Naunga mkono mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naunga mkono mgomo wa madaktari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The secretary, Mar 5, 2012.

 1. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Watanzania tumezoea kutowawajibisha viongozi mtu anavulunda anajua miaka mitano ikifika anachapa lapa huu mtindo waliohuanzisha madaktari wa kuwawajibisha utaleta mabadiliko badala tusisubiri hiyo miaka mitano hii ni kwa manufaa yetu
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja
   
 3. k

  kaeso JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siungi mkono hoja, tutafute namna nyingine ya kuwaadabisha hao viongozi na sio hii ambayo raia wa kawaida ndio wanaumia.
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nami naunga mkono hoja, hawa mawaziri wetu wanatupeleka bora liende wanajua miaka 5 yao itaisha hakuna wakuwasumbua wapo kimaslahi binafsi na sio ya umma, wangekuwa waungwana wangejiuzuru kwa yaliotokea sio hao wa afya hata nishati na madini pia wajifunze toka kwa mataifa mengine hata watani zetu kenya na uganda wana mawaziri wanajiuzuru pindi linapotokea tatizo linalogusu jamii na taifa, hii ndio inatakiwa watanzania nao wajifunze
   
 5. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  namna gani ya kusubiri hiyo miaka mitano halafu apite tena kwa ulaghai wa kula
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu wajua 2015 ndio mbali kabisa sijui kama unatambua hilooooo.


   
 7. T

  Twaa Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu KAESO huoni hata aibu kwa maneno yako? Hivi wewe ulishawahi kulazwa au kuuguza mgonjwa hospitalini? Kama umeshawahi basi wewe unafaa uitwe mtu mwenye poverty mentality!
  Kwangu mimi naunga mkono mgomo wa madr!
  Kumbuka ''haki haiombwi wala hainunuliwi bali inadaiwa'' . Mie naunga mkono hoja ya mgomo wa madr!
   
 8. M

  Mashroud Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisifuye mvua imemnyeshea. Siungi mkono hoja. Ndugu yetu amepoteza mtt wake kwa ajili ya huo mgomo. Mazungumzo yafanyike sio mgomo.
   
 9. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Unajua ili ufanye maamuzi sahihi inabidi uwe na taarifa sahihi. Naomba kumwuliza mleta mada, asume kesho aubuhi unapata Ajali mbaya (Mungu epushia Mbali) unavuja damu kwa wingi, tumekubeba kwenye machela mbio Muhimbili, tunakuta Madokta wamegoma anakuja Mwandishi anakuhoji, Je utaunga mkono Hoja?
  'Usiombe kukutwa na huu Mgomo'. Hauwawajibishi viongozi bali wananchi wa kawaida.
  Mungu epushia mbali huu Mgomo. Amina.
   
 10. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,851
  Likes Received: 1,288
  Trophy Points: 280
  Siwaungi mkono.
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,058
  Likes Received: 6,505
  Trophy Points: 280
  la sasa kali mmmh, sijui,
  nina baba mdogo kalazwa huko muhimbili,
  sijui tuanze kumhamishia hosp. nyingine,
  but haki ni lazima ipatikane.
   
 12. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,232
  Likes Received: 817
  Trophy Points: 280
  hebu suggest an altetnative method which you think is better
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono mgomo wa Madaktari

  Matokeo yasiyo kusudiwa ya mapambano ya kuleta hali njema ya ustawi wa jamii ni azima yaambatane na kafara.

  Katika mapambano haya ya kuleta usitawi wa huduma katika tiba ni dhahiri kwamba wagonjwa ndiyo watakao athirika.

  Lakini pia ikumbukwe kwamba katika mazingira ambayo Dr hana vifaa vya kufanyia kazi,mazingira mabaya na uongozi mbaya ni wagonjwa ndiyo hutolewa kafara.

  Wengi wetu hapa hatujui idadi ya watu wanao kufa kila siku pale Muhimbili kwa kukosa Drip la maji, right medicine na usafi utokanao na ukosefu wa maji.

  Ni wagonjwa wengi sana hufa kwa kukosa huduma muhimu na za lazima kutokana na ukweli kwamba Bajeti ya Muhimbili hutumiwa kifisadi na viongozi Wizarani kujikimu katika ubinafsi wao.
  Madaktari tofauti na kada nyingine nyingi wana uwezo kimizania kuiweka serikali ya CCM katika kilenge na hata kuilazimisha kutekeleza yale ambayoni wajibu wake kutekeleza.

  Ni haki ya kuzaliwa ya Wananchi wa Tanzania kuunga au kupinga chochote kile wakitacho, akini katika kupinga au kuunga mkono kwao ni lazima wawe tayari kubeba matokeo ya muda mfupi na ya muda mrefu.

  Matokeo ya muda mrefu ya kushindwa kuunga mkono mgomo wa madaktari yatakuwa kuendelea kuzorota kwa huduma za afya nchini Tanzania hadi kufikia katika kiwango ambacho kutakuwa hakuna tofauti kati ya kuwa katika Mhabusu ya Polisi na Wodi ya Mwaisela.
  Matokeo ya muda mfupi ni kuendelea na hali iliyoko huko Muhimbili ambapo wagonjwa wengi hufa na idadi yao hubaki kuwa Takwimu katika vitabu huku familia nyingi zikiingiwa na majonzi na misiba inayolazimisha na ufisadi wa serikali ya CCM
  Asilimia inayokaribia nusu ya Watanzania ni waoga sana katika kudai haki zao kiasi kwamba wanatamani wawe katika hali ya ufu ili waweze kudai haki zao.

  Hali ya Kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni tuliyonayo sasa hivi nchini Tanzania haiwezi kutupeleka popote pale kimaendeleo mpaka tutakapo amka katika usingizi wetu mnono wa kifukara na kupambana na serikali ya CCM katika lengo la kuing'oa ili kujenga serikali mpya yenye safu ya viongozi wanao wajibika kwa wananchi wa Tanzania.

  Kwa sababu serikali ya CCM ina Polisi UWT na JWTZ kibindoni mwake mapambano haya ya kuhakikisha inaondoka madarakani ni lazima yawe magumu kwetu wapambanaji,serikali ya CCM ni lazima ni lazima itatumia uvunjaji mwingi wa sheria na haki za binadamu ili kuhakikisha kwamba inabakia madarakani.

  Hatuna Mjomba,shangazi wala kaka mahali popote nje ya mipaka ya Tanzania aliye tayari kupambana kwa niaba yetu. Ili kujikomboa kutoka katika Makucha ya serikali ya CCM ni lazima kabisa kuanzish mapambano katika shughuli zote za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii nchini Tanzania.

  Madaktari wameanzisha mapambano katika shughuli za kijamii wale wote wenye upeo 2020 wataunga mkono mapambano haya yenye nia ya kurudisha heshima ya kila Mtanzania.

  Naunga mkono Mgomo wa Madaktari.
   
 14. B

  Bettina Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muhimbili yenyewe iko juu ya mawe, haina kitu - si madawa ya dharura, mashine za kuuwa wadudu kwenye vifaa, oksijen etc, ukipelekwa Muhimbili ukapona ni Mungu wanko na sio hao madaktari makarani wanaoishia kuandika yaliyokusibu ilihali hawana vifaa vya kukuhudumia. Hapo ni hospital ya taifa, je hali ikoje huko mikoani, wilayani ambapo 95% ya ajali za TZ ndiko zinakotokea? Hata nyuzi za kukushonea huo mshipa unaomwaga damu hawana! Tafakari!
  Naunga MKONO MGOMO wa Madaktari mia kwa mia, tena mmechelewa sana. Na walimu pasheni moto injini, you are the next. Nadhani tuwaachie polisi tu ambao tukiandamana kupigania hali duni ya maisha(incl ufukara wa polisi), wao wanatupiga mabomu na virungu!!!
   
 15. m

  moshingi JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuunga mkono mgomo wa madaktari; mtanisamehe kwa tafsiri yangu, ni sawa na Ugaidi, Ukaburu, Ush***zi, Use**ge wa kupindukia!!!! Wanaoathirika na mgomo huu siyo akina Pinda, Mponda, Nkya, Kikwete, Slaa, Mbowe, Lipumba, Seif,Magufuli, Mwakyembe, Rizi-1, wala wengineo wa tabaka hilo... endapo kama ule mgomo uliopita ungewagusa wangekuwa wamesalimu amri...lakini wanajua hata kama ma-dr wakigoma kwa miaka yote-5 mfululizo, hawataathirika hata kidogo...sisi walalahoi tu ndio tunaathirika... Ni bora MAANDAMANO mara elfu moja huwa wanayaogopa, pia hayawaui walalahoi kwa wingi kama mgomo wa ma-dr. SIUNGI MKONO KABISA MGOMO WA MA-DR.
   
 16. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu wakiandamana wanaletewa polisi na maji ya kuwasha, kumbuka polisi wetu hutumia nguvu za ziada ikiwemo risasi......kuna hospitali ya mkoa haina chumba cha upasuaji, pesa hakuna ila za kuhonga Arumeru zipo na rais kusafiri zipo. Hapa daktari akigoma unalaumu? Huyo mgonjwa anayehitaji huduma ya dharura ya upasuaji daktari amfanyaje? Bora akae nyumbani kuliko kuja kuangalia wakifa wagonjwa kwa huduma duni.
   
 17. d

  dav22 JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  naunga mkono kwa asilimia 100
   
 18. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  tatizo lenu mnaotupinga u dont have to face the hardship we face...umeshawahi kuangalia mtu anapoteza maisha mbele ya macho yako kwasababu tu vifaa fulani vimekosekana?nyie mnafikiri tukifiwa na mgonjwa kwaajili ya uzembe tunafurahia?msiongee tu kwasababu mna midomo but fikiria matatizo tunayokutana nayo tukiwa kazini halafu serikali inashindwa kuwajibika huku kila siku viongozi wanaidhinisha matumizi mabovu ya kodi zetu
   
 19. P

  Papaya Senior Member

  #19
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mazungumzo gani unaona yanaweza fanyika ukapatikana muafaka? bora madaktari wagome tena kazeni buti haswaaa mpaka kieleweke.
   
 20. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Madaktari wakigoma, wanaoumia ni wananchi wapiga kura. Madai ya madaktari yanagomewa na serikari iliyoko madarakani, na inayotaka iendelee kuwa madarakani na viongozi wake wa ccm hata kama wameshindwa kutenda kazi zao kwa ushabiki wa anayewateua.
  Mgomo utawaathiri wapiga kura, ambao ndio wanaendelea kuikumbatia serikari iliyogoma kuboresha maslahi na hali za vifaa na mazingira ya kazi ili kutoa huduma za afya zilizo bora.
  Mgomo utawalazimisha wapiga kura kuiacha serikari iliyo madarakani na kuinyima ushirikiano ili iweze kujirekebisha na tabia ya viongozi wenye uchu wa madaraka na wasiokubali kuwajibika kwa makosa wanayofanya.
  Mgomo ni sawa.
  Viongozi wetu na watoto wao wanatibiwa nje ya hospitali zetu.
  Pinda pia anapaswa ajiuzuru na mawaziri anaowang'angania.
   
Loading...