Nijuavyo mimi kwa upeo wangu kidogo ni kwamba mambo mengine unaweza kupata kuyafanya na kuyajua unapotembelea eneo fulani...mfano unaweza kujifunza vizuri na kwa undani ni jinsi gani Japan wanafanya mambo yao kuleta maendeleo endapo utapata fursa ya kufika hiyo nchi
Sasa swala la kufuta kabisa safari za nje m sioni kama ni jambo la kushabikia moja kwa moja nadhani ilikua kuondoa safari zisizo na tija lakini zile zinazotoa fursa ya mtu kupata elimu ya maendeleo ziwepo..
Jamani mi nisaidieni napata tabu sana kusikia safari za nje kwa viongozi zimefutwa au kuna kitu kinakwepwa?
Safari zimesitishwa mpaka muongozo mwingine utakapotolewa,vibali vya safari vitatolewa baada ya kupima umuhimu wa safari yenyewe tunatakiwa kuelewa mambo machache tu kwamba safari nyingi zilikuwa hazina tija.....Hina tija kabisa, nini mnachoenda kujifunza? Maoni yangu ni safari zote zisizo na tija zifutwe, pia semina sisizo na tija zifutwe, hivi vi mbinu vya kugawiana allowances yaani amalize kabisa watu wanakufa kwa kukosa dawa maospitalini alafu bado mnatetea safari za kijinga.