Naunga mkono mia kwa mia,lakini.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naunga mkono mia kwa mia,lakini....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NEGLIGIBLE, Jun 17, 2011.

 1. NEGLIGIBLE

  NEGLIGIBLE JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  habari wana jamvi,hivi wabunge wote wanaochangia bajeti na kudai kuwa wanaiunga mkono bajeti mia kwa mia tena kwa msisitizo halafu wanaikosoa ni kwamba hawajui hesabu au wasiposema hivyo wataonekana wanaipinga serikali?..................nadhani umefika wakati wabunge wanapaswa kujua kazi zao,ambazo ni pamoja na kuisimamia serikali na sio vinginevyo...................
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wanaiogopa kura ya maoni itawamaliza wasiposema kumbe ndiyo wana haribu kabisa. Wewe ukitaka usionekane mpinzani ndani ya CCM msifie JK, msifei Spika halafu kandia sana upinzani lakini ukiruhusu tu akili yako ifanye kazi vizuri ni lazima utaona mengi ya kuongea na ndipo kura ya maoni itakapokuwa inakusubiri mlangoni! Wewe chunguza, utakuta mbunge wa CCM anaanza kwa utangulizi kama huu hapa chini:-
  Mheshima Spika nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia lakini awali ya yote napenda NIWASHUKURU MARAIS WOTE WA AWAMU NNE (04) kwa jinsi walivyojitahidi kuleta AMANI MAENDELEO nchi yetu. Zaidi ya yote rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete kwa kushinda ushindi wa kishindo na kuwaacha wapinzani wakilalamikia tume sijui kama wangekuwa wao wameshinda wangelalamika au? Hapo anapigiwa makofi na wenzake. Mbunge wa namna hii utafikiri hakuwepo kikao cha bunge kilichopita ambacho angalau hayo ndiyo yalikuwa mahali pake. Anaendelea,
  Mheshima Spika pia nikupongeze wewe mwenyewe binafsi kwa jinsi unavyoliendesha bunge kwa hekima na busara kubwa licha ya kuwepo miongozo mingi toka kwa wenzetu ambao ni sasa imekuwa ni kama jadi yao.
  Nikuombe uendelee kuwa na moyo huo huo wa kuwachukuliwa wenzetu CDM kwa jinsi walivyo. Wabunge wa CCM hapo ndiyo wanafurahi na kuona hizo ndizo point. Bado anaendelea,
  Mheshima Spika siku hizi bungeni kumezuka mtindo wa wenzetu kupinga na kuuhadaa umma, tabia hii ni mbaya inalenga kuichafua serikali dhidi ya wapiga kura wake. Mfano mzuri ni mauaji ya Nyamongo inatia aibu wabunge wenzetu kwenda kugomesha watu kuzika maiti kwa kejeli eti WAMEUAWA NA SERIKALI (Amesahau serikali ni organ na polisi wakimemo!). Anaendelea tabia hii si nzuri hata kidogo na inalishushia hadhi bunge.
  Atendelea na porojo sizizo na msingi mpaka akikumbuka yupo kwenye bajeti anarudi.
  Mheshima Spika kiukweli bajeti iliyowasilishwa juzi na waziri wa fedha Ndg Mkulo ni bajeti inahitaji KUPONGEZWA NA WADAU WOTE KWANI IMELENGA kutokomeza umaskini wa mtanzania. Bajeti hii imeanisha vipaumbele vingi ambavyo vikitelezwa vinalenga kumsaidia kabisa mtanzania wa leo kwa mf. punguzo la tozo ya mafuta (Amesahau mafuta yanaagizwa kwa USD na Tshs inazidi kushuka hivyo itaendelea kuwacost wafanyabiashara kuagiza mafuta). Anaendelea,
  Mheshimiwa Spika mimi nashangaa serikali yetu kunendekeza tabia hii ya kila kitu kutumia dollar katika malipo ya nchi (Amesahau Tshs imeshuka thamani) na hoja zinafanana na ujuha ujuha.
  Mwisho anaambiwa na spika, mh. mbunge muda wako umekwisha. Anaishia kumalizia Mh. Spika NAUNGA HOJA 100%.
  Lakini akisimama mbunge wa upinzani wa upinzaini akasema
  Mheshimiwa Spika, napenda kuwasilisha mchango wangu wa bajeti iliyoakilishwa kama ifuatavyo;
  Mh. Spika bajeti ilisomwa na waziri wa fedha Mh. Mkulo nadhani kila mbunge ameisikia lakini napenda nitoe baadhi ya mapungufu kadhaa ambayo yanaonyesha kuwa bado haijalenga kumukomboa mwananchi wa kawaida. Bajeti yenyewe ikisoma uk. wa... katika kitabu cha bajeti utaona kuwa Tshs ....trill zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya nchi, fedha hizi nyingi ni fedha kutoka kwa wahisani. Tabia hii ya kutegemea wahisani imekuwa ikizolotesha maendeleo sana hapa nchini licha ya kila mwaka kupitisha bajeti za maendeleo kwani KUTEGEMEA WAHISANI kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wahisani kutotoa fedha hizo kwa wakati au wakati mwingine kutotoa kabisa licha ya ahadi iliyokuwepo. Hii hupelekea miradi mingi kukwamia njiani au kutokwisha kwa wakati. Hivyo ni bora serikali sasa ikaacha KASUMBA ya kutegemea wahisani katika miradi ya maendeleo yake.
  Mh. Spika suala lingine ni bajeti ya kawaida. Kwa miaka mingi, nadadiriki kusema kuwa tangu tupate UHURU hakuna bajeti ya serikali iliwasilishwa ikiwa imebalance YAANI MATUMIZI NA MAPATO. Kwa hili ni aibu kwa serikali licha ya kuwa na amani na utulivu yaani tumeshindwa kufikia hatua ya kujitegemea kwa bajeti yetu wenyewe. Hii ni hatari hata kwa rais kwani hata kuwa na muda mwingi wa kutulia ikulu kufanya kazi za wananchi zaidi ya kukuimbilia nchi wahisani kwenda kuomba misaada na hii inathibitishwa na kauli ya rais kipindi fulani kuwa kama mnalaumu safari zangu basi mjue tusingesaidiwa na nchi ingekuwa na hali mbaya.
  Mh. Spika ifikie wakati nchi iwe na mikakati ya kueleweka ya kujitegemea kiuchumi kulingana na rasilimali tulizonazo. Ni aibu kwa taifa kama hili kuendelea kuwa tegemezi kwa miaka dahali na dahali licha ya kujaliwa rasilimali nyingi tu, na tuachane na tabia ya kusema kuwekeza kunahitaji mtaji mkubwa, hii inafanana na ile kauli If you think education is expensive then try igrorance, hivyo nasi kama tunafikiri kuwekeza ni gharama basi tusitegemee kabisa kuachana na umaskini uliotopea.
  Mh. Spika mimi nadhani suala la posho za wabunge ifikie mahali tuwaonee huruma wananchi. Kwa nchi maskini kama Tanzania kuendelea kuwalimbilizia wabunge na baadhi ya viongozi w serikali miposho mingi ni kama kuwahonga indirect vile ili waione na wasiikosoe serikali yao, rai yangu nashauri mishahara iimarishwe kwa sekta zote ili ilete impact kubwa kuliko ilivyo sasa na hii itaondoa hata umaskini kiasi fulani.
  Ataendelea na blalah blalah zake mwisho atamalizia SIUNGI MKONO HOJA.
  Unafiki unakuwepo kwenye KUUNGA MKONO HOJA TU na kusahau point zote ambazo mpinzani ametoa.
  ANGALIZO.
  Niliyoandika ni reflection ya baadi ya uchangiaji wa wabunge wa CCM na wapinzani wafanyavyo bungeni na hayo ni maneno yangu ya kubuni tu, sijamnukuu mtu yoyote.
  Nawasilisha.


   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ukoko sawia kabisa, nilisikia wabunge wakiwasilisha maoni yao yalifanana hivi hivi. Tena kwa ujinga ule ule wa wabunge wa CCM, **** fulani wakati anawasilisha akitamka tu "...hizi ndizo sera nzuri za CCM.." utasikia meza zinapigwa kwa kushangila! Umaskini wote huu kwa miaka 50 without economic significant changes fools are apprising nonesence!

  Kwa ujumla kinachowatia hasira watnzania waelewa ni kuwa "Kwa ujumla hatua ya maendeleo tuliyopiga hailingani na miaka 50 ya uhuru kwa rasilimali tulizonazo full stop!"

  Sasa hivi tungekuwa kama Botswana, tusingekuwa tunazungumzia shule za kata, ujenzi wa barabara za Taifa na Mikoa, zahanati za kata, njaa, mauaji ya wananchi, posho za wabunge nk.

  All these SHAME ON CCM Government!
   
Loading...