Naunga mkono mgomo wa walimu

Waalimu acheni unafiki wa kuamua mambo yanayohusu maisha haiwezekani mwalimu wa degree anamshahara sawa na nesi wa certificate wanaishi nchi moja, mkoa moja, wilaya moja , kata mmoja na kijiji kimoja wananunua vitu kwa bei inayofana .HUU NI WAKATI WA KUAMKA AMASIVYO WASEME MADACTARI WANASHERIA NA WENGINE WAMEFUNDISHWA NA NANI? NAUNGA MKONO MGOMO.
 
NIMESOMA HOJA NYINGI inaonesha walimu hawawezi kugoma! Basi waheshimiwa walimu, msigome maana serikali IMEFULIA haina kitu nasikia hata wabunge wameshauriwa kutoagiza mashangingi. Hata politicians nasikia wamepunguza ZIARA za kwenda kununua hirizi india, wananunua nchirizi na ulozi wa bei nafuu wa bagamoyo. Wanavaa hirizi ambazo ni Made in Tanzania.
 
Wenzetu waganga wametangaza mgomo kesho 23/6/2012. Je sisi walimu lini? Au ni mgomo wa mdomoni tu! Maana sisi kwa midomo tuko juu. Walimu kugoma ni ngumu kama ilivyo ngumu ccm-magamba kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2012)
 
mimi ni mwalimu na nimejiandaa kugoma siogopi kutishiwa kufukuzwa kazi kwa kuwa nazijua haki zangu, ni kweli walimu wengi hasa wale wa msingi nyeti vyao ni vya kusadikika hasa wale wa miaka ya nyuma kidogo hao ndio wanaoweza kutuangusha lakini wale wengi wa sekondari naamini tutakuwa nao pamoja, mungu jalia hili lifanikiwe ili serikali ijue dharauo kwa watu wanaowakata kodi bila kelele soi nzuri
 
Wakati umefika sasa wa serikali kusikia kilio cha walimu cha miaka nenda rudi. Nakubali kwa asilimia zote kwamba walimu nao wagome. Haiwezekani mwalimu wa degree alipwe sana na mwenye certificate katika kada zingine! Hapana enough is enough! Solidality forever.

kwa walimu haiwezekani kugoma.
 
Hakuna watu waoga kama waalimu. Hawataweza kugoma.

Hilo ni neno Mkuu hawana umoja kama madaktari, wana mibwabwajo mingi lakini ikija kwenye vitendo ni ZERO, ZILCH, SIFURI
 
Walimu serikali ya CCM imeishawafanya ndondocha hawana kitu ni wasanii tu wameridhika na wanachopata kila siku tutagoma halafu ugomi sasa ni nini kama siyo usanii. Sina imani na walimu kwa sababu ndiyo wanailea serikali ya MAGAMBA. Big up madaktari huwa hawabeep
 
Walimu serikali ya CCM imeishawafanya ndondocha hawana kitu ni wasanii tu wameridhika na wanachopata kila siku tutagoma halafu ugomi sasa ni nini kama siyo usanii. Sina imani na walimu kwa sababu ndiyo wanailea serikali ya MAGAMBA. Big up madaktari huwa hawabeep
mwalimu wa juzi sio sawa na waleo, hebu fikilia ni walimu wangapi wameajiriwa miaka ya karibuni ambao ni vijana? kama CHADEMA imepata kuaminika na kusambaza fikra za kimapinduzi siku chache tu sembuse walimu? kwani walimu ni kina nani mpaka washindwe kubadilika kifikra? naamini walimu watagoma na matunda tutayaona. MUngu wabariki WALIMU watanzania.
 
Walimu serikali ya CCM imeishawafanya ndondocha hawana kitu ni wasanii tu wameridhika na wanachopata kila siku tutagoma halafu ugomi sasa ni nini kama siyo usanii. Sina imani na walimu kwa sababu ndiyo wanailea serikali ya MAGAMBA. Big up madaktari huwa hawabeep

fikra zinabadilika ndugu, mwalimu wa jana sio wa leo.
 
Inawezekana mtoto wako yuko Stnini si wenzio kwa akina Kayumba wakigoma imekula kwetu 1 kwa 1
 
mimi ni mwalimu na nimejiandaa kugoma siogopi kutishiwa kufukuzwa kazi kwa kuwa nazijua haki zangu, ni kweli walimu wengi hasa wale wa msingi nyeti vyao ni vya kusadikika hasa wale wa miaka ya nyuma kidogo hao ndio wanaoweza kutuangusha lakini wale wengi wa sekondari naamini tutakuwa nao pamoja, mungu jalia hili lifanikiwe ili serikali ijue dharauo kwa watu wanaowakata kodi bila kelele soi nzuri
mkuu ndoto zako zitaisha asubuhi uatashangaa kumekucha na hakuna hata harufu ya mgomo

huo unao uita mgomo nani atakaye uitisha ?? utanza lini ?? sababu ya mgomo ni nini ??

nakumbuka kuna kipindi mgomo ulikuwa hot na tarehe ilipangwa lakini JK aliuzima walimu wakawa hoi

kwa taarifa yako kama walimu wa shule za msingi wataamua kugoma serikali lazima itajali lakini si ninyi wa sekondari chini ya CWT nasikia kuna chama kipya kinafuta usajli kinaitwa UMET - Umoja wa Maafisa Elimu Tanzania labda hicho kinaweza kuwa na msimamo kuliko hawa CWT ya sasa

kwa maana hii mgomo wa kweli utawezekana hadi hapo UMET itakapo pewa usajili wa kudumu
 
Walimu kugoma wanaweza na wana kila sababu.Wakitaka kugoma kwa mafanikio wagome kikanda yaani wagome Walimu wa Singida peke yao,Arusha peke yao,Kigoma peke yao,Lindi peke yao n.k.Madai yao yanaweza kuwa tofauti ila kubwa ni mshahara mdogo na posho kuwa hakuna.Pia Wakuu wa shule kuamua hatima ya Walimu kwa utashi na manufaa yao mfano kama haujipendekezi kwao hupati nafasi ya hela.Pia kuna ukabila mkubwa sana Wilaya ya Iramba wa Afisa mmoja kuweka Wakuu wa shule wa kabila lake na wakiharibu shule hawafanywi chochote.Pia Kilombero kuna kujuana kupita kiasi ambapo ndiyo wilaya inayofanya vibaya sana kimasomo ila Wakuu wamewekana na hawawajibishwi ingawa wengi wao wameshindwa kazi.Hali ya matatizo ya Walimu ilivyo ni taswira tosha ya hali ya Watanzania.Tusiwalaumu Walimu kuwa ni waoga siyo waoga ila mpangilio wa madaraka ndiyo unaowaumiza.Wakuu wamewekwa kiswahiba hivi Mwalimu gani atakuwa tayari kusimama peke yake kutetea maslahi wakati Mkuu wake hataki kugoma eti yeye yuko upande wa Mwajiri.Hivyo ili Walimu wafanikiwe katika madai yao hawana budi kudai madai yao Kikanda na Wakuu wao nao waungane kwenye huo mgomo wasitegemee kugoma nchi nzima kwa sababu mawasiliano ni magumu na pia ugumu wa maisha unatofautiana miongoni mwa maeneo ya Tanzania.Huwezi kulinganisha ugumu wa maisha Iramba na Igunga.Igunga kuna unafuu.Kingine kinachowafanya Walimu washindwe kuwa wamoja ni utofauti wa Elimu yao,madaraja na kukosa moyo wa kizalendo wa kujali kizazi kijacho.Ukweli uliopo Walimu wengi wako kwenye mgomo wa chini kwa chini kwa muda mrefu hawafanyi kazi kwa moyo na kujituma.Wengi wanafanya mambo yao ndiyo maana elimu inazidi kuwa duni kwa Watanzania.Ikiwa Walimu wanafunzi wa UDSM,UDOM NA SUA WANAWEZA KUGOMA WALIOKO KAZINI WATASHINDWAJE?Serikali inayojali maslahi ya Watanzania itasikia kilio cha Walimu.
 
Mchawi wa migomo ya walimu iliyoshindwa ni
1.0. C. W. T
2.0. Walimu wa msingi

1.0.1
C. W. T hawana nia ya dhati ya kuendesha mgomo wenye mafanikio maana viongozi wake wengi wako pale kama mapandikizi na mawakala wa chama tawala.
Teaching allowance ilifutwa mara baada ya kuundwa kwa C. W. T, jiulize kwa nini hawakukomaa palepale isifutwe wameacha ifutwe kwanza ndio waje wadai kuirudisha?

1.0.2
C. W. T wamekaa kideal deal kuliko kusimamia maslahi ya wanachama wake kwa dhati ya kusimamia. Jiulize michango wanayo katwa wanachama halafu jiulize juhudi na ukaribu wa cwt kufuatilia matatizo ya kila mwanachama, mfano kupandishwa madaraja, kudai malimbikizo na stahili nyingine, kama jinsi wanavyokata michango yake mwisho wa mwezi. Je kuna uwiano?

2.0.1
walimu wa msingi wengi ni kikwazo kwa kuwa wengi wameingia ki magumashi kwa vyeti vya watu. (Kumbukeni sakata la eckernforde na chuo cha kange) walimu makanjanja Kugoma, kwao itakuwa ni sawa na kujiingiza kwenye mdomo wa mamba.

Ili mgomo ufanikiwe.
Walimu walimu wa sekondari wajipange wapige mgomo wao peke yake. Period
 
Hilo ni neno Mkuu hawana umoja kama madaktari, wana mibwabwajo mingi lakini ikija kwenye vitendo ni ZERO, ZILCH, SIFURI

Mkiamua kugoma gomeni na muwe tayari kwa lolote,lakini mnapogoma bila ya kuwa tayari kukabiriana na hali yoyote itakayotokea dhidi ya uamuzi wenu hamuwezi kufanikisha mgomo. Wanasiasa (ambao wengine ni walimu kitaaluma) hawawezi kutekeleza matakwa yoyote bila msukumu thabiti toka nje. Walimu wekeni kunji la uhakika na mtaona mambo yenu yanaanza kutekelezwa. Kwa nini huwa mnaogopa sana harakati na kuishia kutamani kugoma bila ya vitendo? Kujifanya na mgomo baridi ni kuathiri wasiohusika, na madai yenu hayawezi kutekelezwa kwa mgomo wa siri (eti mnauita baridi), weka kunji mambo yaeleweke!!!!!

 
Back
Top Bottom