wadau habari zenu ..... mi nina shida moja napenda kuangalia mpira ,....shida ni kujua kingamuzi gani cha bei nafuu nijiunge ili niweze kupata Chanel nzuri za mpira na movie tofauti na dstv ....au cable gan nzuri nijiunge ..... kwa tabata , dar es salaam. .....
asanteni jamani
Kwa sasa naweza kukushauri Receiver ya DVB-S2 yenye uwezo wa kuingiza BISS keys
Kwa kariakoo utaipata kwa thamani ya chini kabisa 80,000/=
Hii itakusaidia kukamata channel zile za Kiarabu Irib TV3,Irib Varzesh ambao wanaonesha soccer la ulaya lakini kwa lugha ya kiarabu fulani hivi maana ni Channel za Iran
Itakudai dish kubwa 6ft na kupanda juu approxmately bei yake ni 120,000/=
uKiikubali hii dili ntakusaidia kupata contentz za hizi channel
Pia kuna decoder ya Champion TV HD receiver inazo channel kuu mbili Redlight HD(Adult channel) na Champion TV ambayo inaonesha mpira wa ligi kuu za uingereza kwa lugha ya kizungu.
Kwa sasa zinauzwa Ghana na baadhi ya maeneo ya Nigeria zimefika,kama una ndugu hayo maeneo fanya makeke upate mzigo huo
Last but not least,Ningekushauri pia kufanya Research wapi upate boxes zenye IPTV au WEB TV kwa ajili ya kustream,hapa nakushauri ufatilie mabox yenye contents ambazo ni Premium maana huwa channel zao ziko optmized kutoitaji net ilo fasta sana yaani hata kwa 3G ya mitandao yetu unaangalia ligi zako bila shida yoyote.
Mfano kuna mdau wangu kanitumia site moja yakulipia lakini bado naifanyia research ila kiukweli iko poa na stream nayo kwa net ya Tigo at a satisfactory rate