! Na hata kama una HIV hakuna neno. Siku hizi kuna dawa na waathirika wengi wanaishi maisha ya kawaida. Nina jamaa kama tisa nawafahamu walipima kama miaka 15 iliyopita wakakuta positive wakansa dawa na sasa wanaishi vizuri kabisa. Kuwahi ni kuzuri na utaishi life span ya kawaida kama utafuata masharti
 
Mawazo pia yanakondesha xo kapime uwe na uhakika, halafu vvu xo mwisho wa life. Mbona wanaish muda mrefu, mzima anaweza kufariki muda wowote na kwa sabab yoyote. MTEmbelee mwanasaikolojia kwa msaada zaid, pole xana mkuu uskate tamaa. Taifa, jamii na familia inakutegemea
 
Back
Top Bottom